Mafuru wa VodaCom kuwa CEO mpya wa TTCL?

jamaa ni kichwa huyu nimefanya nae kazi pale voda... na mpka naondoka pale yule jamaa yuko fiti

sina uhakika kama anapewa cheo kwa kigezo hicho ulichosema mleta mada

TTCL ni zaidi mno ya marketing. Anatakiwa mtu mwenye credentials zilizokamilika
 
Kumekuwa na threads nyingi zinazoonyesha kwamba Mafuru anawekewa njia kuwa CEO wa shirika moja la Umma. Ninachofahamu ni kwamba kama mkuu wa masoko wa Vodacom tulitarajia kuona amefanya kazi nzuri katika ushindani huu wa Mobile services Operators.

Performance ya Vodacom imekuwa ikidorora kutoka mwaka hadi mwaka. Na yafuatayo na matokeo ya Vodacom kwa miaka mitatu kwa faida kabla ya kodi.

Mwaka unaoishia:
31.03.2008 = Shs 54 billion
31.03.2009 = Shs 55 billion
31.03.210= hasara 9 billion

Mafuru ameshindwa kuweka mikakati mahususi ya masoko kuiwezesha vodacom ku- compete na tigO na Zain. Nadhani ameanza kujipendekeza kwa JK ili ahamie kwenye siasa maana pale alipo amekalia kuti kavu.

Kwa kweli hawezi kuleta Tija. Nadhani jambo la msingi ni kwamba akaajiriwe na H Lundega aendelee kumsaidia kusaka vidosho wa miss tz mitaani, namaanisha wale mabinti wanaopenda kuanika mapaja yao nje.

jamani watu fungueni pingu mlizojifunga kwenye fikara ili muwe huru kuchambua mambo. Mnashindwa hata kuweka mpaka kati ya Marketing Functions na overal corporate performance! Mnasahau au mnafanya Maksudi kutotoa credit ya mchango wa Mafuru kuifanya voda The E.A Superior Brand kwa miaka kadhaa mfululizo hadi mwaka huu CRDB iliponyakua taji! Na mara zote ni Mafuru amekuwa akilipokea na kupongezwa kwa kuiwezesha voda kushinda. Nidokeze pia kuwa kupima ufanisi kwa kuangalia namba ulizotoa unapelekea kwenye hitimisho lisilosahihi. Hujataanabaisha ktk kipindi husika kampuni imefanya uwekezaji kiasi gani kutokana na faida, imetafiti, ikatengeneza na kuingiza huduma (3G, M-PESA, etc)/bidhaa mpya ngapi sokoni n.k haya yote ni mambo yanayoweza kufanya figure ionekane kwa sasa inashuka kumbe marejesho makubwa yametegwa mbele.
 
Kijana wa POND kwa mzee wa shamba, muhogo kwa uji!, mwacheni apae. Ni kazi na uwezo wake ndio unamfikisha hapo....msiletee zenu za kifisadi fisadi.

Bahati yake jamani, maana mwaka jana aliikosa ile post ya ukurugenzi pale utalii kumrithi babu wa tanga. hongera baghosha ng'wana wane, matunda ya pugu hayo, au siyo
 
Jamaa anafaa, lakini ajaribu kuondoa mnato ingawa naamini ni hulka ya kuzaliwa wakati mwingine. public post inahitaji kuwa social, vinginevyo nafasi inaweza kukushinda, hasa kwenye sekta ya umma ambako masufuria na majungu ni mambo ya kawaida. usije ukasikia "wee mtoto, siye tuko hapa tangu 1977, usilete sera zako za kwa Mafisadi hapa!"
 
Wana JF kuna hizi tetesi mwenye data kamili atuthibitishie

Wakina R.A and E.L at work wanataka kuweka mtu wao waje wajiuzie watakavyo au waifidisi TTCL hadi ife kabisa maana hata sasa hivi ipo ICU.
 
Ha ha ha katika ile team ya uchakachuaji kwa kutumia mashine, kuna mwakilishi wa VODA. Connect the dot of shareholders!!!! Katibu wa Chama!!! na role ya Vodacom generally kwa uchaguzi huu hasa masula ya ile michango ya CHADEMA Vs CCM!! Tanzania hii, nchi nzuri ila inaharibiwa na wajanza wachache. Sipingi Mafuru ni kichwa bali najali tu asije akaacha kazi yake nzuri kwenda kubeba marehemu TTCL.
 
Mafuru anaweza kufanya kazi nyingine lakini sio u CEO wa kampuni. kwani kuwa CEO unahijika kuwa kichwa hasa na mwenye vision...tangia aanze kazi pale vodacom hajawa mtu wa maamuzi bali ni mshehereshaji je hilo linatosha kuwa CEO? Pili huyu alipata div 3 PCM pale pond akashindwa kwenda ud direct...alienda kuboresha matokeo CBE ndo akajiunga UD kusoma Bcom.....
 
Mafuru anaweza kufanya kazi nyingine lakini sio u CEO wa kampuni. kwani kuwa CEO unahijika kuwa kichwa hasa na mwenye vision...tangia aanze kazi pale vodacom hajawa mtu wa maamuzi bali ni mshehereshaji je hilo linatosha kuwa CEO? Pili huyu alipata div 3 PCM pale pond akashindwa kwenda ud direct...alienda kuboresha matokeo CBE ndo akajiunga UD kusoma Bcom.....
Lakini akiwezeshwa si anaweza
 
huyu si yego , kwani huwajui Yego wewe ?

ananata ?labda siku hizi mbona primary na sec alikua social sana .kipindi naingia sec nikabahatika kupangiwa room mmoja naye .kipindi hicho nko kinda sana.mafuru alikua katibu wa serikali ya wanafunzi yani secönd in comand after mwenyekiti.
Lile geto likiitwa ikulu hamna denti alitugusa kutuharasi.
Vilevile jamaa alikua juu kimasomo ile mbaya.
Nakumbuka kipindi cha likizo nikienda kwao akiniazima novel za chase.
He is a gud man japo i have lost touch with him after so many years
 
Corporate Social Responsiblity inalipa. Kampuni haiwezi kuwepo bila jamii. Kwa hiyo Let him get it na tuone! Tusiogope vijana kupewa madaraka. tumezoea kuwaona walewale wenye mvi kibao na Ama Vipara kama vya kakamiye!! ndi tuamini. Hiyo enzi imeisha.
 
kwactaarifa yenu mafuru alikuwacmarketing km miaka miwili wakipoona ana perfom vizuri wakamleta head of department toka kenya anaitwa dick omondi kumziba mdomo mafuru wakati huo ni marketing manager. huyo dick omondi ndo aliyekuja kuleta hasara vodacom maana jamaa halikufanya lolote jipyaa kazi yake ilikuwa kuwachapa nao wanafunzi tuu. toka hapo mafuru akahamishiwa kitengo cha sponsorship aka Hod then ME. na ndiko alikoondokea. marketing ya voda toka atoke mafuru imelala
 
Mafuru anaweza kufanya kazi nyingine lakini sio u CEO wa kampuni. kwani kuwa CEO unahijika kuwa kichwa hasa na mwenye vision...tangia aanze kazi pale vodacom hajawa mtu wa maamuzi bali ni mshehereshaji je hilo linatosha kuwa CEO? Pili huyu alipata div 3 PCM pale pond akashindwa kwenda ud direct...alienda kuboresha matokeo CBE ndo akajiunga UD kusoma Bcom.....



Ukiangalia kwa makini utagundua kuna chuki binafsi kati ya mtoa hoja na Mr mafuru!tusipoteze muda wetu kujadili mambo binafsi ya watu wenye chuki na maendeleo halali ya watu!!
 
Vetting is still in the process, wote waliofanyiwa usahili wanapaswa kukaa kimya. Hili la Mafuru nililisikia na baadae nikasikia tena watu wakilijadili katika kikao cha pombe nikashangaa maana jamaa mmoja alikuwa anabwabwaja kuwa Mafuru mwenyewe kamweleza kuwa anachukua TTCL.

Binafsi sina tatizo kama akipata hiyo nafasi maana kulikuwa kuna kilio kuwa TTCL inaaongozwa na wageni sasa Watanzania wanataka mzalendo basi apatikane mmoja hata kama sio Mafuru halafu tuone utendaji wake.

Mpaka sasa naridhishwa sana na utendaji wa Mchechu wa NHC, huyu naye alipatikana katika soko la sekta binafsi kwa hiyo siasa za mashirika ya umma anaziweka kando maana hulka ya sekta binafsi ni faida na ufanisi kwanza.
 
Watanzania tuache chuki na majungu, kama jamaa atafanikiwa kuingia pale kweli results mtaziona, hebu angalieni mfano wa NHC na mashirika mengine yaliyopewa damu changa, yanafanya mabadiliko ya kiutendaji vizuri tu. But naogopa yasije mkuta kama ya Tido Mhando.
TUMUOMBEE KIJANA MWENZETU ACHUKUE MZIGO HUO.
 
Back
Top Bottom