Mafuriko

Mafuriko

madaili

Member
Joined
Mar 6, 2014
Posts
32
Reaction score
27
Siku moja ilinyesha mvua kali, barabarani mafuriko balaa.
Mitaani kote kumejaa maji, kuna sehemu magari yote yameshindwa kuvuka, yamepaki kusubiri maji yapungue, jamaa mmoja alikuwa katikati ya maji amesimama ameshikilia mwamvuli. Kwa kuwa kwa kumuangalia haraka haraka jamaa maji yalikuwa yamemfikia kwenye magoti, dereva mmoja aliyekuwa anaendesha jeep alihisi maji si marefu kivile gari yake lazima itapita, akawaangalia watu wote waliokuwa na magari madogo madogo kwa dharau akakanyaga mafuta kuingia majini, matokeo yake jeep yake naye ikazama, baada ya kuogelea kwa shida akafanikiwa kutoka na kusimama juu ya gari yake akamwangalia jamaa mwenye mwamvuli akamuuliza "Wewe inawezekanaje gari yangu imezama wakati maji yanakufikia magotini?". Jamaa akamjibu "Kaka me mwenyewe nimesimama juu ya gari yangu nasubiria waokoaje waje kunitoa."
Dereva wa jeep "fhsofhsoffggggg si ungesema mapema"
 
Back
Top Bottom