Mafuriko ya kutengeneza yana madhara makubwa

Mafuriko ya kutengeneza yana madhara makubwa

H20

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2013
Posts
341
Reaction score
170
Kwanza nianze kwa kutoa pole kwa ndugu na jamaa wa Mwanamke pamoja na mtoto wa miaka 12 waliopoteza maisha kufuatia msongamano mkubwa uliotokea kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Mungu awatie nguvu na subira wafiwa wote.
Angalizo kwa vyama vya siasa wakati huu wa kampeni za uchaguzi.
1. Ni vyema vyama vikazingatia zaidi kueneza sera za vyama vyao zikubalike kwa wananchi na wasishindane ni chama kipi kinajaza watu kwenye mikutano.
2. Tabia za vyama kusomba watu kwa magari kuwapeleka kwenye mikutano ziepukwe kwani zinafanya kutokuwa na uwiano sawa kati ya eneo husika na idadi ya watu waliohudhuria.
3. Tunajua umuhimu wa wasanii katika kuhamasisha na kama mjuavyo wasanii wengi wa Tanzania wanapendwa na makundi tofauti kama watoto, vijana na akina mama hivyo kama chama ikabidi kuwa na wasanii kwenye kampeni kihakikishe mahala kusanyiko litakapofanyika kuna usalama na nafasi ya kutosha.

Kuwa na maamuzi ya busara
1. Kama kiongozi wa nchi, na mgombea uraisi mnakuwa kwenye mkutano na kusifia umati mkubwa ambao hamjawahi kuuona and yet mnashindwa kuona athari iliyopo mbele kwa raia wenu huo ni udhaifu mkubwa kwenye maamuzi na maono yenu. Kama hiyo ilitokea mbele yenu basi mjue kuwa hata nyie hamkuwa katika usalama kwani lolote lingeweza kutokea. Je kwa hali hiyo mnahitaji kura kweli ikiwa hamjali usalama wa raia wenu?

2. Iweje uwanja una mageti 8 then mamlaka husika ifungue mageti matatu tu ili watu waingie na kutoka? Kilikuwa na hofu gani ya kufungua mageti yote? Mamlaka husika inabidi iwe responsible kwa yote yaliyotokea na wawajibishwe. Hapa ni viongozi wote waliokuwepo wanatakiwa kushare responsibility.

UJUMBE.
Mafuriko ya kutengeneza yana madhara. Tuache maji yafuate mkondo wake kwani nature ina namna ya kuyadhibiti. Ukitengeneza mafuriko wakati uko bondeni kwanini yasikudhuru?
 
Oops, well said. Akina Simiyu kwetu njooni humu mkanushe....
 
Umesema vizur sna ila kwa miccm maneno kama haya hawapendi kusikia kabisa kwani kwao ni kama harufu ya kinyesi cha paka
 
H20

ccm wawaache watoto wetu wasome si kuwapeleka kwenye mikutano ya siasa
 
Last edited by a moderator:
Kuna tofauti gani na janga la ghorofa kuanguka na kuua? Wahusika wawajibishwe na wafunguliwe kesi ya kuua bila kukusudia! RIP MAREHEMU WOTE
 
Hili suali la kufungua milango yote haliwezekani kwani litapelekea watu wengi kutoka uwanjani mara tu baada ya wasanii kumaliza kutumbuiza.Sasa wanawafanya watu kama kuku wanamwaga mtama wakijaa tu wanawakomea.
 
Hawakuwa na sababu ya kuleta kwa mabasi na kuwafungia milango
 
Duh, Mungu mwingi wa rehema awapumzishe kwa amani.
 
Gosh, kwanini walifunga milango? RIP poor Tanzanians, out of ignorance you went out of your control.
 
H20

Hahahahaha roho imesuuzika kabisaa maana kamwe blue haiwezi Kuwa Njano.... Mr.president Jana alikua anacheeka kuona watu wengi kumbe walikuwa wamekwenda kutazama show na kwa Habari zilizopo ni kuwa watu Walikua wanagombania kutoka ili wawahi magari ya wasanii yaliyokua yakitoka Nje...!!!unataka Kunambia mtoto wa miaka 12 alimfwata Magufuli pale au yule domo pepe Makamba...??tuache kuwahadaa watanzania maana Mafuriko ya kweli yanajitengeneza sio kulazimisha mnapata Aibu .....rest in peace waliokwenda kwenye Tamasha
 
Last edited by a moderator:
Wasanii wapigwe marufuku kwenye kampeni
 
Kama jamii inayotetea haki ikaa kimya kwa hili nitaumia sanaa.. Rais wa nchi anatoa polee kwa wafiwa.. Hiv hii polee itarudisha maisha.. Anasema pacpo aibuu kwamba "Yalifunguliwa magti 3 wakt yalikuwepo 8" Soo walikusudia kuumizaa watu... Time imefikaa hata jamii ya kimataifa kuiingilia kati..
 
Back
Top Bottom