Mimi siamini kwamba mungu yupo. Sijapata ushahidi wa kuniaminisha kwamba mungu yupo.
Wewe unaniambia, ili kuamini nikasome biblia, kitabu ambacho mungu kakiakndika.
Several problems with this line of thinking.
1. Inabidi uniaminishe kwamba mungu yupo kwanza, kabla ya kutaka nisome kitabu chake kwa mtazamo wa kusoma kitabu cha mungu.
2.Halafu una assume tu kwamba sijasoma biblia. This is wrong. Biblia nimeisoma kuanzia Mwanzo mpaka Ufunuo, halafu nikaisoma kinyumenyume kutoka Ufunuo mpaka Mwanzo, by age 11!
Hizo habari rejareja za binadamu wa kwanza kuwa mweusi au mweupe hazijibu swala la kuwapo kwa mungu.
Halafu concept nzima ya "binadamu wa kwanza" ina betray lack of knowledge of science.
Hmm....imani na kitanda vinahusianaje?
kiranga
hapa ulikuwa una maana gani?
kiranga
kama uliisoma kuanzia mwanzo to ufunuo halafu ukarudi kinyumenyume toka ufunuo hadi mwanzo ili uelewe zaidi au?and at that age ya miaka 11 ulikuwa na uelewa na ulichokuwa unasoma kwa tafakuri ya kina?
kama uliisoma katika hiyo age ya miaka 11 no wonder hukuielewa nashauri usome tena sasa ukiwa na akili nzuri iliyojaa mambo mengi yatakayokusaidia kutafakari vzr.
Imani kwamba kitanda kitakuhimili- na hakitavunjika na kukubwaga chini pindi utakapokilalia- ndiyo inayokufanya ukilalie kitanda.
Ukiwekewa gazeti juu ya matendegu ulilalie huwezi kulilalia kwa sababu hutaamini kwamba "kitanda" hiki cha godoro la layer moja ya magazeti kitakuhimili.
Kwa hiyo hata kukilalia kitanda tu kunahitaji imani.
Imani kwamba ukilala kitanda hakitaanguka.
Imani kwamba kitanda unachokiona ni cha kweli na si hallucinations zako... etc
Nionyeshe anayesema haamini kitu hata kimoja na mimi nitakuonyesha muongo hapohapo.
Je kama kitanda changu ni godoro tu lililowekwa sakafuni?
Sasa hapa sidhani kama hiyo ni imani. Ni suala la ufahamu/ujuzi tu hilo. Unafahamu/unajua kuwa wewe uzito wako na huo wa gazeti havilingani hata kidogo. Na unafahamu/unajua kuwa ukijiegemeza kwenye kitu chepesi sana lazima kitavunjika ua kushindwa kukustahimili kwa sababu umekielemea
Hapana. Kukilalia kitanda ni ufahamu/ujuzi. Si una macho? Si una sense of touch? Si una akili ya kuweza kujua kipi ni hatari na kipi si hatari? Sasa kwa nini kulalia kitanda iwe imani? Imani inahusu visivyoweza au ambavyo havijulikani. Kitanda umekilalia nights kibao halafu bado unaelea kwenye imani tu? Hapana, huo ni ujuzi.
Ni ujuzi. Unajua kuwa kitanda chako kikoje na umeshakilalia sana na hata siku moja hakijawahi kukuangusha.
Sasa hapa kwa msingi huu mtu unaweza kujenga hoja hata wewe mwenyewe inawezekana si wewe ila ni hallucinations zako tu zinazokufanya wewe udhani kuwa wewe ndiyo wewe.
Hapa nakubaliana na wewe. Binadamu tuna ukomo wa ujuzi na ufahamu hivyo mambo mengi sana huwa tunategemea imani zetu tu.
Yaani thread nyingine bana ! Kichefu chefu tuuu.
Wakuu, I hope wote mko poa kabisa. Nataka kuwashirikisha jambo. Kuna hali ya mafuriko makubwa yanayokuja kutokea Tanzania mwezi ujao. Kuna watu ambao Mungu amesema nasi ili tuombe toba kwa ajili ya nchi ili hali hii isitokee na hasa kama itatokea basi isilete madhara ambayo yanaweza kutokea kama hatutaomba Mungu atunusuru na maafa.
Nchi yetu 'imemezwa na chatu'. Hii maana yake ni kwamba nchi hii imetumbukia katika uchawi na kumwabudu shetani as nyoka ni shetani as well as uchawi/ushirikina. Watu waliopewa dhamana kwenye taifa hili iwe serikalini au katika kanisa wamesahau wajibu wao na badala yake wanamkumbatia shetani na kazi zake zote i.e uuaji na umwagaji wa damu zisizo na hatia, uchawi, wizi, uongo na pia ukahaba umekithiri, uaminifu umepungua sana, ufisadi, upagani, ibada za mizimu, kuabudu shetani na mambo mengine yote yafananayo na hayo na kumchukiza Mungu na amekasirika. Mambo yote haya tunayaona day in day out. Na watu wanafurahia watu waovu na uovu kuliko uadilifu na watu wanaotetea haki.
Mungu anaipenda sana Tanzania lakini anachukia uovu huu ndio maana ameonyesha nini kinakuja ili tuombe toba atusamehe na atunusuru na hali hiyo na kama bado itatokea basi isilete madhara makubwa au yasitokee kabisa.
Picha ya mafuriko yanayokuja yanaonyesha mvua kubwa sana ya kutisha na nusu ya Dar ikiwa imemezwa na maji ambayo yamechanganyika na maji ya bahari. Hii inaashiria gharika au kimbunga chenye mvua kubwa.
Kwa yeyote mwenye mzigo wa kuliombea Taifa hili tafadhali omba toba kwa ajili ya nchi yetu na ufunge kwa siku tatu kawaida na sio tatu kavu (utachagua mwenyewe siku za kufunga) ili Mungu atuepushie na balaa hili. Tafadhali mshirikishe na mwenzio.
Nimewashirikisha ili isije kula kwetu tuliopewa huu ujumbe kama tutakaa kimya bila kushirikisha wengine pia waombe.
Usichangie kwa kukashifu na kama huna mchango au huamini basi wewe pita tu na Mungu atakubariki.
Mathayo 18:18, 2 Nyakati 7:14, Isaya 62:6, 45:11
Hakuna ufahamu au ujuzi usio imani. Ufahamu unatoka katika milango mitano ya fahamu. Maana yake ili kufikiri una ufahamu ni lazima kwanza uiamini milango yako mitano ya fahamu.
Unaweza kuona kitanda kipo, lakini process yako ya kulala ni lazima iwe na imani kwamba macho yako mawili yana uwezo wa ku-judge umbali, ama sivyo utaanguka kabla ya kukifikia kitanda. Imani tayari hiyo.
Ukiwa na uvundo mdomoni hata ukiwa katika bustani ya Akihito kipindi cha Spring utaona kichefuchefu tu.
haya mkuu SADAKA tunaweka wapi?
bora uvundo wa mdomo kuliko wa imani !
No wonder you take the bible literally kwamba ni kitabu cha mungu.
No imagination at all.
Zero comprehension.
No capacity for any artistic flair.
Halafu kusema nimeisoma nikiwa 11 haina maana kwamba sijaisoma tena baada ya hapo.
Notion kwamba kulikuwa na "binadamu wa kwanza" ina betray a creationist bias kwamba binadamu aliumbwa in a day, and against the accepted best known scientific theory kwamba binadamu ali evolve.
mimi siweZi sema cha mungu kwa maana kimeshuka toka mbinguni, ila ni kitabu cha mungu kwa maana kina stories zinazomuhusu mungu na inahitaji faith kukiamini na kukitumia kwa kazi za kiroho.
kiranga
is this the best accepted theory? or famous theory?
unaamini sayansi kuwa binadamu alievolve? that was scientific failure of all times. sasa imekuwaje siku hizi hatuevolve tena na kuwa kitu kingine au hapa evolution imefikia mwisho? evolution ina mapungufu mengi sana.
mfumo wa jua na chanzo chake,chanzo cha mwanadamu katika dunia hii,perhaps na sababu ya kuwapo katika dunia,and everything that exist had a start na this scientist are trying and trying to explain but they have not come to consensus. hii tu inathibitisha kuwa majibu yao si sahihi ndio maana kila anayeona anaweza kueleza hili anaeleza na mwingine anampinga.
science haijajitosheleza kueleza vyanzo hizi ikaeleweka.
unajua nimekuwa nikifwatilia haya matheory ya sayansi yanayoeleza chanzo cha kila kitu,
eti wanasayansi wanabishana wenyewe kwa facts za kisayansi halafu wakishindwa wanasema well maybe there is super natural power
but that power is not god.
bcoz when we say it is god it will need us to prove scientific that there is god of which we cant but there is supernatural being.!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!