Mafunzo ya njiwa...

Mafunzo ya njiwa...

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Kuanzia mwaka 1994,nilipokuwa darasa la nne, hadi mwaka 2000 nilipokuwa kidato cha tatu, nilikuwa nafuga njiwa. Nilifanikiwa kuwa na njiwa takribani 2000. Kilichofanya nisiendelee kufuga ni kuhamia kwangu Bweni nikiwa kidato cha tatu.Nyumbani hakukuwa na muangalizi mbadala kwangu.

Kwa miaka 6 ya ufugaji wa njiwa, nimepata mafunzo mengi sana. Nitashiriki nanyi katika mafunzo hayo kutokana na nilichokiona na kukizoea.

Kwanza, njiwa wana wivu. Dume la njiwa haliruhusu kabisa jike lake kufuatwa au kuvutiwa na dume lingine. Wivu huongezeka mno wakati jike anapokaribia kutaga. Dume husika humtinga jike popote aendapo na kumfukuza ili aelekee hasa tunduni. Wivu wa hali ya juu.

Pili, njiwa wana mapenzi, ikiwemo huba (intimacy) na uaminifu.Njiwa hugawana wawili wawili-jike na dume kwa kila kundi. Ni kama ndoa hivi. Hapo,kila mmoja huwa na huyo huyo tu. Hata pale jike au dume fulani linapokosekana,anayebakia hapati mwingine hadi pale ambapo upungufu utajitokeza mahali pengine au mpya kuletwa. Hii ina maana kuwa,kama dume ni moja na majike ni mawili au madume mawili na jike ni moja, hakutakuwa na mapenzi yoyote.

Pia, njiwa 'hula denda' kabla ya kupandana. Denda husaidia kuamsha hisia za mwenza. Ya kwamba, njiwa huandaana kabla ya 'majambo'.

Tatu, njiwa husikitika. Panapotokea msiba, njiwa wote husimama kwa mguu mmoja kama alama ya huzuni na masikitiko. Siku hiyo,mapenzi na kula husimama kwa muda.Ilikuwa ikinipasa 'kuwaambia' msiba husika pale ili kuwarudisha kawaida. Kama taarifa haitolewi,wote huruka na kupotea pindi mwili wa marehemu unapotolewa ndani.

Nne, njiwa wana uelewa mkubwa. Huikariri mbinja ya mfugaji. Mbinja ikibadilishwa,hawaji. Hii hutumika kuwaita ili waje kula. Kwa kufurahi kwao,njiwa waweza kutua mabegani,kichwani na viganjani huku wakijidai kwa furaha. Wakati wa kula,njiwa hawapigani lakini kila mmoja hula kwa kasi kubwa na akitosheka huondoka kwenda kupumzika.

Tano, njiwa husaidiana.Hapa ni hasa jike na dume lake.Kusaidiana kwao hasa huanzia pale jike linapotaka kutaga. Ni mayai mawili tu. Wakati huo,dume humsaidia jike kumpelekea vijiti na manyoya kwa jike kutengeneza kiota ndani ya tundu rasmi lililotengenezwa. Halafu,dume na jike husaidia katika kulalia mayai yao.Hulalia kwa siku 14/15. Hufanya zamu. Tena,husaidiana katika kulisha makinda na kuyafunza kuruka na kadhalika.

Kiukweli,kupitia njiwa wangu nimejifunza mambo mengi. Mengine nitaandika siku nyingine. Wameniongezea vitu maishani. Asanteni njiwa wangu!
 
Tatu, njiwa husikitika. Panapotokea msiba, njiwa wote husimama kwa mguu mmoja kama alama ya huzuni na masikitiko. Siku hiyo,mapenzi na kula husimama kwa muda.Ilikuwa ikinipasa 'kuwaambia' msiba husika pale ili kuwarudisha kawaida. Kama taarifa haitolewi,wote huruka na kupotea pindi mwili wa marehemu unapotolewa ndani.

Thats amazing.
BTW unawaambia kwa njia gani kwamba kuna msiba?
 
Thats amazing.
BTW unawaambia kwa njia gani kwamba kuna msiba?
Huwaambia kwa lugha ya Kiswahili tu kwa maneno-taarifa. Kwa mfano: "Jamani hapa kuna tatizo limetokea.Kuna msiba. Ndiyo maan kuna watu wengi na vilio.Msishangae wala kushtuka." Wakati wa kusema hivyo,ni wakati wa kuwapa chakula kwa pamoja ili waje wote mahali fulani
 
Huwaambia kwa lugha ya Kiswahili tu kwa maneno-taarifa. Kwa mfano: "Jamani hapa kuna tatizo limetokea.Kuna msiba. Ndiyo maan kuna watu wengi na vilio.Msishangae wala kushtuka." Wakati wa kusema hivyo,ni wakati wa kuwapa chakula kwa pamoja ili waje wote mahali fulani

Hee!!! Napenda kujua zaidi kuhusa hapa
 
Hii ya njiwa kijuwa kuna msiba nakubaliana nayo maana kuna Mzee mmoja Wa busara kila msiba ukitokea kwake basi njiwa hawatoki nje yaani mtaani full kutetemeka..
 
Ha ha ha hakika na njiwa dumee Ana ishara akiona mwewe kuna jinsi analia majike yote huingia ndani

Dah, wewe kweli unawafahamu njiwa vizuri,nilisikia eti ukichinja njiwa wenzake wakikuona wote wanakimbia na hawarudi tena!!
 
Dah,wewe kweli unawafahamu njiwa vizuri,nilisikia eti ukichinja njiwa wenzake wakikuona wote wanakimbia na hawarudi tena!!



Yeah Ni kweli kuna siku nilishuhudia njiwa alishikwa kwa ajili ya kuchinjwa sasa mchinjaji akaenda mbali nikauliza nikapewa story hiyo hiyo
 
Back
Top Bottom