Sakasaka Mao
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 14,933
- 20,987
Ujenzi ni usimamizi. Usipoangalia kwa kujifanya boss, gharama ya nyumba1 unaweza kuijenga kwa gharama ya nyumba mbili!Ni FUNDI mzuri tatizo lazima ushinde hapo hapo ukitoka tu kashaiba Mimi ni MTU wa tano kumpasua baada ya kugundua kauza cement![]()
Nimeshuhudia jamaa alivyokuwa akiibiwa sementi iliyokwisha changanywa na mchanga tayari.
Alikuwa akifika asubuhi anawauliza mafundi 'leo mnatumia mifuko mingapi?'
Wakisema minne, basi anatoa kiasi hicho, wanachanganya bila kulowanisha na maji kwanza.
Akimaliza zoezi hilo anaridhika na kuamini kasimamia, anaondoka.
Huku nyuma, mafundi wanaanza kuuza sementi iliyokwisha changanywa na mchanga tayari.
Ndoo moja lt10 sh.1000/=.
Anayekuwa akinunua, kama hana ujenzi siku hiyo, basi ana kariba ya kufyatulia matofari, ipo standby.
Akiishakununua ndoo 5, basi anafyatua tofari 5 anazipanga, anasubiri tena.
Mafundi wanahadithi nyingi za kuchefua.
Hawaaminiki na hawastahili malipo ya kuaminiana kabla hajakufanyia kazi na kumaliza. Halafu usimamizi unatakiwa uwe tight na wa akili.