Mafua yananitesa;ni nini hasa dawa yake?

Hello wana JF!
Mafua yamekua yakinisumbua mara kwa mara yaani kila baada ya kama wiki hivi ni lazima yatanipata na huwa naugua kwa zaidi ya siku tano mfululizo.nimekua nikitumia piliton na codril bila mafanikio.kuna rafiki wangu mzungu alinishauri niwe natumia juice ya machungwa kwa wingi lakini leo ni cku ya tatu mfululizo nakunywa hiyo juice bila mafanikio.wakuu naomba mawazo na msaada wenu nitumie nini maana hata sauti yangu kwa sasa nimekua kama wabana pua.

acha kunywa whisky baridi.....
 
Inawezekana ni allergy, kuna kitabu kimoja kinaitwa EAT RIGHT hebu kinunue unaweza kujua ni vyakula gani hutakiwi kula.
Utaangalia tarehe uliyozaliwa then utapata instructions
 
Hili tatizo la mafua na mimi huwa linanisumbua sana. Tofauti na Baba Collin, mimi najua niko allergic na vitu kadhaa, ikiwamo moshi wa namna yoyote ingawa zaidi ni moshi wa sigara, pia perfum na sabuni zenye harufu kali, vumbi, na hata maji ya baridi (ya kuoga!!). Kama alivyosema mdau mwingine hapo juu, mafua huwa yanatibika kwa dawa kwa siku saba, lakini kama hutumii dawa yanakauka kwa wiki moja! Mara nyingi mimi natumia citrizine na flucorday (ingawa kwa siku za karibuni zimekuwa adimu sana). Dawa kama codril, coldaur, n.k. (zenye caffeine) huwa situmii kabisaaaaa, hizi hunifanya niwe kama TEJA!
 
nenda hospitali coz mafua siyo mazuri ndo hapo halafu mtu anaweza kupata sinus ile mafua kutoka damu
 
Changanya konyagi na asali!changanya vizuri!kunywa!mafua yanabaki historia!nilishafanya hivyo after my mom told me that!nina miaka mitatu sasa sijui mafua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom