Hii dawa tiba yake ni nini?

Super Charged

JF-Expert Member
Jan 12, 2020
922
1,635
Habari wana Jamii,Natumaini Mko salama

Ngoja Niende Moja kwa Moja Katika Mada
Mimi Ni Kijana.

Katika Utafutaji Wangu Wa Maisha Nakumbwa Na Hili Tatizo.

Sijaajiliwa,Naishi Kimchongo Mjini (Dar) situmii Nguvu sana Kupata pesa,Pia Situmii Akili nyingi sana Kupata Pesa,Sipati Pesa Kwa njia Haramu,Sina mpenzi mcharuko Yaani Kiufupi sina Mpenzi Kabisa,Sinywi Pombe,Sivuti sigara au Bangi,Sina Anasa Yoyote Ile Hata Mpira,Movie Sifatilii,Tabia Mbovu Sina zaidi Ya Tabia ya Kununua Madada Poa wa bei ghali wa Exotic Tanzania,Telegram,Tinder Na Dangulo La sinza Africa Sana.

Ambapo Pia Nimeapa Kuiacha Baada ya Kuona Natumia pesa Nyingi Na Pia Naelekea Kubaya Kwani Nimeshaifanya Mara 8 Tangu Nilipoanza Kuifanya Mwaka Jana.Mitandao yote ya Madada poa Nimeshaifuta na Magroup Nimeleft Na namba zao Nimefuta.

Yaani Kiufupi Sina kitu Cha Kunifanya Yanitokee yote Haya Yalonikumba.Ukimwi au Jongwa Lolote Hatari Nashukuru Mungu sina Nimepima Hivi Karibuni

Sikuamini Mpaka Siku Ya Jana Nilipokutana Na Jamaa zangu Ambao Huwa Hatuonani Mara Kwa Mara Tunaonana Mara mbili au Tatu kwa Mwezi.

Waliponiambia "Mbona Umekonda Sana. Sura Inakosa Nuru Alafu mtu Akikuangalia anaona Kama Unamaisha Magumu sana.Yaani umebaki Mifupa" Niliumia Sana Nikijichek Ni kwel,Na Pia Kuna Watu walishawahi niambia Mwaka Jana Mwishoni Lakini sikuwaamini.Leo Nimeamini Kabisa

Tusikazanie Sana kwenye Kununua Madada Poa Kwani Mbali na Hivo Sina anasa Kabisa.Naomba Ushauri wangu Ndungu zangu Nifanyaje Kurudisha Mwili wangu Kwani Afya Ndo Kila kitu Kwenye Maisha.

Kama kuna Dawa ya Kuongeza Mwili(Uzito) Naomba Kujuzwa Nitainunua.Au Kama Kuna Formula Yoyote Ile Ya Kufata.

Lakini Kama Kuna Dawa au Food Supplement ndo Itakuwa Vizuri zaid.

Nakula Mara Mbili au Tatu Na Huwa nakula Kidogo Kiukweli sizingatii sana kula Kwani Kupata njaa Kwangu Ni shida Mpaka nikae Mda mrefu sana bila kula. Sina mda maalumu Wa Kupumzika Ila Napata muda Mrefu wa Kupumzima tu Ila Sio muda Maalumu.

Kwani Utumiaji wangu wa Laptop Na Mitandao ya Kijamii ndo Upataji wangu Wa Pesa.Kwa Hiyo Najiamulia mm Muda gan Nipumzike Ila Mara nyingi nalala saa 6-7-8 Usiku Naamka Saa 11 Asubuhi Kisha Saa 12:30 Nalala tena Mpaka saa 3 Asubuhi.

Umri-Miaka 22
Urefu-Sio mrefu
Jinsia-Wa kiume

Nimeeleza Yote Ili Mjue Ratiba Zangu,Tabia Yangu ili Mjue Wapi Pa Kunishauri au kunisaidia
Madaktari,Makaka Zangu, Wajomba Zangu,Baba zangu, Babu zangu Pia, Naomba msaada Wenu Mimi Kijana wenu Kama kuna Dawa, Food Supplement au formula Yotote ya Kufuata Naomba Kujuzwa Ili Nirudishe Afya Yangu Kwa Sasa Natia aibu Hata Nikitembea.

Kama Usiponiangalia Sura Naonekana Kama Kijana wa 16-17 Years Nilivyombembamba

Msaada Tafadhari Wakubwa zangu
 
ngoja hao mababa, makaka, wajomba na babu zako waje mimi bibi yako nipo nimekaa pale nachochea kuni tule tulale.
 
Habari wana Jamii,Natumaini Mko salama

Ngoja Niende Moja kwa Moja Katika Mada
Mimi Ni Kijana...
Jambo, kwanza kabisa, naomba nikukumbushe kwamba afya yako ni jambo la muhimu sana katika maisha yako. Ninakupongeza kwa kuelezea waziwazi hali yako na kuomba msaada. Hapa chini nimeorodhesha mambo kadhaa unayoweza kuyafanya ili kuongeza uzito na kuboresha afya yako:

  1. Kula vyakula vyenye virutubisho vingi na protini nyingi. Vyakula kama vile nyama, samaki, mayai, karanga, na mboga za majani ni muhimu kwa afya yako na zinaweza kukusaidia kuongeza uzito wako.
  2. Punguza matumizi ya vyakula vyenye sukari nyingi na mafuta mengi, kama vile soda, keki, biskuti, na vyakula vya kukaanga.
  3. Kunywa maji mengi ili kudumisha mwili wako ukiwa na unyevu wa kutosha.
  4. Fanya mazoezi ya mara kwa mara ili kujenga misuli yako na kuongeza hamu ya kula. Mazoezi ya kujenga misuli kama vile kuzungusha vyuma vya uzito, push-up, squats, na sit-ups yanaweza kukusaidia.
  5. Tumia virutubisho vya chakula, kama vile whey protini (inapatikana kwenye maziwa/jibini), kama sehemu ya lishe yako ya kila siku. Virutubisho hivi vinaweza kukusaidia kuongeza uzito wako na kujenga misuli yako.
  6. Angalia masaa yako ya kulala na pumzika vya kutosha. Kupata usingizi wa kutosha ni muhimu kwa afya yako na inaweza kusaidia kuongeza uzito wako.
  7. Tafuta ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari wako au mtaalamu wa lishe ili uweze kupata lishe bora na mipango ya mazoezi kulingana na mahitaji yako maalum ya kiafya.
Natumaini kwamba vidokezo hivi vitakusaidia kuimarisha afya yako na kuongeza uzito wako. Usisite kutafuta msaada wa kitaalamu ikiwa unahitaji. Kumbuka, afya yako ni muhimu sana, na unastahili kuwa na maisha ya afya na furaha.
 
Shukran sana mkuu Ushauri Wako Nitautendea Kazi,Nimeskia Kuhusu Vidonge Vya kuongeza Uzito.Je ushawahi Sikia. Je,Hiki Kitu Kipo Au Ni Scam
 
Shukran sana mkuu Ushauri Wako Nitautendea Kazi,Nimeskia Kuhusu Vidonge Vya kuongeza Uzito.Je ushawahi Sikia. Je,Hiki Kitu Kipo Au Ni Scam
Ndiyo, nimesikia juu ya vidonge vya kuongeza uzito. Kuna aina mbalimbali za vidonge hivyo sokoni, lakini si vyote ni salama na vina ufanisi.

Ni muhimu kufanya utafiti na kushauriana na daktari kabla ya kutumia vidonge hivyo. Pia, vidonge hivyo havifai kuwa njia pekee ya kuongeza uzito.

Ni muhimu pia kula vyakula vya afya, kama vile protini, wanga na mafuta yenye afya, na kufanya mazoezi ya mara kwa mara ili kuimarisha afya yako kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom