Mafua yananitesa;ni nini hasa dawa yake?

Baba Collin

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
456
58
Hello wana JF!
Mafua yamekua yakinisumbua mara kwa mara yaani kila baada ya kama wiki hivi ni lazima yatanipata na huwa naugua kwa zaidi ya siku tano mfululizo.nimekua nikitumia piliton na codril bila mafanikio.kuna rafiki wangu mzungu alinishauri niwe natumia juice ya machungwa kwa wingi lakini leo ni cku ya tatu mfululizo nakunywa hiyo juice bila mafanikio.wakuu naomba mawazo na msaada wenu nitumie nini maana hata sauti yangu kwa sasa nimekua kama wabana pua.

huwa natumia sinutab, ila nina mwaka sasa sijapata mafua wala kikohozi, I Thanks God for that

Nakushauri utafute daktari mtaalamu wa allergies. Yeye atakuambia ni kitu gani uko allergic na kushauri dawa au sindano.

Mkuu chunguza nadhani una allergy labda vumbi,vinywaji vya baridi na nk.

Fanya mazoezi, Kapime fungus pia, Jitahidi kunywa maji mengi. Allergy nalo ni tatizo kubwa, ni vizuri kuonana na Dr.

Hello wana JF!

Mafua yamekua yakinisumbua mara kwa mara yaani kila baada ya kama wiki hivi ni lazima yatanipata na huwa naugua kwa zaidi ya siku tano mfululizo.nimekua nikitumia piliton na codril bila mafanikio.kuna rafiki wangu mzungu alinishauri niwe natumia juice ya machungwa kwa wingi lakini leo ni cku ya tatu mfululizo nakunywa hiyo juice bila mafanikio.wakuu naomba mawazo na msaada wenu nitumie nini maana hata sauti yangu kwa sasa nimekua kama wabana pua.

Baba Collin! Upo mkoa gani hp Tanzania ye2?

Inavyoelekea wewe unaathirika kirahisi na mafua (susceptible to common colds). Ila kwa bahati mbaya mafua hayana tiba!! Kilichopo ni dawa tu za kukupa nafuu.

Kuna baadhi ya mambo unaweza kufanya yatakayosaidia kupunguza kuathirika mara kwa mara. Kwanza kabisa ongeza matumizi ya hand sanitizer. Kila ushikapo vitasa vya milango au kila ushikapo sehemu zishikwazo na watu wengi basi unajinyunyizia kidogo hiyo hand sanitizer.

Hii ni kwa sababu vijidudu vya mafua huwa tunavipata kwa namna hiyo. Unashika sehemu ambayo mtu aliyekuwa navyo naye alishika. Halafu labda bila hata kujijua unajikuta unajishika na wewe sehemu za usoni na matokeo yake unapata maambukizi.

Pia kila mara ushikanapo mikono na mtu kama vile katika kusalimiana, hakikisha baada ya hapo unanawa mikono yako na kujipaka hiyo hand sanitizer. Hand sanitizer huua asilimia 99.9 ya vidudu vinavyosababisha mafua na maambukizi mengine madogo madogo.

Ongeza uchukuaji/ ulaji wa vyakula vyenye vitamini C na madini ya zinki kwa wingi ili kusaidia kuimarisha kinga yako ya mwili.

Zaidi ya hapo pia nenda kwa daktari ukapate na ushauri wa kitaalamu zaidi.

nashukuru kwa ushauri wako mkuu.je hii hand sanitizer ni nini na wapi naweza kuipata?

Celestamine ndo mwisho wa mafua kidonge mia5 kimoja kwa siku tu umepona!

Kapime hospitali allergy na pia magonjwa mengne haswa fungus hata uti mi kuna m2 alikuwa hvyo hvyo lakn aligundulika na uti akawa treated na mafua kwisha pia dawa za kienyeji sasa tumia tangawizi nyingi,pia menya vitunguu saumu kata vipande vipande kama vidonge kisha meza na maziwa fresh ya moto,get wel sun buddy,

nashukuru kwa ushauri wako mkuu.je hii hand sanitizer ni nini na wapi naweza kuipata?

Hand sanitizer ni kisafishia mikono mbadala. Hutumika zaidi pale ambapo mtu huwa hayuko karibu na bomba la maji na sabuni. Kwa Tanzania sidhani kama unaweza kuzipata kirahisi kwenye haya maduka yetu ya kitaa. Labda utafute kwenye yale maduka makubwa makubwa ya madawa na vipodozi. Na sidhani kama kuna kampuni nchini zinazozitengeneza. Nadhani kama madukani zipo basi zitakuwa zinaagizwa tokea nchi za nje.

Similar Discussions

Back
Top Bottom