Maflyover ya Dar es Salaam yanamsaidia nini mtu wa kijijini?

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,752
4,463
Inawezekana ni ikawa ni swali la kijinga kwa baadhi yenu ila kwangu lina maana. Dar kunajengwa maflyover pale Tazara na Ubungo.

Najiuliza hivi haya madude yanayomaliza pesa lukuki yatamnufaisha nini mwananchi anayeishi huko mikoani na vijijini ambaye hana mpango wa kuja Dar??

Nimejiuliza jibu sijapata kabisa. Naomba msiniambie inapunguza foleni, kwa sababu hata magari ya mwendokasi tuliaminishwa hivyohivyo lakini foleni haijapungua. Angalia kuanzia Morocco airtel hadi Mwenge au hadi Posta au hadi Kawe.

Nisaidieni majibu tafadhali
 
Sababu kuu ya msingi kupunguza foleni na kuondoa muda unaopotea barabarani kwa ajili ya uzalishaji.

Sababu za ziada ni kwamba inapendezesha mji hata nyie wa mikoani mkija mnapiga picha.

Poleni mkuu kwa kusahaliwa lakini siku yenu itafika
 
Tunapunguza folen kuokoa bilion 14 zinazopotea kwa mwaka ili tuzilete huko tuwajengee vyoo, shule, hospital nk.
Shida ni vipaumbele ndugu!! Kama rasilimali fedha ni ndogo fanya kwanza vipaumbele!! Kuliko kukimbia ovyo hili halijaisha umeanza jingine!! Watu sasa huduma za afya ni shida kuliko eti unajenga fly over!! Mala treni ya umeme?!! Huku uwiano wa wanafunzi na walimu ni tatizo, madaktari hawatoshi!! Juzi CAG aliongea vizuri sana neno bajeti ni kitu cha msingi sana na ukikipuuzia malengo kufikiwa ni ngumu
 
IMG_20170324_195515.jpg
 
Kwani hospitali ,barabara za huko mikoani zinamnufaisha vipi mkazi wa Dar

Foleni ya hapa tazara unakaa 1hr,2hr ,utafiti wangu mdogo nimegundua abiria wa gongo la mboto ndio wanaoongoza kwa kusinzia kwenye daladala ,yani ukienda njia ya tazara andaa 2hrs kabla

Pili hii njia ni ya airport na ni njia inayoongoza kwa foleni,njia ya malori,scania ,viwanda nk

Njia inayoingiza kodi kubwa iweje iwe na foleni kuanzia saa kumi na mbili asubuhi mpaka usiku,hii njia kila sekunde ni foleni kasoro usiku tu

Ningekuwa rais naapa bajeti ya mikoani yote ningehamishia kujenga fly overs 4 hapa tazara

Hii njia ndio inanifanya nitembee na simu 2 full charge na nikirudi nahakikisha simu inakuwa full charge kupoteza muda kwenye foleni lkn cha kushangaza mpaka nafika destination simu 1% ndio inabakia
 
Maendeleo ni Suala mtambuka, huwezi ukaona athari ya Moja kwa moja km hutotumia jicho la tatu..,Ila ujenzi tu ni Ajira tosha, kukamilika kwa mradi huu kutasaidia kuongezeka kwa uzalishaji maana muDa ni mali, kupunguza foleni,kuongezeka kwa Usalama Barabarani na Raia kwa Ujumla, taswira mpya ya mji (kivutio) n.k...
 
Law of priorities!

Ni suala pana sana Ndugu.Baadhi wamejitahidi kukujibu vizuri hapo juu.Nitarudi kukuelezea vizuri.
 
Huko kijijini mnatuangusha sasa. Mnafikiria kwa levo ya Kijijini kweli.

Tunaokoa pesa zinazopotea kutokana na upotevu wa Muda na Mafuta kwenye foleni,
Halafu hizo pesa tunawaletea umeme wa REA huko ili msibaki gizani milele.
 
Unfortunately wanaojibu kwa kejeli Wana mama, baba, Kaka na dada zao huko mikoani ambako wanakunywa maji ya Kwenye mabwawa ya kunywesha ng'ombe.
Wakienda hospitali hakuna Dawa.
Wanaogopa hata kurudi huko kwani hata bara ni mbovu haitamanishi.

Mungu tubariki waafrika.
 
hata sisi watu wa dar pia hatuna faida nayo maana kupoteza hela buree wakat vijijin hawana hata barabara ya kufika zahanati
Acha uongo mkuu, kwa foleni hizi za Dar fly over zinahitajika sana unless you are speaking from upcountry
 
Inawezekana ni ikawa ni swali la kijinga kwa baadhi yenu ila kwangu lina maana.dar kunajengwa maflyover pale Tazara,na Ubungo.najiuliza hivi haya madude yanayomaliza pesa lukuki yatamnufaisha nini mwananchi anayeishi huko mikoani na vijijini ambaye hana mpango wa kuja Dar??nimejiuliza jibu sijapata kabisa.nisaidieni


Ni kwa ajili ya Dar ili kuondoa kero ya foleni, huko vijijini kuna utitiri wa magari unaosababisha foleni?
 
Back
Top Bottom