Mafisadi wahaha kuwachafua wenzao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafisadi wahaha kuwachafua wenzao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by banyimwa, Mar 4, 2011.

 1. b

  banyimwa Senior Member

  #1
  Mar 4, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa mara nyingine tena mafisadi wameibuka na kuendelea kuisogeza mbele ajenda yao ya urais 2015 kwa kuja na ujumbe mfupi wa maandishi ambao kwa sasa unaenea kwa kasi jijini Dar es Salaam. Ujumbe huu unawahusisha baadhi ya vigogo wa CCM ambao wanawaona kuwa ni mahasimu wao wa kisiasa, na harakati na maandamano yanaoyoendelea kwa sasa nchini. Ujumbe huo unasomeka hivi: "NJAMA ZAFICHUKA!!! mpango wa CHADEMA ni hatari tayari wamejipanga kupita kila mkoa kuhamasisha vurugu na maandamano za kuikataa serikali, pindi hatuwa za kuwadhibiti zitakapofanyika kuna mawaziri na wakuu wa mikoa wamekubaliana watajiuzulu kuunga mkono waandamanaji kwa kisingizio cha kutetea haki za binadamu. Mawaziri hao wametajwa kuwa ni samwel sitta, mwakyembe na membe na mkuu wa mkoa wa kigoma bwana Simbakalia!!?"

  Kwa kuangalia mantiki ya ujumbe huu, hupati shida kugundua kwamba hii ni sehemu ya siasa za maji taka zilizoasisiwa na kuratibu vizuri na vinara wa ufisadi ambao akili yao ni kufanya kila liwezekananlo kuingia ikulu 2015, licha ya dhambi zao za unyonyaji ambazo zimetufikisha hapa watanzania. Hawa wamekuwa na mtindo wa kujifanya kumtetea Rais lakini wakati huo wakifanya vikao vya usiku vy kumhujumu na wakati huo huo kutumia vyombo vyao vya habari na vile walivyovinunua kuunga mkono maandamano ya nchi za kiarabu na wakati huo huo wakionyesha kwamba sababu za maandamano aktika nchi hizo, zipo pia hapa nchini kwetu. Ndiyo hawa hawa waliotoa kwenye RAI wiki mbili zilizopita kwamba kuna njama za kumuangusha Rais na kuwahusisha viongozi na wafanyabiashara kwenye mpango huu. Nashangaa hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya gazeti hili, mmiliki na mhariri wake! Jambo lililo dhahiri ni kwamba watanzania HAWADANGANIKI NA HILA NA GHILBA HIZI!
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Acha wajambe jambe.
  Watu washaelewa somo.
   
 3. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mbona washachelewa? Yaani wanaomba shuka wakati kumeshakucha!

  Watu sasa wameweza kupambanua na kujua nani kwetu ni rafiki na nani kwetu ni adui. Huo mradi wa kujitakasa mbona unaoneka kugoma? Watu wanataka kujua hatma ya malipo ya Dowans ambayo wanayajua yanakoelekea. Huyu Simbakalia wa watu sijui kawakosea nini maana hayumo hata katika vita vyao vya kisisasa katika ngazi ya taifa!
   
 4. b

  banyimwa Senior Member

  #4
  Mar 4, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Si utani, jamaa hawa wamepania na watanzania wakizubaa tu watashtuka nchi imeshagawanwa. Wana ajenda ya mbali!
   
 5. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wao ndio wanao chochoe vurugu kwa uchu wa madaraka na kuwadhibiti watanzania wenye nia njema na nchi yao!

  Tanzania bila mafisadi ianwezekana kataa ujumbe wowote wenye kuangusha na kudhoofisha juhudi za kuelimisha umma juu ya nchi yao na mstakabali wa nchi kwa kukataa mafisadi!
   
 6. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,644
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  nchi hii bana shida sana
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni TCRA kwa nini wasithibiti uchafu wa namna hii?
   
 8. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,167
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Acha wasinzie wakati Mwalimu wa Watu Dr (PhD) Slaa anapiga somo mikoani, wengine huwa hatusomi meseji labda waanze kutupigia
   
 9. M

  Mchili JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hawa mafisadi wamekamata kila angle. Hata hao TCRA sio ajabu wamewekwa mfukoni mwa hao mafisadi kama serikali ya JK ilivyowekwa humo.
   
 10. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  TCRA wako wapi au nao wamekuwa jumuiya ya CCM kama UWT? Tel No.
  zinazosambaza huo ujumbe zinajulikana kwanini hawachukui hatua? Mbona
  kunapotokea sms za kumchafua JK utawasikia mara moja TBC1 na kutoa maonyo
  makali?

  Sasa huyo Simbakalia wa watu masikini sijui kawakosea nini CCM? Sitashangaa hata Njoolay
  RC Sumbawanga naye akaungaanisha huko. CCM ni fitina tu kwenda kwa mbele.
  Sasa naamini kauli ya Pinda kuwa mafisadi wana nguvu kuliko serikali. Lakini sisi tunasema
  hawatashinda nguvu ya umma.

  Ninaomba hiyo tel No. ili niwapelekee hao TCRA nione watafanya nini.
   
 11. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2011
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nadhani maandamano yanayofuata yawe ni ya kushinikiza kukamatwa kwa Rostam Aziz, mhujumu namba moja wa uchumi wa taifa letu. Hakika kama mtu huyu hashughulikiwi sasa nchi hii itazidi kwenda kombo.
   
 12. kyemo

  kyemo Senior Member

  #12
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyo bwana kwenye red hapo simwamini kabisa kama anaweza kuwa kwenye msururu mmoja na hao aliotajwa nao au ndio washampandikiza,darubini yangu imemmulika
   
 13. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #13
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  source ya hii habari haijatajwa nahofia kuchangia mada kama vile tumekaa kwenye vijiwe vya kahawa kusogeza siku.Kati ya waliotajwa sidhani kama ni kweli manake tunajua Sita na Mwakyembe ni wapambanaji wa ufisadi.Simbakalia nimeshakaa nae Kigoma na hapendi kujihusisha na mambo ya siasa yeye ni mpigani na amelenga kuitoa KIgoma kimasomaso uwe mkoa unaokalika na unaofaa kibiashara sasa kahusikaje hapa? na pia ni kati ya wakuu wa mikoa wanaolipwa vizuri na juu kuliko wakuu wengine wa mikoa nadhani mwafahamu cheo chake....
   
 14. n

  ngoko JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii nadhani ni silaha yao ya Nuklia kabisaa, nakumbuka waliitumia mwaka 2005 wakati wa kinyang'anyiro ndani ya ccm waka manage kuwapaka matope Salim , Sumaye etc. Kumbuka siku ya mwisho Sumaye alisema kuna wagombea wanaharibu wenzao kwa kalamu sijui wakifika ikulu watafanyaje , kama siyo kutumia bunduki ????? , wakati huo watu hawakujua nini jamaa anajaribu kuwajulisha wananchi na badala yake akaonekana kama mfamaji . Sasa tuone tena kama itawasaidia , hope haitaweza maana walijichimbia kwenye ulaji wa raslimali wakajisahau .
  Yet macho
   
 15. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,089
  Likes Received: 885
  Trophy Points: 280
  wakumbuke kuwa mtanzania wa leo si yule wa miaka kumi iliyopita. watu washastukia move........... kwanza watu wao sio wasomi thats huoni hata comments zao za kujitetea kwenye JF hawatumi. hawawezi kutmia mtandao..... wafuasi wao ni wale waishio vijijini ambao asilimia kubwa ni maskini wasioelewa. ila safari hii sisi watanzani tuishio mjini tutawasaidia. heko kwa wote tunaoendelea na mapambano dhidi ya ufisadi.
   
 16. O

  Ohotaite Kintu Member

  #16
  Mar 4, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naungana na wale walio na mashaka na ujumbe huu. Aliyeutoa naomba atusaidie kusema unatoka namba ipi ili tumwulize Professor Nkoma ni hatua ipi ataichukua kwa SMS za kipumbavu (kama ipo kweli) kama hizi.
   
 17. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #17
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,130
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  wanaogopaaa aaahaa wanaogopa nguvu ya umma inakuja ni maandmano ya kukamata m1 m1
   
 18. I

  Idofi JF-Expert Member

  #18
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 1,542
  Likes Received: 820
  Trophy Points: 280
  waende hadharani kwa wananchi kama slaa
   
 19. b

  banyimwa Senior Member

  #19
  Mar 4, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wakuu hii sms imezunguka sana kiasi cha kwamba kupata original sender inahitaji ufuatiliaji mkubwa lakini naamini TCRA wakitaka wanaweza kumpata originator wa hiyo sms. Ukweli ni kwamba hawa jamaa wamejiandaa kumshughulikia kila wanayedhani ana mpango wa kutibua mpango wao wa kisiasa wa leo na 2015. Ambacho sijakielewa mpaka leo ni jinsi walivyomuingiza Simbakalia wa watu kwenye axis hii. Nadhani kna mahali walikwaruzana.
   
 20. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #20
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Taarifa tulizonazo ni kwamba huyo jamaa kwenye red ndiyo adui namba moja wa mafisadi kwani wanadai ndiyo anawazuia wao kum-control bwana mkubwa na kumpa ushauri uliojaa upotoshaji. Hawataki hata kumuona na sasa anasukiwa zengwe zito wamn'goe hata kwenye hiyo nafasi ya uwaziri.
   
Loading...