Mafisadi sasa wavamia sekta ya simu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafisadi sasa wavamia sekta ya simu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by akili, Sep 9, 2009.

 1. a

  akili Member

  #1
  Sep 9, 2009
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HABARI zinazotoka chunguni zikiwa bado moto kabisa ni kwamba sasa mafisadi wamenuia kwa udi na uvumba kuteka nyara na kumiliki kila kampuni inayohusiana na masuala ya simu na intaneti nchini.

  Kwa mujibu wa habari hizo kampuni ya simu iliyoingiza njia mpya ya mawasiliano hapa nchini inamilikiwa kwa kiini macho na Watanzania waliokuwa katika nyadhifa za juu nchini miaka si9 mingi iliyopita na hivi sasa wamegeuka wafanyabiashara wakubwa vyanzo vya mitaji yao vikiwa havijulikani.

  Hata hivyo inasemekana wamiliki halisi ni mafisadi wale wale wa EPA na waliokwishachota fedha kwenye mabenki, chama fulani cha kisiasa na ambao wana monopoly haramu kwa baraka za serikali zilizotoka na iliyoko madarakani.

  Nia ya jamaa hawa ni kuhakikisha kuwa wanashika biashara yote ya serikali ikiwemo shule za msingi na sekondari na vyuo vikuu ili wachune buzi na kuamka matajiri kwa kwenda mbele milele.

  Hata hivyo, inafahamika fika kwamba vyuo vikuu vikipewa vianzio vyenyewe vina uwezo wa kuwa watoaji huduma za intaneti na mawasiliano mengine.

  Kwa njia hiyo vyuo vikuu vitakuwa sio tu vimeepuka gharama zitakazobebeshwa na mafisadi hawa bali pia vitajitengenezea pato sio haba na kupambana vyema na ukata unaokabili vyuo hivyo.

  Hili, hata hivyo linakuwa gumu kwa sababu ya kizito mmoja katika wizara ya elimu ambaye anasifika kwa kupenda kitu fedha na amewaweka hata viongozi wa juu mikononi mwake. Ofisa huyo anang'ang'ana kwamba lazima vyuo vinunue huduma za intaneti na televisheni na redio toka kwa washirika wake wa kisiri kibiashara.

  Inaaminika Ikulu na Rais mwenyewe hawana habari kabisa na ishuu hii (ambayo kama ile ya sekta ya madini, nishati na mali asili) habari anazopata zinaonesha kila kitu ni safi lakini mambo yemeoza na wale anaooamini wanamsaidia kuonekana kiongozi bora ndio wanaomfanya aonekane kiongozi wa ovyo kabisa.

  Kiongozi huyo katika wizara ya elimu ana sifa ya kuwasomesha watoto wake wenye bongo lala sio tu kwenye vyuo vikuu nchini bali hata nchi za nje. Na kutokana na ushawishi na fedha aliyonayo husafiri hata nje kwenda kuona watoto wake wasio na akili wanafaulu kwa janja janja tupu!

  Ni dhahiri kuwa kutokana na utatu huu usio mtakatifu kati ya mafisadi, makatibu wakuu wa wizara na wafanyabiashara laghai Watanzania wasitegemee nafuu yoyote kwenye sekta ya habari na mawasiliano.
   
 2. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu Akili
  Unajua hapa ni JF where we dare...
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Sep 9, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ukitaka kuishika nchi kiuchumi ni lazima kushika miuundombinu hiyo.. Mawasiliano (simu na news media) Nguzo za umeme na nishati, Financial Intitution na mwisho imani ya Jeshi la nchi.
  Mafisadi wameisha jikita sehemu hizo na kilichobakia ni sisi kuamini tu kwamba Tanzania ni Tafa maskini yaani umaskini ni part ya Identity yetu!
   
 4. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu Akili vipi tena ulikuwa hujui kwamba mafisadi walianzia huko kwenye simu, Oil Sigara, na Bia? Walianza siku nyingi sana huko mkuu!

  Respect.

  FMEs!
   
 5. O

  Omumura JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa hali inavyoelekea, sasa hawa jamaa mafisadi wameamua kwa kwenda mbele, kilichobaki sasa tugawane nchi yetu wajameni, liwalo na liwe tu!
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,466
  Trophy Points: 280
  acheni hizo" fear mongering" hao mafisadi mnawapa chati sana kwa kuzungumza kwa kuwahofia,while in reality hawana akili sana,its not their fault kwa yote wanayoyafanya,its our fault,we the people.
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  Sep 10, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Warusi walikuwa hivyohivyo hadi alipokuja Putin akawaweka chini.
   
 8. C

  Cool Member

  #8
  Sep 10, 2009
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  sasa hao mafisadi nani awaguse? Aanzie wapi? Sheria zetu ni shalow sana!!! Labda atokee dictator atumie ubabe tu
   
 9. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #9
  Sep 10, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  mi nafikiri hii ndo solution
   
 10. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #10
  Sep 10, 2009
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,272
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Nadhani hii thread in kitu muhimu imekosa. Takwimu. Ikiwa tutaanza kueleza juu juu tu kuwa kitu fulani, blaa blaaa, na kwa kuwa uanzishwaji wake unahitaji mtaji mkubwa ni ufisadi basi tutakuwa tunapoteza point muhimu katika dhana nzima ya ufisadi.
  Ningetazamia muanzishaji wa thread hii angekuwa ametoa maelezo ya kina kuhusu makampuni anayozungumzia na hao wamiliki wake ni akina nani ili wana JF wenyewe waone kama kweli swala hilo ni ufisadi.
  Sijui Celtel iliyoanzishwa na Mohamed Ibrahim na baadae akaiuza na kubadilishwa jina kuwa Zain ni ufisadi.
  Sikatai kwamba kuna ufisadi lakini jambo likianzishwa basi mwanzishaji atoe maelezo ya kina yaonyeshe wazi juu ya ufisadi huo.
  Kumbuka talent ya biashara ni pamoja na uwezo wa kuwa mjanja kibiashara.
   
 11. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #11
  Sep 10, 2009
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Hii thread ipo shallow kama unavyosema. Inakuwa kama ni udaku sasa .. zile story za "Mtu huyo anaeanziwa na jina A anaishi karibu na nyumba iliyokaribu na hoteli kubwa hapa mjini....." Ndio magazeti yetu ya udaku yanavyoandika habari zake ... lakini hapa JF it's were we Dare to talk openly!

  Taja hayo makampuni, au hao viongozi tutengeneze hoja nzito!
   
 12. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #12
  Sep 10, 2009
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Hii thread ipo shallow kama unavyosema. Inakuwa kama ni udaku sasa .. zile story za "Mtu huyo anaeanziwa na jina A anaishi karibu na nyumba iliyokaribu na hoteli kubwa hapa mjini....." Ndio magazeti yetu ya udaku yanavyoandika habari zake ... lakini hapa JF it's were we Dare to talk openly!

  Taja hayo makampuni, au hao viongozi tutengeneze hoja nzito!
   
 13. M

  Magezi JF-Expert Member

  #13
  Sep 10, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nakumbuka wakati barabara ya ubungo-mlandizi inajengwa na magufuli akiwa waziri wa ujenzi wakati huo, jamaa yule tomas mwenye gereji na kiwanda kidogo pale kimara bucha aliambiwa avunje sehemu ya gereji yake kwani ilikuwa barabarani. Jamaa akagoma akaenda mahakamani, lakini nilishuudia magufuli alikuwa anaenda dodoma bungeni, alisimama pale akashuka akaacha amemwambia yule bwana tomas kwamba "naenda dodoma nikirudi nikute hapa pamevunjwa", jamaa akakaidi kwa kuwa alisha fungua kesi mahakamani, magufuli alivyo rudi, ile sehemu ilianza kuvunjwa saa mbili usiku na mpaka asubuhi hakuna kilicho baki barabarani.

  Tukipata rais kama huyu, TZ inaweza kwenda.
   
 14. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #14
  Sep 10, 2009
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,272
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Namuomba moderator aifunge hii thread mpaka hapo aliyeianzisha atakapoleta "data" kamili.
   
 15. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #15
  Sep 10, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu nafikiri hakuna mtu ambaye anamlaumu mmiliki wa celtel (Zain) kuwa ni fisadi. Ukweli ni kwamba jamaa waliingia TTCL kukiwa na makubaliano ya kushirikiana na kuifanya TTCL ikue lakini badala yake walianzisha celtel na kuimega pale kwani hata office makao makuu ya zain pale science ni mali ya TTCL. Hivyo inawezekana jamaa na akili ya biashara lakini kwenye process anafanya ufisadi kama aliofanya. Hivyo la muhimu ni kufuauatilia kwa undani ili unconclude kuwa huyu ni FISADI au la.
   
 16. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #16
  Sep 10, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Ukishasema kuwa wanataka kumiliki "Kila kampuni" ina maana kuwa walishaivamia hiyo sekta na sasa wanataka kuimiliki sekta nzima na kwa kununua kampuni zote za simu(hata hivyo sijui hata ziko ngapi) hivyo heading yako haiko sahihi. Kwasababu kwenye hizo sekta jiulize swali moja;je kumeshawahi ama kuna mafisadi waliowekeza/kuvamia kwenye sekta hizo?

  Pili huwezi kusema eti vyanzo vya mitaji yao havijulikani na wakati huo huo ukisema ni wale wale wa EPA waliochota fedha benki kuu nk.sasa hivyo sio vanzo vya mitaji? Unajiuliza swali halafu unajijibu?Once again unazunguka mbuyu tu.

  Mwisho unadai kuwa watahakikisha wanshika biashara zote za serikali ikiwemo shule za msingi na sekondari na vyuo vikuu,swali langu ni kuwa,je hizo institution unazihusisha vipi na sekta ya simu?Ungetoa ufafanuzi kidogo zaidi...Otherwise ungetake your time kabla hujapost thread hii ili kuepuka mvutano usiokuwa na msingi utakaopoteza tu muda na mwelekeo wa mada halisi kama hipo.
   
Loading...