Mafisadi na Wapambe wao mguu juu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafisadi na Wapambe wao mguu juu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Asha Abdala, Sep 30, 2008.

 1. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Haya- Kibunango, Masatu na Mkamap, someni hapa basi jamani mchangie mjadala


  Utaifa Unayoyoma

  Mafisadi na Wapambe wao mguu juu!
  Changamoto kwa kizazi kipya, Watanzania watu wa ajabu!
  Ufisadi ni Kabila la wauwaji kuliko Mungiki wa Kenya!
  “Mke wangu nakuvisha pete hii iwe ishara ya upendo wangu kwako, iwe ishara ya uvumilivu wako kwangu katika shida, raha na taabu za umasikini unaosababishwa na ufisadi katika nchi yetu” hayo ni maneno mazito yaliyotolewa kwa hisia kali zilizojaa uchungu na mwanandoa mmoja aliyoitoa kanisani wakati akifunga pingu za maisha na mwenza wake hivi karibuni..Sina hakika kama aliambiwa aseme maneno hayo!

  Nilichotaka kuanza kusema ni kwamba ninaridhishwa na mchango mkubwa wa wanaharakati hususan vyombo vya habari katika kuisimamia serikali hii iliyoshinda kabla ya kuanza, na kushindwa tangu ilipoanza.

  Ninaona matumaini huko tuendako. Kwani ni wazi kuwa injiri ya vita dhidi ya ufisadi inazidi kupata waumini,inazidi kupata wafuasi wengi. Kilichobaki tujenge mahekalu na masinagogi kwa utakaso wa damu na moto. Tujiapize kwa Mungu na Mola wetu ili iwe kumbukumbu kwa kizazi kijacho, na kwamba wasije kutokea tena watawala mafisadi wa aina hii hata kutanduka kwa nchi hii nzuri, yenye kila neema na utukufu wa Mungu,lakini inayokabiliwa na changamoto nyingi za ufukara!..Amina.

  Nakumbuka vita ya sasa ilianza na ufisadi wa akina Yusuf Manji. Leo tumefikia wa akina Chenge. Hapa katikati kuna wengi wamethibitika kuwa ni mafisadi. Lakini wameachwa watambe. Wanaendelea kunywa juisi ya utawala kama mashetani wanyonya damu.wakidhani wametupumbza . Na kwamba tumesahau.

  Hebu fikiria. Sisi ni nchi masikini. Wafanyakazi wa nchi hii ni masikini pia, ten asana.hawana nyumba wala kibanda vya kuishi na watoto wao. Lakini katikati ya umasikini wetu anakuja mtu mmoja mwenye asili ya Asia Yusuf Manji, anachota kifisadi takribani billioni 83 kutoka mifuko ya hifadhi ya jamii ya NSSF..anaachwa!

  Na kwa matusi, kejeli na dharua anajifanya mfadhili wa soka. Kwamba tumwone kuwa ni mzalendo, mwenye uchungu na wa kuinua vipaji vya vijana wetu ilhali anatumia vijisenti kati ya mabilioni aliyowaibia wafanyakazi na Taifa kwa ujumla.

  Kiasi kilichofisadiwa na Bwana Manji cha bilioni 83 ni zaidi ya fedha iliyotolewa na Ummoja wa ulaya chini ya mpango wa Budget Support 2005/06 ambapo tulipata takribani bilioni 80.

  Kwamba kama tungehakikisha Manji hachukui pesa zetu pale NSSF, tusingekuwa na sababu ya kwenda kutembeza bakuli kuomba msaada kuinusuru bajeti isikwame. Hebu tafakari kwamba unaishi katika nchi ambayo mtu mmoja anaiba pesa nyingi kuliko msaada wanchi kutoka Umoja wa Ulaya (hizi ni jumla ya nchi 26)! Halafu serikali inasema haina fedha, Haiwezi kutoa huduma ya afya bure. Wanafunzi wa chuokikuu ni lazima wachangie! Bajeti imefika ukomo! Wananchi tujifunge mkanda. Kweli?

  Asilimia 75.9 ya watanzania wanaishi vijijini (The Economist 2008) ambako umasikini wa huduma na kipato ni wa hali ya kutisha kutokana na kilimo duni kwasababu serikali imeshindwa kuwekeza vya kutosha kubadili mtazamo wa kilimo, kutoka kilimo cha ujima (cha jembe la mkono) walau hata kupiga hatua ya kutumia ng’ombe

  Kwasababu ya ufisadi, serikali imebaki inakili kuwa kilimo ndio uti wa mgongo lakini kila mwaka wakulima wanalia hawana zana za kilimo. Wanavunja mgongo kwa jembe la mkono. Wakiomba hata mkopo wa ng’ombe wanaambiwa hawaaminiki! Benki haziwaamini. Hawawezi kurejesha mkopo. Ukigusa mkopo wa trekta ndio usiseme.kila mwaka serikali inasema haina fedha.

  Kwa mwaka wa fedha 2006/07 wizara ya kilimo ilinunua jumla ya matrekta 132 (makubwa 81, madogo 51) sawa na wastani wa matrekta 6 kila mkoa kwa mikao 21.Yaani serikali inayotamba kufanya mapinduzi ya kilimo nchini inapeleka matrekta 6 kwa mkoa mzima. Serikali ikihojiwa kwa nini isitoe zaidi? tunalalamika jamani namna hii hatuwezi kufika. Wanasema tufanye wakati pesa hatuna?

  Wakati serikali inasema haina fedha kuwawezesha wakulima watumie trekta.Na kwamba wasimwamini kiongozi yeyote anaye waambia atabadili falsafa na mtazamo wa kilimo kutoka hiki cha kuvunja mgongo kwa jembe la mkono mpaka kutumia trekta, Serikali hiyo hiyo imepoteza zaidi ya trilioni 1.3 (bilioni 1,300) benki kuu zilizochotwa na kampuni pamoja na miradi mbalimbali ya kifisadi. Hizi pesa za EPA zilikwishafanyiwa uchunguzi na kutangazwa ni billioni 133, sawa na asilimia 10 ya pesa zote ziliobiwa.kazi bado ipo!

  Kama serikali hii ingekuwa na walau chembe ya akili ya huruma kwa watanzania ambao asilimia 76 ni wakulima,na kwamba asilimia 45 ya pato la Taifa linatokana na kilimo. Kiasi cha trilioni 1.3 zilizoibiwa kingetosha kununua kwa uchache matrekta 65,000 (kwa bei ya milioni 20 kwa trekta).. ambayo kwa vijiji 12,000 tulivyonavyo nchi nzima ni sawa na matrekta 5 kila kijiji tofauti na hali ya sasa ambapo serikali inanunua matrekta 132 kwa mikoa 21.

  Kila mwaka kiasi cha watoto 183,800 wanafariki dunia kila mwaka, sawa na watoto 20 kwa saa wanakufa kutokana na magonjwa ambayo asili yake ni utapiamlo (ukosefu wa lishe unaosababishwa na ufukara) na ukosefu wa huduma bora za afya kuanzia vijijini mpaka wilayani kutokana na serikali kutenga fedha kiduchu kugharamia huduma za jamii.

  Kwa mfano; Mwaka 2006/07 serikali iliombwa kutenga kiasi cha milioni 540 kwa ajili ya uendeshaji wa hospitali ya Mwananyamala yenye hadhi ya hospitali ya wilaya iweze kuboresha huduma. Serikali ikasema haina fedha, na badala yake ikatoe milioni 200 kwa ajili ya Mwananyamala.

  Unaweza kutafakari kama hii ndio hospitali zilizopo mbele ya macho ya serikali inatendewa hivi, Je za kwetu Kigoma, Rukwa, Lindi….nk?

  Hali hii ndio inayosababisha wagonjwa kufariki kwa kosa dawa. Ndio inasababisha wagonjwa kubebana kwenye kitanda kimoja hospitalini, ndio inasababisha wagonjwa kulala sakafuni kwenye hospitali zetu, ndio inasababisha mama na dada kulazwa kwenye mabenchi wakati wa kujifungua.

  Lakini tunajiuliza, kweli serikali haina fedha?. Mkataba wa Richmond peke yake uliigharimu serikali hii kiasi cha dola za kimarekani milioni 172, sawa na billioni 260 za kitanzania. Pesa hizi ni mara 520 ya mahitaji ya pesa za kuendesha hospitali ya Mwananyamala.

  Kwamba kwa wastani wa mahitaji ya milioni 540 kama gharama za kuendesha hospitali moja ya wilaya, bilioni 260 zingetosha kuendesha hospitali zote za wilaya kwa takribani miaka mine.

  Unyonge, upole na kujifanyakwetu hayawani ndio kumetufikisha hatua ya mafisadi kujibu kwa jeuri wanapohojiwa masuala ya msingi kuhusu madhambi yao ya ufisadi..

  Nakumbuka wakati Chenge anatangazwa kwenye orodha ya mafisadi kutokana na yeye kuwa Mkurugenzi wa kampuni ya kifisadi ya Tangold ambayo ina uhusiano wa kifisadi pia na kampuni ya Meremeta alimjibu mwandishi wa gazeti moja kuwa “siwezi kujibu utumbo”

  Leo Waziri Chenge anahojiwa kuhusu tuhuma za kumiliki kiasi cha zaidi ya bilioni moja kwenye akaunti moja, anajibu “Hivyo ni vijisenti, mnapaswa kujua kuwa tunatofautiana viwango”…

  Inawezekana kwa Chenge bilioni moja ni vijisenti kwani mpaka sasa umekwishatolewa ushahidi ulioanikwa na gazeti la MwanaHalisi kuwa anamiliki takribani bilioni 25.na amechagua kujibu kwa kukaa kimya. !

  Lakini pamoja na Chenge kuona kuwa dola milioni moja (zaidi ya shilingi bilioni) ni vijisenti, lazima ajue kuwa kipato cha mtanzania wa kawaida (percapita income) ni dola 320 kwa mwaka (Pocket World in Figures-2008 edition). Kwa hiyo dola milioni moja alizonazo change kwenye akaunti moja ambazo kwake ni vijisenti, ni sawa na takribani mapato ya watanzania wakawaida 3000 kwa mwaka mzima.Kumbuka kuwa hawa ni watanzania wa kawaida kabisa,sio wale mafukara waliojaa vijijini kwetu na hata kwenye jimbo la Chenge.

  Nakumbuka Aprili 15,2008 Mh Mbunge Kimiti aliihoji serikali kuwa Rukwa kuna tatizo kubwa la Umeme, na kwamba mwaka 2007 peke yake umeme ulikatika mara 1365, anaihoji serikali ni lini itaondoa adha hiyo?.

  Katika majibu yake Ngereja alikiri ugumu wa kuondoa tatizo hilo kwakusema “gharama za kuhakikisha Rukwa inakuwa na umeme ni zaidi ya pesa za NORAD zinazozungumzwa na Mh Mbunge. Nachojua ni kwamba kiasi cha pesa kinachotakiwa pale ni takribani bilioni 10”alisema Ngeleja.

  Sasa tunajiuliza. Kumbe Rukwa haina umeme miaka yote hii kwakosa bilioni10?. Yaani kumbe fedha alizonazo Chenge (bilioni 25) ambazo ameshindwa kuzitolea maelezo kama amezipataje ni zaidi ya mara mbili ya fedha zinazohitajika kuhakikisha Umeme unapatikana Rukwa?...

  Hivi kweli watanzania tumejifanya wazembe wa kufikiri kiasi cha kuachia kikundi cha watu wachache watumie mabilioni yenye uwezo wa kutunusuru dhidi ya ujinga,maradhi na njaa?.

  Kwamba tumeridhika kuwa adhabu ya kujiuzulu ya akina Lowassa, Karamagi, Msabaha inatosha kwa wezi wa mabilioni kama haya? Mbona tuna wauwa masikini wenzetu kwa wizi wa simu za elfu ishirini , thelathini? Nasikia kuna vijiji ukiiba hata muhogo wa kutafuna kwenye shamba la mtu hulali siku hiyo! Sasa najiuliza Wako wapi raia hawa wanaojiita wenye hasira kali?

  Nadhani kuna haja ya kuwachukulia hatua kali za kisheria hawa wanaojifanya raia wenye hasira! Haiwezekani kwamba watu hawa hawa wenye ujasiri wa kuchoma masikini wenzao moto wa petroli kwa wizi wa simu, lakini hawaoni uchungu dhidi ya mafisadi hawa wanaosababisha takribani 183,800 kufariki kwa kukosa huduma za afya na magonjwa ya utapiamlo na huduma bora za afya!

  Inasikitisha sana kuona nchi tajiri, yenye wananchi wapole,wenye uvumilivu usio na mfano lakini bila kosa tunafungwa mnyororo wa umasikini na mafisadi. Unyonge na upole wetu ndio umetufikisha hapa.

  Kila nikitafakari kuhusu tambo na majigambo ya mduara wa ufisadi nchini sipati picha juu ya nini itakuwa hatma ya Taifa hili huko tuendako. Kwa jinsi matendo ya ufisadi yanavyoibuliwa kila kukicha yananifanya niamini kuwa nchi hii haikuwa na haina mwenyewe kwa muda mrefu sasa.

  Kwamba nchi hii hapa ilipofika ni pa wananchi kuchukua hatamu, na kufanya maamuzi wenyewe. Ninaposoma uchambuzi wa ufisadi wa unaoendelea nchi hii kwa upande mmoja, na kilio cha serikali kushindwa kuwaepusha raia wake dhidi ya vifo, adha na majanga ambayo chimbuko lake ni umasikini unaotokana na ufisadi,

  Ukitazama watanzania tunavyohangaika na wengine hata kufa kwa umasikini, katika ya wanadamu wachache wanaotapanya mali za nchi hii unaweza kushawishika kutafakari maoni ya baadhi ya watu kuwa kwa hali hii, kuendelea kuendesha siasa za majadiliano ni njia ndefu mno ,na muda mrefu mno kwani tunakabiliana na nyoka mrefu anayegonga kila kila kona, na kila kukicha.

  Kwamba tunakosea kufanya siasa kama harakati za kupigania ustawi katika nchi inayohitaji ukombozi. Ustawi na ukombozi ni mambo mawili tofauti. Na hata mbinu zake ni tofauti pia.

  Nashukuru sana mwenendo wa utawala wa Kikwete ambao pamoja na kuendeleza na kujiendesha kwa ufisadi lakini ndio utawala ambao ni rahisi kujua matendo ya kifisadi yanayofanywa na watawala wake.

  Simlaumu sana Mh Kikwete kwa kushindwa kupambana na ufisadi kwa hofu ya kuanguka kwa utawala wake. Nachojua mimi ni kwamba uamuzi wa Kikwete kuacha mafisadi watajwe kwa upande mmoja na huku akiwa hana ujasiri wa kuchukua hatua kwa upande wa pili, ni ujumbe kwa Umma uamue juu ya hatma ya yeye mwenyewe (Rais) na mafisadi anaowakumbatia.

  Nakwamba yupo tayari kwa adhabu ya Umma wakati wowote; iwe kabla ya 2010, wakati wa 2010 au hata baada kutegemea wananchi wanachukuliaje uamuzi Mkuu wa dola kukubali kwa vitendo kuwa ameshindwa kutumia mamlaka yake kuwalinda raia wanaokandamizwa na mafisadi, na badala yake anatumia mamlaka yake kuulinda ufisadi na usanii uneoendelea.

  Na hapo ndio tunarudi kwenye hoja kuwa tatizo la Tanzania ni pamoja na watanzania wenyewe. Kwamba sumu na mikakati ya CCM kutufukarisha imepiga ganzi akili zetu, na sasa tumejenga tabaka kubwa la wananchi masikini wasiojali wala kuchukua muda kutafakari uhusiano wa umasikini wao na ufisadi unaoendeshwa na kikundi kidogo cha binadamu ambao kwa matendo yao wanastahili sifa mbaya kuliko Mungiki wa Kenya.

  Lakini ninapiga moyo konde! Na kuwapa moyo wapiganaji wa vita hii ngumu kuwa hata kama safari ni ndefu, iliyojaa adha na mateso ya majeraha ya upanga na tindikali, lakini muhimu ni kwamba tupo kwenye mstari sahihi…Siku za utawala wa kifisadi na mafisadi zinahesabika sasa!

  Tuendelee kusimamisha kalamu dhidi ya mapanga yao kwakuwa gharama ya kuacha ni kubwa kuliko damu ya watu wachache inayoweza kumwagika kwa tindikali na mapanga.

  Naamini siku watanzania wakijua kuwa wanakufa kwa magonjwa yanayotibika kwasababu ya ufisadi, wanakosa mbolea vijijini kwasababu ya ufisadi, wanakosa pembejeo kwasababu ya ufisadi, nchi hii haitatawalika. Na huo ndio utakuwa mwanzo na mwisho wa utawala dhalimu,wa kilaghai! Kisanii, na mbaya zaidi unaoendekeza rushwa na dhambi ya ufisadi.

  Hatupaswi kujuta kwa ugumu wa vita hii kwani ni hofu yetu ya kuwakabili watawala tangu mwanzo ndiyo iliyotufikisha hatua ya kutawaliwa na binadamu ambao kwa maadili yao tusingewaamini hata kuongoza SACCOS vijijini leo tunawakabidhi hazina ambayo ni moyo wa uchumi wa nchi.

  Tunawapa urais, uwaziri, na ubunge waamue hatma ya maisha yetu na watoto wetu. Tumeamua kuweka rehani maisha yetu kwa viongozi ambao tusingewaamini hata kuongoza kundi la mifugo jamii ya mbuzi kwa kujifinya hayawani tusio na maamuzi kwa ulaghai wa khanga, kofia na pilau, na sasa tunajuta! Utaifa unayoyoma; mafisadi na wapambe wao mguu juu. Na hii ndio changamoto kwetu kizazi kipya kwani tupo leo na kesho.
   
 2. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,613
  Likes Received: 2,020
  Trophy Points: 280
  Makala hii ni ya mwaka...No doubt.
  Ingekuwa la maana kama ingetengenezewa kijarida kabisa na visambazwe kwa wananchi bure...Hadi vijijii vyote 12,000 kama alivyovitaja mwandishi....Hadi huko Sumbawanga kwa kina Nchimbi.

  Ni makala ambayo tulikuwa tuiki dream kama itakuja kuandikwa siku moja...Ni makala ambayo wajukuu wawasomee babu na bibi wasioweza ama kujuwa kusoma.

  Tafsiri bia zifanywe kwa baadhi ya makabila ambao wataelewa vizuri zaidi..Kama hata mikutano ifanyike na kama ni wamasai waelezwe pia kwa kimasai nk.

  Ni makala safi sana na wakati huu wenye kukatisha tamaa kwa kweli ni very uplifting na tuombe Mungu wananchi waweze kuielewa.
   
 3. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2008
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,123
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  There are signs of hope kweli. Lakini inaonekana watanzania wengi for some reason or other wanashindwa kukonect the dots kati ya vitendo vya ufisadi na maisha yao mabovu, sina uhakika atatizo ni nini.
   
 4. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2008
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,686
  Likes Received: 21,951
  Trophy Points: 280
  Dada Asha maandiko yako ni mazito sana, na naamini kama maandiko kama haya yangewafikia watu kule vijijini na wakayaelewa yanayosababisha ufukara wao kwa hakika wale wanaoenda na kugawa t shits na kofia kama danganya toto wangepata mapokezi yanayowastahili.
   
 5. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Jamani nyie niliowataja, mbona hamji kujadili? Basi mwiteni Mtanzania aje kuwasaidia pamoja na Kubwa JINGA

  Asha
   
 6. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Dada Asha,

  Kwi kwi kwi!!! unataka tujadili nini hapa? Sana sana mtu unaweza kuishia kumshikia panga
  Manji.

  Tatizo la TZ sio kwamba watu hatujui tunaibiwa, tatizo ni kwamba hatujui nani atatuokoa.

  Mimi nimewahi kuandika kwamba ukimfuatilia kila mtu mpaka hapa JF, wanaoshi maisha safi ya maadili na kufuata haki ni wachache mno.

  Mimi msimamo wangu ni ule ule, laiti kila anayekuja hapa, akitumia nafasi aliyo nayo kuendeleza ndugu yake mmoja, wawili au watatu, baadaye nchi itakuja kuwa na watu ambao hawatakubali kuibiwa na akina Mengi.

  Ujinga wetu Tanzania ndio unatufanya tuendelee kuibiwa.

  Mimi nimwendaji wa vikao vya waheshimiwa wakija Ulaya. Ila kitu kimoja nilichoamua, sitakubali hata siku moja kwenda kunywa hata juice yao huko hotelini wanakotumbua mali za wananchi. Nimekaribishwa mara nyingi lakini nilishajiwekea msimamo wangu, I am happy na umaskini wangu kuliko watu na akili zao wanajichana, wanatoa tips utafikiri wana visima vya mafuta, huku kule kwetu Kyela watu wanakufa na njaa?

  Kuchukia madhambi kusiishie tu kwenye kuandika hapa JF, lazima kweli tuchukie kwa matendo. Mafisadi hawazidi asilimia 1, kama wasingelikuwa wanaungwa na wengi wetu, kwasababu ni ndugu, ni rafiki nk. huenda tungelishinda mapambano.
   
 7. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2008
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Heshima mbele kwa risala nzito uliyotubandikia ngoja nidownload niisome kwa makini niweze kuchangia sawasawa,kabla sijatawanya huku kyela vijijini.Illetaracy rate ya huku ni 70% kwa umri wa kuanzia miaka 35 kwenda mbele.Na hii ndio siri ya wananchi wa huku kufunga ndoa na CCM.Nakumbuka mwaka 1975 kulifanyika operation maduka,ampapo maduka ya wahindi yalifungwa kupisha maduka ya ushirika.Akja Aboud Jumbe kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili,wananchi wakasoma risala jinsi wanavyoteseka kwa kukosa bidhaa muhimu,badala ya kujibu Makamu wa Rais akajibu hakuja kufungua maduka ya watu binafsi.Baada ya jibu hilo ikatokea vurugu ambayo imeacha historia watu 77 walipelekwa detention Gereza la Ruanda mbeya.Siku ya kusomwa shitaka lao,wananchi wa kyela wapatao 5000 wakasafiri kwenda kusikiliza kesi ya ndugu zao akiwemo kaka yake Kifukwe rais wa zamani wa yanga(Marehemu Ikupilika).Hali pale mahakamani ilikuwa tense afisa usalama wa mkoa akataarifu Dar,Mwalimu habari zikamfikia na akatoa amri ya kuwatoa bila masharti yeyote.
  Leo najiuliza ujasiri huo wa kyela umeenda wapi? mbona watu wanatutia vidole majichoni tunawaangalia tu.Inasikitisha sana!
   
 8. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160

  Charity begins at home. Tatizo tunajua sana kulaumu ila tunshidwa kwenda hatua moja mbele. Mawazo yako ni mazuri sana! Napendekeza uwe mwanzilishi wa kuchapisha vijarida hivyo nasi tutafuata!
   
 9. C

  COMRADE44 Senior Member

  #9
  Oct 4, 2008
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 108
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  This is a fantastic deseration on Bongo.Your effort is not wasted in compiling this piece,I can assure you.Yes we need to print out copies and distribute to those who dont have access to the internet and JF.It is like you have put in writting what we all talk about in bits and pieces,here and there,now and then.
   
Loading...