Elections 2010 Mafisadi kumng'oa mbunge Mahiri 2010....


vyovyote vile....tusiwadharau wananchi.....tuwaache ndio wawe waamuzi wa mwisho....ideally wananchi watamu-evaluate Mbunge wao kutokana na aliyo ahidi na anayotakiwa kutekeleza akiwa kama mwakilishi wao bungeni + jimboni.....kama wanajimbo ni Kabuntas na wakamchagua tena kabuntas......still the ball uko uwanjani kwao kuamua.......
 

Naam usemacho ni kweli kabisa tusije tukajikuta tunacheza mdundiko unaopigwa na fisadi Rostam na kundi lake bila kujijua na yeye huko aliko kukenua gego mpaka gego na kutamba kwamba Watanzania hawana msimamo. Lazima tuwe makini mno katika uchambuzi wetu dhidi ya vita vinavyoendelezwa na kundi la mafisadi, vinginevyo tunaweza kabisa tukajikuta tuko nao upande mmoja.
 

Wananchi hakuna anae wadharau, ila uzoefu unaonyesha wakati mwingine wanalazimishwa kupiga kura kwa mbinu za "kisanii". Rejea kishindo cha asilimia 80 mwaka 2005 na kilio chetu sasa hivi kuwa tulichagua udhaifu. Yaani wananchi asilimia 80 walichagua kiongozi dhaifu kwa makusudi ya potelea mbali? au sanaa.... tusichoke kufikiri jamani, fikra ni uwanja mpana.
 
Ogah, Mkuu wangu humu JF ama kweli watu wanakurupuka sana bila hata kupima...
Kinachoendelea ndani ya CCM ni siasa za majungu wala sii swala la Taifa....Huyo mbunge wa Mshapu Nd. Mpendazoe anacholia ni kilio cha ndani mwake, he has all the rights, kufanya hivyo kwa sababu ni mgombea, hajakataza mtu..na Mafisadi wapo na wapo ndani CCM! hili halina ubishi, na wao wanajua zaidi kuliko sisi nani ni nani! na huyu bwana hana haja ya kuwaridhisha wananchi isipokuwa wanachama wa CCM kwani uchaguzi anaozungumzia ni wa ndani ya chama.

Majungu yapo, mbona Chacha Wangwe alipiga kelele na majungu ndani ya Chadema tukamwelewa na kuomba majibu na tukaweza kutenganisha na utawala wa nchi nzima..
Kwa nini wananchi bado mna fikra kwamba ukiwa mbunge wa CCM au ukiwa mgombea kiti chochote ndani ya CCM basi bila shaka wewe ni mwakilishi wa Taifa zima... kama vile tunaunga mkono system mbovu inayobomoa badala ya kujenga..
It's about time wananchi mnatakiwa kufikiria nje ya kabati la CCM..lakini kama watu bado akili zetu ni CCM tuuu na uchaguzi mzima ni ndani ya CCM, basi tumekwisha na hakika CCM itatawala milele..
 
Jamani mbona mnamshambulia Mhe. Mpendazoe wakati si yeye alielalamika?

Mada hii imeanza kwa Bill kutoa maoni yake kutokana na mtiririko wa nakala za magazeti kuhusiana na mkakati alioona yeye wa kumng'oa Mbunge huyo. Siasa inahitaji subira. Mpeni nafasi na Mpendazoe kutetea kiti chake. Hajalalamika wakuu.
 

Inaonekana kama ameweka ubia na lile jimbo, mteule ama sijui wa milele hadi kifo chake....take home meseji ....kama hakuna alichokifanyia wananchi wake basi apishe wengine...!
 

Mkuu Msanii heshima kwako.

Nakubaliana sana na mapendekezo yako karibu yote. Kama hayo uliyoyapendekeza hapo yakifanyika hivyo, nadhani tutaweza kuwa na uongozi bora zaidi nchini.

Tatizo ninaloliona katika moja ya mapendekezo yako ni la Gavana wa BoT na wakurugenzi wa idara zake (nyeti) kupitishwa na Bunge. Mkuu, labda unieleweshe zaidi. Ila naona Gavana wa BoT na Mkurugenzi wa idara za BoT ni wataalam wa fedha na masuala mengine ya kitaaluma na Bunge ni la wanasiasa. Sina uhakika kuwa Bunge lina uwezo wa kutusaidia katika hilo kwa ufanisi mkubwa. Kwa maoni yangu, Bunge linaweza kupata shida kusaidia kutokana na ufahamu wa Bunge zima kuhusiana na taaluma za viongozi hao ambao si wa kisiasa.
 
Nahamasa kweli na uchaguzi wa mwakani - maana swali langu kubwa litakuwa - hivi kuanzia uchaguliwe ubunge, na kuwa mbunge, umekaa muda gani jimboni hapa! Ama ukichakuguliwa kuwa mbunge tutahakikishaje unaishi katika jimbo hili uone hali halisi ya maisha yetu, uwe na ofisi ambayo tutagonga na kukuta! Tulete maswali yetu uyapeleke huko bungeni!
 
Ninafahamu kwa hakika kwamba Shigela alikuwa anahusika na hii kesi hapa chini akiwa mtuhumiwa muhimu. Siku ambayo alikuwa aitwe kuandika maelezo ya ziada polisi, akatangazwa kuwa Mkuu wa Wilaya. Ninachoweza kusema ni kwamba, tuna tatizo kubwa katika mfumo wetu wa sasa wa uteuzi ambapo watu wetu wa UWT hawana muda wa kufanyia upekuzi wateule, ama wanakuwa wako pamoja na wanaotakiwa kuteuliwa kwa hiyo kuwafichia mambo yao. Hii kesi hadi sasa imekufa.



http://www.thisday.co.tz/News/547.html
 
Last edited:
Uongo mtupu, kwa lipi hasa alilolifanya katika mapambano dhidi ya mafisadi mpaka wamfuate. Ni akili finyu sana kufikiri mtu kama Rostam atumie pesa zake kwa mtu dhaifu kama huyu. Mlovezoe.............. huna kitu kaka, kila mtu ana haki ya kugombea. Kama hukutimiza ahadi zako jiandae kukaa pembeni.
Onyo msiwape nafasi waongo kuleta dhread za kujaza kurasa
 
Uongo mtupu, kwa lipi hasa alilolifanya katika mapambano dhidi ya mafisadi mpaka wamfuate. Ni akili finyu sana kufikiri mtu kama Rostam atumie pesa zake kwa mtu dhaifu kama huyu. Mlovezoe.............. huna kitu kaka, kila mtu ana haki ya kugombea. Kama hukutimiza ahadi zako jiandae kukaa pembeni.
Onyo msiwape nafasi waongo kuleta dhread za kujaza kurasa
 

hapo ndio bunge litakuwa la mafisadi tu kwa ajili wao ndio watakuwa wana hela za kugombea....
lazima uwelewe kuna wabunge wengi kuwa bungeni si kufata kipato bali kinga kutokana na mambo yao waliyoyafanya na wanaweza kuzamini wabunge wengine
hii sera ya mishahara ya wabunge lazima muifikirie vizuri, embu fikiria mmbunge baada ya miaka mitano hana hela ya kugombea si itabidi aende kwa RA, alafu unazani ataweza kumuhukumu kweli
 
hamna kuwindwaa yeyote atakayedondoka ni uwezo mdogo tuuu wa kuwahudumia watu wakeee...na wabunge wengi ccm waliingia kifisadi (wizai wa kura na rushwaaa kubwaaa)..

mafisadi ni akina nani na kwa nn??? (naomba kufahamu)

hatuwezi kuendelea hivi jamani kwani nchi ni zaidi ya majunguuu na wivu wa kijingaaaaa...

hatujaibiwa chochote mpaka sasa kwani rasilimali baki ni mara 100,000,000,000,0000 ya zilizotumikaaa...
 
Sawa mkuu, ni busara zaidi ugombee kupitia upinzani.Kung'ang'ania kugombea kupitia CCM hilo bundi la ufisadi litakuandama.Nasema hivyo kwa sababu CCM tayari wana makundi matatu,yaani CCM Asili(Nyerereists),Mtandao Masilahi(Mafisadi) na Mtandao Matumaini(Anti-mafisadi).Yapimeni makundi hayo ili ujitambulishe uko kundi gani.
Huu ni ushauri wa bure kwa wote mnaotaka kugombea!
 
Kwani nani alimuambia huyo Mpendazoe kuwa hilo jimbo ni mali yake? Yaani yeye akwia Mbunge watu wengine hawaruhusiwi kuja kugombea unapofika wakati wa uchaguzi!

Tena huyu Mpendazoe ameripotiwa kuwa ni mjumbe wa bodi ya William Diamonds (samahani kama nimekosea kuliandika jina vizuri) na huwa haendi kwenye vikao kutoa maoni ya serikali hivyo tunaendela kuibiwa tu madini yetu.
 
Jamani wana JF.Watu wakiona maji ni mazito jimboni kwao, then wanakimbilia kusema kuwa fulani ni fisadi ili kuomba huruma ya magazeti.Magazeti ya kimwandika mara moja basi huyo tayari ni maarufu na wana JF kuanza kum support

Wana JF tusiwe wajinga.Hao wanao wataja mafisadi waulizeni kwanza kuwa kule kwenye majimbo yao wamewafanyia nini wananchi?

Sasa nimegundua kuwa,kinachotuangusha sana katika nchi hii ni haya magazeti.

Jamaa akienda bungeni na kusema Rostam fisadi basi huyo ni mzalendo na anafaa kuchaguliwa.Je huko anako toka ahadi zake amezitekeleza.

IPPMEDIA.Angalieni sana huyo Mwakyembe wetu. Usanii mtupu.Tsh 76m zetu tulizomchangia pale ubungo TBS amejengea ghorofa yake kule kunduchi.Sasa huo ni uzalendo?
 
IPPMEDIA.Angalieni sana huyo Mwakyembe wetu. Usanii mtupu.Tsh 76m zetu tulizomchangia pale ubungo TBS amejengea ghorofa yake kule kunduchi.Sasa huo ni uzalendo? Reply With Quote

76m hazijengi ghorofa wewe ni nyumba ya kawaida kabisa....ebooo....ubungo TBS ndo nini bureau of standards?
 
Hapa ndipo usanii wa wabunge wetu unapokuwa wazi na napata ugumu kuuelewa msimamo wa umma wa watanzania na wenzetu wengi humu JF. Giza na mwanga haviishi pamoja - ama kuna mwanga na giza halipo au giza limetanda na mwanga hauonekani, full stop.

Hii habari kuwa kuna wabunge mahiri ndani ya CCM wanaotetea maslahi ya taifa na hapo hapo kuna wabunge mafisadi ndani ya CCM hiyo hiyo inanipa shida. Either you are with them or you are against them, period - CCM haiwezi kukamata huku na huko, moja lazima iwaponyoke.

Kila kukicha tunashuhudia mwisho wa siku wakikumbatiana na kupongezana kwa kumwadhibu Zitto au kwa kukataa mabadiliko ya katiba au kwa kukebehi hoja ya Dr. Slaa au kwa kuunga mkono bajeti hewa ya fedha au kwa kupinga hoja ya kuiwajibisha serikali - ndio, wako pamoja !!
CCM na ufisadi ni kama konokono na gamba lake.​
 
76m hazijengi ghorofa wewe ni nyumba ya kawaida kabisa....ebooo....ubungo TBS ndo nini bureau of standards?

S
Code:
Mkuu,
Upeo wako mdogo kuelewa.
Hapo unataka maana ya neno TBS au kujua ufisadi wa huyo kaka yako msema ovyo?.
76M alitumbukiza kwenye ujenzi wa Nyumba yake ambayo ni Ghorofa.
 
Upeo wako mdogo kuelewa
.

Haya bwana nakubali


Hapo unataka maana ya neno TBS

TBS can mean anything ie Taking Back Sunday, Towcester Building Supplies, Trinitarian Bible Society, ndo sababu ya kukuuliza....naona umefanya dili...
kujua ufisadi wa huyo kaka yako msema ovyo?
.

Mtazamo wako wa kijinga huo, can substantiate that?

76M alitumbukiza kwenye ujenzi wa Nyumba yake ambayo ni Ghorofa.

Shida yako iko wapi hapo?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…