Nape msimamo wako kisiasa ni upi kutetea maslahi ya umma au binafsi

CHITEMBEJA

Member
Apr 18, 2011
50
95
A.mdogo wangu Mnauye mimi mbona sikuelewi unaniacha mbali kwa uanasiasa wako ni kwa ajili ya maslahi ya Watanzania ikiwemo familia yako na wewe mwenyewe au ni yako binfsi.

Ninashindwa kukuelewa msimamo wako kisiasa ni kupinga uovu au kupinga uovu wa wanaokupinga wewe kushika madaraka?

Ugomvi wako ni baadhi ya viongozi wa upinzani au wa CCM au wa serikali ni upi wa kimaslahi binafsi au wa umma hasa wanapofanya maovu?

Na mwisho matamko mengi unayoyataoa unalenga nini kujifurahisha kutaka umaarufu kuwashinda viongozi wote wa CCM au ni ya dhihaka hebu jipambanuwe kidogo ueleweke.

Msingi wa maswali yangu.

Mimi ni mfuatiliaji sana wa siasa za nchi hii maana zinagusa maisha yangu na familia yangu moja kwa moja kwa hiyo siwezi kujibaraguza kuwa sijali na napuuzia hapana.

Kwa msingi huo Nape awali kuchomoza kwako kwa upande wangu ilikuwa katika kugombea uenyekiti wa wa Vijana taifa ulipotaka kumng'oa Nchimbi lakini mizengwe ikapikwa na wabaya wako wakakutosa ki aina aina mimi mtu wa kusini huku ambao tulikuwa tunakushabikia tuliumia sana, na tukawalaani sana Nchimbi na genge lake la akina ...................... ambao wewe mwenyewe unawafahamu.

Ukaendelea kufuatwa fuatwa mapaka wakakung'oa umoja wa vijana wakiwa na lengo kukung'oa ujumbe wa Halmashauri kuu kisa kilikuwa wewe kujaribu kupigana na kundi lile kwa njia ya kuonyesha dhamira ya uongozi wako kuwa ni kupambanana maovu hata kama anaefanya ni ndugu yako hapa ulianza na kitega uchumi cha vijana maovu yaliyokuwepo katika mkataba.

Wewe ulikuwa source mzuri wa gazeti la Mwanahalisi kuhusu sakata lile na ukajizolea umaarfu uliyowafanya watu wakuamini kama mpiganaji wa maslahi ya taifa na unachokiamini ndicho unachokisimamia.

Mapambano hayo uliyaendeleza ndani ya CCM kwa chini chini na katika vikao vingi na ukaoenekana kuwa mwiba na hasa kwa wale uliyokuwa unapambana nao ambao karibu wote walikuwa katika madaraka.

Wenyewe waliyokuana kero kwao kwa kuwaparamia paramia wakati huna uwezo huo ni sawa debe tupu haliachi kutika wakaona kelele ili kukunyamazisha wakamwambia mkubwa wao akutulize njaa inayokusumbua kwa kukupa kitu kidogo tu UKUU WA WILAYA hayo yalikuwa mawazo yao siyo yangu.

Mtego huu ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani ulinyamaza kimya ukaja huku kwetu ukawa unachapa kazi kwa kuimba nyimbo zile zile ulizokuwa unawakatalia kuimba wakati hawajakulaghai na haka kacheo.

Nilikuwepo wakati unaapishwa na katka shughuli zako nyingi kule Masasi ulikuwa mtu mwema sana kwao na siyo wananchi na ungekaa muda mrefu pale ungeibuka na kashifa Mungu alikusaidia ukaandolewa mapema na wale wale waliyokupeleka hapa baada ya kuona kuwa mtego wao umefanikiwa kwa zaidi ya asilimia mia moja.

Wakakuchomeka CCM katika nafasi uliyonayo mtego wao ulikuwa kukuonyesha wewe mbele ya jamii ni mtu wa namna gani/ kwa siyo kweli kama ulivyokuwa unajinadi ni njaa tu hilo ndilo lengo lao siyo langu kwa mujibu wa matukio yanayojionyesha kati yako na hao wenzako.

Ukiwa katika nafsi hiyo kijana wa watu ulidandia haraka sana yale yote yaliyokuwa yanakifanya chama chako kuwa kinyaa mbele ya umma wa kimasikini sana ambau hauna uhakika na mlo wa baadae unaishi kwa kubahatisha hasha huku niliko mimi sijui kwa mama huko Singida nayo ni ya ufisadi uliyoyakuta wenzako kama wanajaribu kupigana nayo bila mafanikiyo na wengine wamekaa kimyaa kama hawakuwahi kushiriki vita vya maneno matupu.

Kijana kwa kauli zako za kila siku kila mara ukapamba magazeti vyombo vyote wa kielectronic vya nje na ndani ukajizolea umaarufu wa ajabu tusiyojua mitego tukaamini kuwa sasa umewaingiza katika anga zako ni kusuka ama kunyoa kumbe wapi bwana wale wakubwa walikuwa wanachekea ndiyo maana hawakushtuka hata kidogo.

Nape sioni sababu hapa kunukuu yote uliyokuwa unaysema kwa nguvu zote mwaka jana juu ya ufisadi na kiama kinachokuja kwa watu hao ambao ulizunguka nchi nzima kuwatukana kuwakashifu na kuwaambia siku zao zimekwisha na ukiwataka wajisalimishe wenyewe mapema ninakumbuka nilikuwa ninakusikiliza katika radio moja ya njee ulisema haya katika kusizitiza hatua ambayo itachukuliwa na chama juu ya mafisadi hayo papa ambao ulisema Chama hakihitaji ushahidi wa mahakamani "ndiyo hatukukuta na gongo lakini mdomoni unanuka gongo ni wazi umekunywa" hayo yalikuwa maneno yako katika kuwathibitishia umma kuwa kwa vyo vyote vile Chama kitawachukulia hatua wote wanaolalamikiwa bila huruma.

Lakini cha ajabu Nape muda ulipita na tukaingia mwaka mwingine wa uchaguzi kila mmoja akategemea kuwa wale waovu ndani ya Chama kuanzia ngazi za chini hadi juu hii itakuwa fursa ya kuwaondoa kupitia vikao vya kuchuja majina bila kutaka ushahidi wa kukutwa na gongo bali kunukia gongo mdomoni.

Cha ajabu ni Chama kikafanya kufuru kuanzia ngazi ya kata nchi nzima hadi taifa na waliyofanya fujo yote ni wale wale ambao ulisema lazima wang'oke ili kunusuru chama wao ndiyo wenye fedha walifuma mtando mzuri kuanzia ngazi chini hadi taiafa kwenye chama na jumuiya zake ndiyo maana mimi binafsi ninadhani ni kuwaonea kamailivyofanyika kuwahukumu watu wanyonge tu waliyojiokotea vijesenti vya mafisadi kupitia uchaguzi huu na kuwahukumu kuwanyang'anya madaraka yao ambayo ni mtego baadae hapo kuwa utawapatia tena ridhiki au mtaji wa kupata genge barazani pake maana kila baada ya uchaguzi umuhimu wa watu hawa wanaotumika katika uchaguzi kulubuni watu unakwisha mapaka uchaguzi mwingine.

Nape katika mchujo uliyofanyika hasa wa nagazi ya Taifa wewe ukiwa mmoja wapo miongoni mwa majianyalikuja mkononi mwako ni pamoja na ya watu wale uliyokuwa unaimba nyimbo zao kila kukicha ukawachafua kwa kila aina nchi nzima kwa kutumia fedha za wanaCCM wenzako walalahoi maana hukuwa unajigharamia katika ziara zile ulizokuwa unaonekana unacheza ngoma na vijana na wanawake bali zilikuwa za Chama.

Kila mmoja muumini wako alikutegemea kuwa hapo ndipo patamu sasa wamekataa kujiondoa wenyewe nacho Chama kimewavumilia kiungwana na sasa kupitia vikao hivi Nape hatakamatika mpaka watu hawa wang'olewe kwa ujasiri mkubwa kama walivyofanywa akina Mkono na kuambiwa wakitaka watoke na familia zao wakafyata mkia.

Lakini cha ajabu majina yaliyojadiliwa ni ya akina Kweka watu wadogo sana yale yaliyokuwa yanatabiriwa kuwa ndiyo yangekuwa moto sidhani kama kuna aliethubutu hata kuyagusa ukiwemo wewe bwana mkubwa na wala mpaka leo hii hujatueleza mwsho wa sakata lile ulilokuwa umelianzisha laa kinaja wewe huna haya wala mshipa wa iabu unajua kula matapishi yako tatizo ni nini hasa Nape mbona unatuyumbisha waumini wako tukueleweje.

Badala yake NAPE sasa watu wale ndiyo unaowakumbatia nimekuona mara kadhaa ukiwa nao hata pale ambapo wao hawahusiki na upo tayari kufanya kazi chini yao laa mdogo wangu njaa mbaya sana ifi wewe unajionaje na nafsi yako inajisikiaje unapokutana na watu kama hawa ambao wanakujua ulichokuwa unawafanyia na dhamira yako baada ya kukosa uenyekiti wa vijana Taifa, na kutokupata madaraka serikalini mpaka walipokutuliza na ukuu wa wilaya?

lakini pia wakati watu wanakutafakari wewe na wanaokupa madaraka hayo ya kichama maana yao na wewe kuyakubali maana yake nin i katika hali kama hii sasa unajifariji au unawatumikia hawo wakubwa wako kwa staili ya kitoto kabisa ambpo watu sasa watazidi kukushangaa.

Ifika kadi ya CCM au ya Chadema ni wakati gani inakuwa na maana kwa Chama? Slaa kuwa na kadi ya CCM wakati ndiye mwiba wa CCM inakufariji nini wewe hujui kuwa kuokoka siyo maneno ni vitendo? Mwanaccm ni nani alie na kadi au mwenye matendo ya CCM kukipenda Chama Slaa huyu anaekibomoa Chama Chako Kila siku ifi unaweza kuichukulia hoja hiyo ukawafanya watu wanaomwamini kumwona mnafiki kwao au kwa CCM.

Kwa mujibu wa maelezo yako na Slaa Mwenyewe ni dhahiri kuwa Sysytem ya CCM ni mbovu na inaweza kuchezewa chezewa kama anavyotaka Slaa huku akiwatupia madongo, unamruhusuje nyoka kuingia ndani ya nyumba Nape?

Wewe hujakiri kuwa Slaa ni nyoka wa Chama chako sasa how come unagundua kuwa bado anajipenyeza katika matawi yenu na kulipia ada kadi yake anatafuta nini huyu siyo kuna wanaccm wanaitumikia Chadema hebu waulize wale waliyokuwa wanapokea ada zake walikuwa hamjui Slaa kuwa ni mbunge wa Chadema aliondoka CCM?

Kama uwepo wa Slaa CCM haukuwa ushushu kwa Chama Chake ni wa CCM kwa nini sasa wewe unamuumbua kada wenu mbele ya kadamnasi ataifanyaje basi hiyo kazi mliyotuma Chadema? AAA mimi sikuelewi hili la VIONGOZI WA CHADEMA NA CUF NA WENGINE KUWA NA KADI AU UANACHAMA WA VYAMA VIWILI UNALISAIDIA NINI CCM NA UMMA KIJUMLA?

Kwa sababu hujatueleza kwa kuwa kwao na kadi mbili ninyi mnanufaikaje mnawatumia vipi ili jamii iwahukumu kuwa ni wanafiki au wasaliti isije kwa kujipenyeza kwao katika CCM ni kwa manufaa ya upinzani kama tunavyoona kuwa sasa CCM haina privace tena kama zamani vikao vyao vyote vinajulikana maamuzi yake hata kabla ya kikao kumalizika na diyo maana gazeti kama mwanahalisi lilifanikiwa kuibua makubwa ya CCM HASA MAOVU KWA SABABU AKINA SLAA WAPO NDANI NA NYINYI MNACHEKELEA MICHANGO YAO BILA KUJIJUA KUWA MNAUWAWA.

NINAOMBA NAPE KAMA ANASOMA ANIELIMISHE SINTOFAHAMU YANGU JUU YA MSIMAMO WAKE KISIASA NI KWA AJILI YA MASLAHI YA UMMA AU BINAFSI.
Edit Post Reply Reply With Quote

 

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
48,718
2,000
Nape hakuwi kuwa na msimamo wa kutetea umma hata siku moja, muulize zile siku 90 za mafisadi kama hajikwisha bado!
 

waubani

JF-Expert Member
Nov 21, 2012
540
250
Nape alishaachaga hizo habari za kupigania wananchi, sikuhizi ni muumini wa unafiki wa kucheza na maneno tu ili alitumikie tumbo lake tuu (siku hizi tena kitambi kimekuwa kikubwa.) Anajua sana anawakosea sana wananchi ila ndio hivyo tena NJAA NI UTUMWA.
 

adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
12,071
2,000
watu kama Nape nikama kuwapotezea kwa muda, wakitoka madarakani niwakuweka ndani mojakwamoja maana wanakaa kupiga

propaganda kwa faida ya matumbo yao, taifa linateketea, uchumi unayumba watu wanaangamia, wao bila haya hata aibu kutwa

kutuchanganya majukwaani na mitandaoni hili halikubali.
 

manduchu

Member
Apr 2, 2012
84
95
Nionavyo mimi wanachi hawatetewi kama hakuna sera mathubuti, ambazo zikifanyiwa kazi wataondokana na hali duni ya maisha yao. Viongozi wengi wa siasa wa bara la Afrika na wapiga kura wao, bado hawajaling'amua hili. siasa zetu nyingi zimekuwa zikiwalenga watu.( nani atatufaa na, si sera zipi zitatufaa). mpaka hapo tutakaponza kufikiria sera na si watu gani wanatufaa hakuna wananchi watakaotetewa na siasa zetu, siasa ni sera na kufanya maamuzi kwa maslahi umma.
 

BJEVI

JF-Expert Member
Jan 19, 2011
1,359
1,195
Nape kengele tu ndani ya ccm....inapigwa pale watu wanapotakiwa kukusanyana kama primary vile.
 

SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
30,909
2,000
Huyo anafahamika ni mchumia tumbo, huoni tumbo lake lilivyofutuka mbele, huyo ni fisadi kama walivyo mafisadi wengine tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom