Mafia: Tumeibeba sana CCM sasa tutaiacha rasmi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafia: Tumeibeba sana CCM sasa tutaiacha rasmi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mizizi, May 23, 2011.

 1. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Tunasikitika sana kutamka haya lakini imefika wakati wa kusema. Kisiwa cha Mafia tumekua wanachama na wapenzi wa ccm, na tumekuwa tukiichagua wakati wote wa uhai wake. Pamoja na chama hiki kukipenda na kuendelea kukiunga mkono, hali imekuwa tofauti na matarajio yetu kwa nusu karne sasa. Kisiwa hichi kimekosa barabara nzuri, hakuna kiwanja cha ndege bora, usafiri wa majini sio wa kuridhisha, hakuna shule bora, zilizopo zote ni za kidato cha nne, hospitali mbaya, hata sekta ya uvuvi nayo imesahaulika. Pamoja na hayo yote, kisiwa cha mafia tumesahaulika hata kwenye kugawa keki ya taifa, kwani hakuna kiongozi aliyewahi kuteuliwa nafasi yeyote ile kama ya ukurugenzi, U-DC, RC, hata makatibu wa chama ngazi yoyote ile tangu uhuru mpaka sasa, si kama mafia hakuna walio na sifa zinazofanana na wateule tuliowahi kuwa nao au tulio nao, ila ni kutokana na kudharauliwa na viongozi wote waliowahi kutawala nchi hii, pia kutokana na upole wetu na kutoonyesha kuleta upinzani kwa chama hiki.
  Nadhani sasa umefika wakati wa kujibu mapigo kwa vitendo kwa ccm kwamba, dharau na hila zote tulizovumilia sasa inatosha. Tumetengwa vya kutosha, tumebaguliwa inatosha, hali tulikuwa nayo inasikitisha. Kama ccm si mshirika wetu wa dhati na kweli, ni muda sasa wa kujivua kutoka kwao. Haiwezekani wilaya ya mafia pamoja na kuwa na idara ya maji tangu kuanzishwa kwake, ni kijiji kkimoja tu ndicho chenye maji yanayozalishwa na idara hiyo, ni vijiji viwili tu ndivyo vyenye umeme tangu uunganishwe miaka ya sabini. Zao la nazi tunalotegemea limesahaulika, hakuna kiwanda cha kusindika mafuta ya nazi sasa, hakuna soko la uhakika, hakuna usafiri wa uhakika wa kusafirishia nazi hizo, hakuna anayeshughulikia hilo, hakuna hata ahadi juu ya hilo.
  Hayo machache, nitaleta zaidi.
   
 2. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  poleni sana.hata hivyo hamjachelewa.kama kweli muna nia basi naamini mtakiunga mkono chama mbadala CHADEMA ili ikifika 2015 ishinde kwa kishindo.
   
 3. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  wazee wa Bweni mpooo?? Wazee wa Kanga mpooo??? Watu wa far north esp Bweni kwa Dk. Dau wa NSSF nawafagilia sana! Kuku wako manati ya nini?? Poleni maana imewachukua muda kutambua ukweli kwamba CCm is now for tycoons not you wakwea nazi na wavuvi!!
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Tangazeni kujitenga na tanzania,muhamie comoro mtapata maendeleo!sijawahi sikia kiongozi yeyote kutembelea huko
   
 5. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #5
  May 23, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  sio nyinyi tu,angalieni hali za sehemu zote wanaojifanya royal kwa CCM!! Tafakari,chukua hatua!
   
 6. Manyenye

  Manyenye Member

  #6
  May 23, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Pole sana ngoja 2015Hatua ya kwanza kumuona CHADAMA
   
 7. Taluma

  Taluma Senior Member

  #7
  May 23, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duuh hiyo heading?
   
 8. Tumaini Jipya

  Tumaini Jipya JF-Expert Member

  #8
  May 23, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Duuu,ni kweli Jamani,nimeshawahi kufika Mafia sehemu inaitwa Kilindoni na Chole,hali ni tete saaaaana,Maisha ni duni mno,kweli wamewekwa pembezoni kama sio kutengwa!!
  Tia bidii mkuu kuwaamsha wengine huko!!
   
 9. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #9
  May 23, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Tumevumilia tumeshindwa, Mbunge wa kipindi flani alitangaza nia ya kujitenga wakamzima. Sasa nadhani tunahitaji kufikiria upya hilo. Kwani rasilimali tunazo, kama bahari nzuri kwa uvuvi, fukwe nzuri kwa utalii, tuna gesi kama songo songo, zao la nazi, korosho na mabonde mazuri ya kilimo pamoja na kina cha maji ya kutupatia bandari nzuri.
  Kwani tumechoshwa na unyonyaji na dharau!
  Kwa sasa hakuna kiongozi yeyote wa chama hapa mafia anayejishughulisha na mambo ya chama, kwani hata hao viongozi wa chama wamekosa hata hoja za kuwajibu wananchi kwa sasa, kwani ahadi zimejirudia mara nyingi bila utekelezaji, sasa imebaki stori tu. Hata huyo mbunge wa Mafia amekosa hata usema huko bungeni, nadhani nyinyi ni mashahidi, inawezekana hata kumfaham hamumfahamu. Viongozi wa serikali ya ccm wamedhurumu maeneo ya ardhi za walalahoi wa mafia na kuuzia wawekezaji uchwara, sas ni migogoro ya ardhi ndio urithi wao, kuna kijiji kimoja nilitembelea na kuambiwa wanakijiji wote wameshitakiwa kwa kosa la uvamizi wa eneo. Karibuni mtasikia yaliyotokea huko tarime yakitokea mafia. Kwa sasa ni wakati mzuri sana kwa chama kinachohitaji kuungwa mkono kufika mara moja, kwani wananchi kwa kweli wamekata tamaa
   
 10. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #10
  May 24, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  poleniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
   
 11. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #11
  May 24, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  CCM hawana tofauti na tamthiliya ya Marimaaaaaaaaaaaaa mzahamzaha tuuu
   
 12. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hamna lolote ni UJINGA TU!!! Subirini GATI lenu na huo uwanja wa ndege mnaojengewa...
   
 13. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2011
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Wajinga sana nyie. Mlifikiri CCM wajomba zenu wale wawaletee haki zenu kwenye kisahani!!??
   
 14. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kutuita wajinga mnakosea sana, kwani kila mtu alizaliwa na ujinga, akaelimishwa ndio akelewa, akawa mwelewa, sasa kama waelimishaji wanabagua sehem za kwenda tutajua vipi haki zetu? Nadhni si vyema ukatuita wajinga kisha kisha ukaishia hapo hapo, inawezekana wewe ni mjinga zaidi na ndio maana huna cha kutuelimisha, acha wanaoweza kutuonyesha njia, tena acha kabisa kuchezea hisia za watu, watu tuna uchungu sana na umasikini wetu, kama wewe ulisomeshwa kwenye shule za kuondoa ujinga moja kwa moja kaa kimya, sisi tunaongea tumesoma kwenye shule za kata, tumemaliza na bado ujinga tunao, na hatukupenda kuwa wajinga, mazingira ndio yametulazimisha!
   
 15. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Inaonekana wewe huijui Mafia vizuri, mimi nanaishi hapa maisha yangu yote, Uwanja wa ndege sio kipaumbele cha mwananchi wa mafia, kwani hata ukikamilika hautaleta mabadiliko yoyote kwa mwananchi wa kawaida. Kwani hakuna mvuvi au mkulima ama mpanda minazi wa mafia anayeweza kulipa nauli ya kusafiri kwa ndege ama kutumia ndege kusafirisha samaki kupeleka ferry kuuza ama nazi na ng'onda kupeleka dar na kwengineko kuuza.
  Kwa taarifa yako, hilo gati halikuanza leo, ni miaka mingi linajengwa na halijakamilika, na hata likikamilika story haitakuwa kama inavyotarajiwa, kwani umbali wa mafia hadi dar kwa vyombo vya baharini ni Notiko miles 180 hii ni kujumlisha na mzunguuko wa miamba yote, imagine nauli itakuwa shilingi ngapi ikiwa znz to dar ni notiko miles 47 na ni almost 30ths?
   
 16. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #16
  May 24, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Ninyi Mafia, Tanga, Lindi, Rufiji, Mtwara na Songea inabidi mfuate nyayo za Kigoma
   
 17. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145

  Wewe ndio huijui Mafia. Kwa nini Bulji amepata ubunge tena Mafia kama sio Gati na Uwanja wa ndege tena kwa ahadi kuwa airport itapeleka barabar ya lami mpaka Utende!!!?? Mbona nyumba za barabarani kwenda Utende zote zimepigwa alama kwamba zitafisdiwa kwa ajili ya Barabara ya Lami kwenda Utende?
  Gati tayari mmeshaanza jengewa na karibu litamalizika, au unataka niaattach picha hapa?
   
 18. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,663
  Trophy Points: 280
  Dunia nzima hawaitaki ccm!
   
 19. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #19
  May 24, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Unaweza kuthibitisha ni mwananchi gani aliyelipwa fidia ya nyumba yake kwa upanuzi wa barabar? Waweza kunitajia hiyo pesa ipo kwenye bajeti ya serikari ipi? Na ahadi ilitolewa wakati gani? Au na wewe unataka kusema hujui janja ya ccm kupata kura? Unakumbuka mbunge kimbau aliahidi kujenga bara bara kwa mchanga kutoka Ulaya, ilijengwa? Hizo ni siasa tu. Kwani kutiwa X nyumba za kando kando ya bara bara ndio kujengwa barbara? Angalia ilani ya ccm 2005- 2010 ilisema waislamu watapatiwa mahakama ya kadhi, ipo wapi? Pia ilisema kila wilaya itajengewa chuo cha veta, muda umepita, mafia kipo wapi? Balleni? Kilindoni? Chole? Malimbani? Utende? Au kirongwe na jojo?
   
 20. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #20
  May 24, 2011
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  2015 msirudie makosa! fanyeni mabadiliko!
   
Loading...