Mafia: Tumeibeba sana CCM sasa tutaiacha rasmi

Mafia: Tumeibeba sana CCM sasa tutaiacha rasmi

Ndugu Mizizi, kama ulikuwa hufahamu UJINGA na UMASIKINI wenu ndiyo mtaji wa CCM kupata kura. Kwa maana hiyo CCM watataka muendelee na hali hiyo ili waendelee kupata kura zenu ki-ulaini. Angalia sehemu zote wanazoonesha opposion kwa CCM halafu linganisha na sehemu ambazo ni royal kwa CCM? Be the judge yourself.

Mkiikataa CCM tu mara moja utaona mara ya pili kama mtairudisha mbunge wenu anakuwa naibu waziri, gati inajengwa etc. CCM wanachukuliwa kura zenu for granted ndiyo maana hawafanyi juhudi zozote za kuwaondolea UJINGA na UMASIKINI wenu kwasababu ndiyo mtaji wao.

Elimu ya uraia ni mhimu kwa kila mwananchi kufahamu kwamba kura yake ndiyo inamuajiri Rais, Mbunge, Diwani etc. Wenzetu wamendelea kwasababu hiyo tu.
 
Poleni sana. Kwnza niwajulishe kwamba nyerere aliacha uongozi siku nyingi na alishakufa tangu 2009 oktoba. Alikuja Mwinyi naye kaacha tangu 1995. Alikuja Mkapa naye kaacha tangu 2005. Hao waliongoza nchi na labda mulipiga kura bila kujuwa munayemchagua. Sasa tangu 2005 kuna mtu anauza sura pale ikulu, sijui ni nani ila kwenye vyombo vya habari nasikia katokea MSOGA Bagamoyo. Wengine wanasema huyo jamaa musitegemee kuletewa maendeleo, umeme, barabara wala zahanati. Siku akikosea njia kuja huko atawaagiza mujitegemee tujenga shule ya kata lakini hataleta walimu mpaka YESU mwokozi arudi. Huyo jamaa anamaliza 2015 hivyo kama munataka maendeleo WOTE HAMIENI CHADEMA NA 2015 CHAGUENI CHADEMA ILI IWAKOMBOE UTMWANI CCM.
 
Mkuu UMMATi,
Shukrani kwa ujumbe, nitaufikisha ujumbe huo kwa nguvu zote, ila pia hao wapambanaji wanatakiwa waje kutoa semina elekezi kwa wananchi huku!
 
Bw mzizi, ahsante kwa kutujuza mimi nilikuwa sinalo hilo,ila mafia mmbunge tuliyenaye ni mbumbumbu,ki upeo hata uwezo wa akili yake,analaghai kwa salam alykum na kujifanya muungwana. sasa maji yale pale hayatoshi hospitali, hayatoshi majengo wala kurungeni na msitu ndio huo tu unaotegemewa kutunza maji.sijui anawapigania watu gani.labda kila mtu awe na kisima chake sasa. nyundo uko wapi bw ulisema utagombea au umeogopa muhali? mzizi itabidi uni pm

Mkuu nipo, tunaendeleza harakati! Hayo ya mambo ya Mafia yanahitaji umakini mkubwa kuyazungumzia, inawezekana pia ikawa ni siasa, ila cna maana ya kwamba yapuuzwe! Kuhusu mimi kugombea hilo ni suala la muda, muda mwafaka ukifika nitatoa kauli, kuhusu 2010 mda wetu nadhani ulikuwa haujafika!
 
kama utaweza kuwashauri na wenzako itapendeza sana...isije ikawa peke yako ndo unajivua gamba.
 
Hao wanagundua hilo leo? Anyway mmefanya maamuzi sahihi mabaharia!
 
Mkuu nipo, tunaendeleza harakati! Hayo ya mambo ya Mafia yanahitaji umakini mkubwa kuyazungumzia, inawezekana pia ikawa ni siasa, ila cna maana ya kwamba yapuuzwe! Kuhusu mimi kugombea hilo ni suala la muda, muda mwafaka ukifika nitatoa kauli, kuhusu 2010 mda wetu nadhani ulikuwa haujafika!

wewe bw kijana, unafaa, elim inatosha ujanja unatosha, ukoo uaofahamika kumbuka (sokomoko).angalia ile mafia documentary, wanajifanya wanatoa msaada vyandarua na uwanja wa mpira. sijui lakini mimi sijaona cha msingi pale. labda walichofanya ni kupata picha za video za kuwafanya waendelee kuihadaa dunia kupata misaada ili waendelee kupanda british airways. kama tunahitaji umakini kuyazungumza ni pm ili tupate points ambazo pengine si wote tunazifaham.lakini kwa majina niliyoyasikia wewe ni mzalendo mwenye uwezo, jitahidi uwaokoe jamazo
 
Mkuu nipo, tunaendeleza harakati! Hayo ya mambo ya Mafia yanahitaji umakini mkubwa kuyazungumzia, inawezekana pia ikawa ni siasa, ila cna maana ya kwamba yapuuzwe! Kuhusu mimi kugombea hilo ni suala la muda, muda mwafaka ukifika nitatoa kauli, kuhusu 2010 mda wetu nadhani ulikuwa haujafika!

au uliogopa muhali ukienda usewe utakosa madafu? madafu ata hapo si yapo bw?
 
Wewe ni nani mpaka usemi wako ndio uwe usemi wa watu wote wa mafia? Matatizo uliyosema sio ya mafia tu ni sehemu nyingi tu za Tanzania, kumbuka kura yako ni moja tu, unless hayo uliyosema uwe kweli umetumwa na wana mafia.
 
Tumevumilia tumeshindwa, Mbunge wa kipindi flani alitangaza nia ya kujitenga wakamzima. Sasa nadhani tunahitaji kufikiria upya hilo. Kwani rasilimali tunazo, kama bahari nzuri kwa uvuvi, fukwe nzuri kwa utalii, tuna gesi kama songo songo, zao la nazi, korosho na mabonde mazuri ya kilimo pamoja na kina cha maji ya kutupatia bandari nzuri.
Kwani tumechoshwa na unyonyaji na dharau!
Kwa sasa hakuna kiongozi yeyote wa chama hapa mafia anayejishughulisha na mambo ya chama, kwani hata hao viongozi wa chama wamekosa hata hoja za kuwajibu wananchi kwa sasa, kwani ahadi zimejirudia mara nyingi bila utekelezaji, sasa imebaki stori tu. Hata huyo mbunge wa Mafia amekosa hata usema huko bungeni, nadhani nyinyi ni mashahidi, inawezekana hata kumfaham hamumfahamu. Viongozi wa serikali ya ccm wamedhurumu maeneo ya ardhi za walalahoi wa mafia na kuuzia wawekezaji uchwara, sas ni migogoro ya ardhi ndio urithi wao, kuna kijiji kimoja nilitembelea na kuambiwa wanakijiji wote wameshitakiwa kwa kosa la uvamizi wa eneo. Karibuni mtasikia yaliyotokea huko tarime yakitokea mafia. Kwa sasa ni wakati mzuri sana kwa chama kinachohitaji kuungwa mkono kufika mara moja, kwani wananchi kwa kweli wamekata tamaa

CDM ratibuni ziara ya kanda ya kusini; na mafia kiwe kituo muhimu.
 
Ndugu yangu pole. Mimi kama mwana jamiiforums nasikitika kwa majibu uliyopewa na wana ccm wenzako kwa kuwatukana ndugu zetu wa Mafia. ccm ndivyo walivyo wameshindwa kuwaendeleza sasa wanawatukana. Tena huyo aliyekujibu ana cheo kikubwa ccm.
POLENI SANA.
 
Asante mzizi, nimejifunza mengi kuhusu mafia, napata moyo kuona kuna watz wameamka sasa amsheni na wenzenu walofanywa kafara na chama cha mazingaombwe na ahadi fix
 
Wewe ni nani mpaka usemi wako ndio uwe usemi wa watu wote wa mafia? Matatizo uliyosema sio ya mafia tu ni sehemu nyingi tu za Tanzania, kumbuka kura yako ni moja tu, unless hayo uliyosema uwe kweli umetumwa na wana mafia.

Wewe kama umekariri kama lazma uwe maarufu ama cheo ndio usemee matatizo ya watu ndio usikike basi utakuwa ni mmoja kati ya waliotufikisha hapa tulipo. Unakumbuka kilichomfanya Brown akose u PM uingereza? Ni kudharau mama mmoja tu mchovu ambaye alikuwa anahoji sera ya uhamiaji,, jamaa akasau kuzima kinasa sauti, safari yake ikaishia hapo! Mimi ni mwananchi wa kawaida kabisa masikini lakini ni mtanzania.
Kura yangu moja usiidharau kabisa, kwani in thamani kubwa sana.
Matatizo ni kweli yapo kila sehemu, lakini si kweli kwamba hapa tanzania kuna wilaya inakosa shule ya high school hata moja, kama ipo nitajie, kuna wilaya tangu uhuru imekosa kiongozi wa kuteuliwa kwenye serikali kwa ngazi yoyote ile, kuna wilaya inakosa hakimu wa mahakama ya mwanzo na wilaya miezi ama mwaka mzima, na haya yanahitaji cheo kuyasema?
Mawazo kama haya ndio yanayoipeleka ccm kuzim,
Na ww kama ni mmoja wa viongozi basi hufai kuongoza hata nyumba kumi, jivue gamba na uache dharau
 
Ndugu yangu pole. Mimi kama mwana jamiiforums nasikitika kwa majibu uliyopewa na wana ccm wenzako kwa kuwatukana ndugu zetu wa Mafia. ccm ndivyo walivyo wameshindwa kuwaendeleza sasa wanawatukana. Tena huyo aliyekujibu ana cheo kikubwa ccm.
POLENI SANA.

Kaka hao wanaotoa matusi wapo kivulini. Sisi tulio juani ndio tunaeona machungu. Ila mwisho wao utafika, kwa heri ama kwa shari! Mwisho ni mwisho tu!
 
Sehumu zote wanakoshabikia Magamba hali ziko hivyo lakini kwenye nguvu ya umma hakuna uhuni kama huo. Kazi ni kwenu watu wa mafia
 
ccm ni tumaini lililozimika, wale wote wenye macho ya kuona, masikio ya kusikia na ufahamu wa kuelewa mambo wanafanya maamuzi ya kuikikimbia, pamoja na kwamba kelele za kusema ''tunafanya maamuzi magumu ooo tunavua gamba ooo tunaoondoa mafisadi ktk NEC haitasaidia'' kwa hiyo Mafia fanyeni haraka kuondoka humo hiyo chama kitawadidimiza kabisa kimaendeleo.
 
Hilo gati likowapi mlilotuahidi? Au ndio uchaguzi umeshapita? Shame on you magamba
 
Back
Top Bottom