Mafia boxing mipambano yenu ya ovyo

Mafia boxing mipambano yenu ya ovyo

masai dada

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
17,377
Reaction score
19,264
Rafiki yangu mmoja kapigana usiku uliopita, hivyo imenibidi nimpe support.

Watu wanakesho, halafu mnakuja kutoa judgment za kijinga. Sijawahi kuona mabondia wazuri wakipewa nafasi, ila mnaendekeza utanga

Mtu kama Ibra Classic mngemchukua mkampa hizi nafasi mnazowapa mabishoo.

Rafiki yangu yupo under Mafia, lakini kidogo alitembeza mkono—yaani kidogo sana. Alipoteza, lakini majaji wamempa ushindi. Sijaongea naye tangu nimefika home; yaani naona hadi aibu.

Aisee... napata hasira.
 
rafki yangu mmoja kapigana usiku uliopita so imebidi nikampe suport....

watu wanakesho afu mnakuja kutoa judgement za kijinga sijawah ona
mabondia wazuri wapo ila mnaendekeza utanga
mtu kama ibra classic mngemchukua mkampa hizi nafasi mnazowapa mabishoo
rafk yangu yupo under mafia ila kidogoo alitembeza mkono...yaani kidogo sana ila alipoteza lakini majudge wamemba..mi sijaongea nae tangu nimefika home yaani naona hadi aibu
aiseee ....napata hasira
Rafiki yako naye kabebwa sio 😃😃😃
 
Nilikuwa nikisikia kuna vitasa nilikuwa nahakikisha nawahi kwenye TV naangalia mapambano yote mwanzo mwisho mpaka usiku wa manane. Kuna siku bondia mtanzania alitandikwa na bondia wa nje (siwakumbuki majina) toka raundi ya kwanza mbongo anakula kichapo mwamnzo mwisho. Kuja kwenye matokeo majaji wakampa mbongo ushindi. Toka siku hiyo nikasema mimi na ngumi za kibongo basi. Majaji wetu jau sana. Wakiona mbinu ya kumpa bondia wanayemtaka ushindi imeshindikana kabisa basi utasikia wametoka sare wakati watu wote wanaona mmoja kapigwa kabisa na mwingine kashindwa. Saa nyingine unaona kabisa hata bondia aliyepewa ushindi kwa utata au sare ya utata yeye mwenyewe anaona aibu.
 
Niliacha mambo ndondi kwasababu hizi hizi... hata kocha wangu baada ya kuona mazingira yetu akanipa option nihame na kuomba urai nje kama napenda sana mchezo wa ndondi ila kama hapa hapa aka akaniambia nisipoteze mda
 
Rafiki yangu mmoja kapigana usiku uliopita, hivyo imenibidi nimpe support.

Watu wanakesho, halafu mnakuja kutoa judgment za kijinga. Sijawahi kuona mabondia wazuri wakipewa nafasi, ila mnaendekeza utanga

Mtu kama Ibra Classic mngemchukua mkampa hizi nafasi mnazowapa mabishoo.

Rafiki yangu yupo under Mafia, lakini kidogo alitembeza mkono—yaani kidogo sana. Alipoteza, lakini majaji wamembania. Sijaongea naye tangu nimefika home; yaani naona hadi aibu.

Aisee... napata hasira.
Nimetazama nimepatwa na kichefuchefu kwanza yapo kisiasa na uhalisia wa kimashindano haupo,knock out zote naweza ziita full mchongo labda angalao moja.
 
Hassan Mwakinyo yupo mbele ya muda.
Daa huyo naye ana yake. Watanzania tulikesha tunamuombea ashinde mkanda wa dunia. Alichotufanyia watanzania ndio ikawa laana kwake mpaka leo haujulikani anaenda mbele au anarudi nyuma. Ile bahati aliyoipoteza sidhani kama itakaa irudi maishani mwake. Kibaya zaidi akatuona watanzania wote mazwazwa eti viatu vilimbana.
 
Nimetazama nimepatwa na kichefuchefu kwanza yapo kisiasa na uhalisia wa kimashindano haupo,knock out zote naweza ziita full mchongo labda angalao moja.
mafia wangejua kwa stahili hii pia wanaua viwango vya mabondia
cause bondia atamtegemea judge
 
Daa huyo naye ana yake. Watanzania tulikesha tunamuombea ashinde mkanda wa dunia. Alichotufanyia watanzania ndio ikawa laana kwake mpaka leo haujulikani anaenda mbele au anarudi nyuma. Ile bahati aliyoipoteza sidhani kama itakaa irudi maishani mwake. Kibaya zaidi akatuona watanzania wote mazwazwa eti viatu vilimbana.
Kwenye mchezo kuna kushindwa,sare au kushindwa.
 
Daa huyo naye ana yake. Watanzania tulikesha tunamuombea ashinde mkanda wa dunia. Alichotufanyia watanzania ndio ikawa laana kwake mpaka leo haujulikani anaenda mbele au anarudi nyuma. Ile bahati aliyoipoteza sidhani kama itakaa irudi maishani mwake. Kibaya zaidi akatuona watanzania wote mazwazwa eti viatu vilimbana.
mwakinyo alizungua sanaaa
ya kwanza eti viatu
ya pili eti chumba sijui imekauje

hivi kweli bondia mzoevu ambae anategemea kuingia kwenye level za kidunia
vitu kama hivyo kweli ni vya kuwa sabbu kuu ya kuzingua???
naujua ugomvi wao na mafia ila na yeye mwakinyo kuna namna aliziuza zile mechi..

ugomvi wa mwakinyo na mafia ulianza kwamba mwakonyo hataki kubeba wenzake wa kutoka tanga...yaani kuwafungulia kimataifa
au hata bongo hapa mapambano ya mwakinyo hamna mtoto anaetoka tanga anapanda
so wanajaribu kumzalisha mwakinyo mwingine🤣🤣 ndo huyo bishoo aliyepigwa na akashinda
 
Niliacha mambo ndondi kwasababu hizi hizi... hata kocha wangu baada ya kuona mazingira yetu akanipa option nihame na kuomba urai nje kama napenda sana mchezo wa ndondi ila kama hapa hapa aka akaniambia nisipoteze mda
sure....
yaani tena kwa sasa kama upo nje ha mfumo sahau
 
Nilikuwa nikisikia kuna vitasa nilikuwa nahakikisha nawahi kwenye TV naangalia mapambano yote mwanzo mwisho mpaka usiku wa manane. Kuna siku bondia mtanzania alitandikwa na bondia wa nje (siwakumbuki majina) toka raundi ya kwanza mbongo anakula kichapo mwamnzo mwisho. Kuja kwenye matokeo majaji wakampa mbongo ushindi. Toka siku hiyo nikasema mimi na ngumi za kibongo basi. Majaji wetu jau sana. Wakiona mbinu ya kumpa bondia wanayemtaka ushindi imeshindikana kabisa basi utasikia wametoka sare wakati watu wote wanaona mmoja kapigwa kabisa na mwingine kashindwa. Saa nyingine unaona kabisa hata bondia aliyepewa ushindi kwa utata au sare ya utata yeye mwenyewe anaona aibu.
mkuu jana ndo ilikua kichefuchefu
kama yule mtoto karusha clean punch ..basi hazizidi 6
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom