Mafao ya NSSF yachukua sura mpya Ilala

Wakuu Niko hapa ofisi za NSSF Ilala karibu na Mwalimu Complex nafuatilia mafao yangu baada ya kuachishwa kazi katika kampuni moja ya kichina mwaka mmoja uliopita.

Lakini hali iliyopo hapa, watu wamepandwa na hasira baada ya kuambiwa hawawezi kupata mafao yao kwasababu shirika liko kwenye uchunguzi wa kubaini kama kweli fomu zilizowasilishwa kuomba mafao ni za watu walioachishwa kazi.

Kaka mmoja analalamika kuwa alifungua madai Juni mwaka Jana akaambiwa akae miezi 6. Aliporudi akapigwa miezi 3 tena.

Leo karudi anaambiwa baada ya mwaka 1 mpaka wakamilishe uchunguzi.

Wafanyakazi wa NSSF waliopo hapa wana wakati mgumu kuwatuliza watu kwasababu majibu yanayotolewa hawakubali.

Changamoto nyingine, wakiomba waonyeshwe sehemu ya kutoa malalamiko kwa uongozi wa shirika wamegoma na wanasema lazima wakubaliane na utaratibu uliopo.
wanawapiga kalenda ili mfe..
ila acheni utani hakuna shirika ambalo lipo makini kama PPF. sijui wengine ila hawa jamaa hawakuniletea longo longo hata siku mooja nilikuwa napata huduma utadhani nipo kwenye migawaha ya macdonald ama subway
 
Pesa za nssf zote zinatumika kujengea fly over za tazara na ubungo.. kuweni na subira tu.. mkifa kabla hamjapata serikali itazitumia kuboreshea miundo mbinu ya nchi yenu wapendwa.
 
Nadhani tunakoelekea hili jambo la kuwekeana mafao liwe ni jambo la hiari. Maana pesa zinapelekwa huko kwa kukatana mishahara yetu ila ukifika muda unazitaka pesa zako namna kuzipata ni ngumu utadhani unaomba pesa ya msaada. Sio vizuri NSSF Mungu anawaona.

Dalili ya watu kukata tamaa ni kila kitu kumwachia Mungu, kauli za mungu anawaona ni kauli za kukata tamaa kweli kweli... inauma sana...
 
Mama angu ni nesi ,anastaafu feb!
Sijui yuko mfukp gani!

Hakyamama sijui itakuaje
 
Izzi ni akili za kuumiziakichwa fisifisi
Serikali imekosa wa kudhurhmu imehamia kwa mafao ya wanyonge

Bora kidogo nssf kuliko Ppf ambao wanasema hawatoi mafao kabisa inaniuma saaana
 
Nadhani tunakoelekea hili jambo la kuwekeana mafao liwe ni jambo la hiari. Maana pesa zinapelekwa huko kwa kukatana mishahara yetu ila ukifika muda unazitaka pesa zako namna kuzipata ni ngumu utadhani unaomba pesa ya msaada. Sio vizuri NSSF Mungu anawaona.

whitehorse ,
Mkuu,
Tukichanganya Mungu na haya yanayotendwa inakuwa siyo Sawa.

Huyo Mungu anasisitiza haki ila hawa kuwaachia Mungu awaone ni kupoteza muda.

Dawa yao ni 2020 kila anayepitisha sheria za hovyo huko bungeni kwenye jimbo apate kura mbili tu yaani ya mke wake na yake mwenyewe.

Hapo ndiyo Mungu atawaona vizuri.

Ila wakipata kura zote na kushinda wataendelea kupitisha sheria uchwara na kupitishwa bila kipingwa.

Any way, vyama vya wafanyakazi, walimu vyote naona hakuna wanachokifanya zaidi ni kusifu na kuabudu tu.
 
Mtamkumbuka sana Dr Dau! Enzi zake, mafao yalikuwa yanachukua wiki moja tu! Yani ukijaza fomu zote zikakamilika leo, unaambiwa njoo baada ya wiki moja uchukue cheki yako! Na kweli ukienda unakuta cheki iko tayari kabisa. Sasa mtaisoma namba... The downfall of Dr Dau was a downfall of the many... Ndio hapa tujifunze watanzania tuache majungu kwa kuwa hayajengi!
 
Kuwe na makampuni binafsi ya mafao ya watumishi,kwisha!!

Mkuu,
Wazo lako halina nafasi tena kwa hawa wakwapuaji wa hela za wanyonge.

Wana jiandaa kuunganisha mifuko yote na kuwa miwili tu, mara utabaki mfuko mmoja.

Yaani ni valuvalu na vyuma kukatika kweli kweli.
 
SSCRA kazi yao ni hipi? Au hicho kiliundwa ili watu wapate ajira tu?

Hiyo ni ajira kwa vilaza wa vigogo ilitengenezwa.

Mifano ni mingi angalia hata hawa Public Procurement Regulatory Authority (PPRA) wanafanya ujinga tu pale Mjini hakuna wanachokifanya wala wanachokielewa.
 
kuna watu wanadhani uongozi mbaya wa nchi utawadhuru wapinzani tu.....kwa hiyo endeleeni kushabikia ccm....
 
Wakuu Niko hapa ofisi za NSSF Ilala karibu na Mwalimu Complex nafuatilia mafao yangu baada ya kuachishwa kazi katika kampuni moja ya kichina mwaka mmoja uliopita.

Lakini hali iliyopo hapa, watu wamepandwa na hasira baada ya kuambiwa hawawezi kupata mafao yao kwasababu shirika liko kwenye uchunguzi wa kubaini kama kweli fomu zilizowasilishwa kuomba mafao ni za watu walioachishwa kazi.

Kaka mmoja analalamika kuwa alifungua madai Juni mwaka Jana akaambiwa akae miezi 6. Aliporudi akapigwa miezi 3 tena.

Leo karudi anaambiwa baada ya mwaka 1 mpaka wakamilishe uchunguzi.

Wafanyakazi wa NSSF waliopo hapa wana wakati mgumu kuwatuliza watu kwasababu majibu yanayotolewa hawakubali.

Changamoto nyingine, wakiomba waonyeshwe sehemu ya kutoa malalamiko kwa uongozi wa shirika wamegoma na wanasema lazima wakubaliane na utaratibu uliopo.

Wito wangu ni huu!

Msiache kujishughulisha na shughuli nyingine zakuwaingizia vipato wakati mkisubiria hizo hela zenu huko nssf.

Sijawahi kusikia matajiri wakilalamikia hizo hela ila sisi masikini. Ni Muhimu sana tukawa makini na muda muda.

Nguvu nyingi tunayoiweka kwenye kudai mafao inatunyima nafasi ya kuwa creative na productive na muda.

Tafuteni namna nyingine ya kuwaingizia vipato was mkiwa mnafuatilia mafao. Hili litawapunguzia hasira. Wakati mwingine kosa au tatizo sio shirika, lakini kama huna hela ya kula mfukoni ni rahisi kuhisi ama kudhani mnahujumiwa.

I stand to be corrected, mimi pia nimeajiriwa. Ipo siku na mimi nitahitaji hizo hela, Mwenyezi Mungu anijalie busara.

Kulalamaika kinadhoofisha sana Mwili na Akili.
 
Aisee nitaomba update mtakapofanikiwa nami nifatilie mzigo wangu, Nssf morogoro kuna kamama kamoja kalinijibu hayo sishughuriki nayo mm....ila nilikasitiri kwakuwa hakanijui nilivyo na misala, nashukuru Mungu sikukapa vibao nadhani ningekuwa mahali pengine leo, nasubiri update yako nami nifike Arusha nikadai mafao yangu rasmi...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom