Kande
Senior Member
- Mar 15, 2016
- 116
- 106
Wakuu Niko hapa ofisi za NSSF Ilala karibu na Mwalimu Complex nafuatilia mafao yangu baada ya kuachishwa kazi katika kampuni moja ya kichina mwaka mmoja uliopita.
Lakini hali iliyopo hapa, watu wamepandwa na hasira baada ya kuambiwa hawawezi kupata mafao yao kwasababu shirika liko kwenye uchunguzi wa kubaini kama kweli fomu zilizowasilishwa kuomba mafao ni za watu walioachishwa kazi.
Kaka mmoja analalamika kuwa alifungua madai Juni mwaka Jana akaambiwa akae miezi 6. Aliporudi akapigwa miezi 3 tena.
Leo karudi anaambiwa baada ya mwaka 1 mpaka wakamilishe uchunguzi.
Wafanyakazi wa NSSF waliopo hapa wana wakati mgumu kuwatuliza watu kwasababu majibu yanayotolewa hawakubali.
Changamoto nyingine, wakiomba waonyeshwe sehemu ya kutoa malalamiko kwa uongozi wa shirika wamegoma na wanasema lazima wakubaliane na utaratibu uliopo.