SoC02 Mafanikio

Stories of Change - 2022 Competition

Ibojr

New Member
Jul 24, 2022
3
3
MAFANIKIO

KAMA ilivyo ada kila mtu anahitaji kuwa na mafanikio katika maisha yake. Vivyohivyo hata mimi ninatamani kuwa miongoni mwao.

Swali la kujiuliza ni kwanini tuliowengi hatufanikiwi na wachache kati yetu ndio hufanikiwa? Inakupasa kujiuliza kwa makini nini ufanye ili na wewe ufanikiwe na sio kulalamika au kuwasema vibaya wale waliofanikiwa zaidi yako. Naamini njia za kufikia mafanikio ziko nyingi sana na zinatofautiana kutokana na mazingira tuliyopo hivyo basi kinacho hitajika ni kutambua mazingira uliyopo na kufanya maamuzi sahihi.

Mimi naamini kuna uzio mdogo sana mithili ya uzi wa kufumia nguo ili kuyafikia mafanikio ila wengi wetu huona kama vile ni ukuta mkubwa mithili ya ukuta wa Berlin. Inahitajika nguvu kubwa sana ya kiakili kisha nguvu kidogo sana ya kimwili kupenya katika uzio huo na kua miongoni mwa watu waliofanikiwa kimaisha.

Ili mtu aonekane amefanikiwa kimaisha lazima awe na kipato kizuri hivyo basi fedha/ngawira ama kwa jina lingine Ankara zisiwe zinamsumbua hiyo ni tafsiri ya ujumla ya mafanikio.

Hata tajiri maarufu duniani namzungumzia Bill Gate hatuhesabu idadi ya kampuni alizonazo bali tunazithaminisha kampuni alizonazo. Labda nikupe mfano rahisi kwa kule kwetu Umasaini ili uwe tajiri wa kijiji lazima umiliki idadi kubwa ya ng’ombe,mbuzi na kondoo kwa mantiki hiyo ili kumpata tajiri wa nambari moja wa kijiji hautochukua idadi ya mifugo bali thamani ya mifugo ya mfugaji,ni mfano mdogo tu nataka ukuamshe kimawazo.Hivyo basi huwezi kua na mafanikio ya kimaisha pasipokua na fedha au vitu ambavyo vinathamani.

Tajiri mmoja maarufu duniani aliwahi kuhojiwa kuhusiana na mafanikio yake aliulizwa hivi:-

1.‘‘Ni kitu gani kimekufanya uwe tajiri mkubwa leo hii wakati tunajua umetokea katika familia ya kimasikini sana?’’

2.‘‘Je kuna uwezekano wewe kufilisika na kurudi katika umasikini tena?”


Tajiri yule alicheka kwa sauti ndogo kana kwamba alikua akitabasamu tu kisha baada ya muda kidogo akaanza kwa kusema

Kwanza ‘‘kitu kikubwa kilichonipa utajiri ni UVIVU simaanishi UVUVI nimaanishacho ni uvivu unaoujua wewe kitu kingine kwa kuongezea sijawahi kutafuta fedha katika maisha yangu na mpaka nakufa sitowahi kutafuta fedha”

Pili “sitokaa nikafilisika maishani mwangu” muulizaji alihamaki kama mimi na wewe tulivyopigwa na butwaa kwa sasa ila alichomuuliza ni kwanini unasema hivyo? Tajiri yule alijibu kwa mapana kwa kusema hivi:-

Yeye huwa ni mvivu sana vilevile ni mchapakazi wa hali ya juu. Namaanisha mvivu wa mwili lakini mchapakazi wa akili. Anasema ili mtu ufanikiwe inakupasa uwe mvivu kimwili lakini mchapakazi kiakili kwani utakapokua na minguvu sana kila kitu kikukabilicho utahitaji kutumia nguvu kukitatua ili kuonesha umwamba wako hatakama ni kufunga mlango utataka kuubamiza kwanguvu pasipo na sababu za msingi lakini ukiwa huna nguvu au mvivu utataka kutumia hata remote control kufunga au kufungua mlango akatoa mfano kwa kusema:- walioanzisha utumwa duniani ni jamii ya wahindi wekundu waliokua wakiishi MAREKANI miaka mingi iliyopita, jamii hio ilikua dhaifu sana kimiili hivyo basi maisha yao yalikua magumu sana kwa mfano wakitaka kula lazima wawe wengi ili kumuuwa swala au sungura hali iliyo wapelekea kuumiza vichwa vyao ili kutafuta ufumbuzi au njia rahisi kwa kila jambo wanalotaka kulifanya kutokana na hali hio waliamua kusambaa ulimwenguni kwa ajili ya kutafuta watu wakuwasaidia majukumu yao,hapo ndipo chimbuko halisi la utumwa lilipoanzia.

Hali hio iliendelea kwa muda mrefu lakini bado hawakuridhishwa na matokeo kwasababu watumwa ni binadamu kwa maana hiyo huchoka na kufa pia.

Hivyo basi waliamua kuachana na biashara ya utumwa na kuanza harakati za mapinduzi ya viwanda duniani.

Kumbe basi ili tufanikiwe tunahitajika kuwekeza nguvu za ziada katika mikakati kwanza halafu utendaji ufuatie kwani ukianza na kutenda bila kua na mikakati madhubuti hutofikia lengo.Najua kwa kiasi fulani utakua umeshaanza kujifunza kitu hapo.

Kwa kuongezea tuu inasemekana miaka 1000 ijayo kuanzia sasa sekta zote unazozifahamu wewe hakutakua na watendaji wa moja kwa moja katika nyanja hizo kwani mashine ndio zitakazokua zikifanya kazi kwa asilimia 98 huku asilimia 2 tuu ndio wanadamu. Hiyo ni kwa takribani sekta zote isipokua sekta moja tu ya siasa kwani inahitaji ushiriki wa binadamu kwa asilimia lukuki. Hebu jaribu kufikiria jimboni kwako kuwe na mbunge ambaye ni Roboti inawezekana kweli? vipi kuuziwa nyanya au vitunguu na Roboti? Inawezekana eeeh!kwa kiasi kikubwa sana.Kwasasa Ulaya ni kitu cha kawaida walianza na mbwa sasa ni Mashine yaani roboti.

Kitu kingine ni kutafuta fedha.Najua wengi wetu kila kukicha tunatafuta fedha za kujikimu sisi na familia zetu sasa nashangaa tajiri kama yeye kusema hajawahi kutafuta fedha na hatokaa akatafuta fedha,tusimnukuu vibaya alichokua akimaanisha ni hichi :-

Kila kitu katika ulimwengu huu kina njia zake,ili uishi lazima uzaliwe,ili ufike peponi au mbinguni lazima ufe. Kuzaliwa na kufa hizo ni njia za kutufikisha pahala fulani vijana wa siku hizi wanaamini ili umpate binti mzuri lazima uhonge hio si maana yangu mimi ni imani ya vijana na sitaki kuwaingilia hata kidogo. Kwa wale wapenzi wa mpira wanaamini mpira wa miguu unanjia zake sio kama zama zetu unatoka na mpira goli hadi goli hapana saivi unaweka kwenye njia tu! kwa maana ya ujumla ni Mfumo ama Formation kama wanavyosema wenye lugha yao.

Hivyo hivyo ili upate fedha huhitajiki kutafuta fedha unachopaswa kufanya ni kushika mifereji ama njia za fedha kwani hakuna kitu kisichokua na njia yake yakupita iwe zionekanazo au zisizoonekana kwa macho lakini ni njia. Kwahio naanza kumuelewa tajiri yule alivyosema hajawahi kutafuta fedha na hatotafuta fedha mpaka anakufa kwani nahisi alichofanya ni kutafuta njia ambazo anaamini fedha zinapita na kuzishika.

Kuhusu kufilisika imani yake kubwa ni kwamba hatoweza kufilisika kamwe endapo tuu masikini au watu wenye uwezo mdogo au kipato cha chini wataendelea kuwepo duniani kwasababu utajiri wake umeshikiliwa na masikini sio matajiri. Usilolijua masikini ni jeshi kubwa ulimwenguni ambalo unaweza kuliamini asilimia 90 endapo tuu huduma unazozitoa zinawagusa moja kwa moja katika maisha yao ya kila siku. Kama huniamini nakupa hii kama mfano hai mko katika mizunguko yenu ya kawaida wewe na rafiki yako kipenzi kwa bahati nzuri mkaona bidhaa kisha kuvutiwa nayo,kutokana na ubora wa bidhaa hio mkaamua kila mmoja wenu anunue ya kwake. Wakati wa malipo wewe ukatoa noti ya shilingi elfu kumi na rafiki yako akatoa noti ya shilingi elfu mbili. Kabla ya kumkabidhi muuzaji fedha zenu ili awapatie chenchi mkafikiria si bora alipie tuu mmoja wenu! Je wewe mwenye noti ya elfu kumi ndo utalipia au rafiki yako wmenye noti ya shilingi elfu moja? Kumbuka noti zote zinathamani au uwezo wa kununulia bidhaa hiyo.

Naamini ukiwa unatabia ya kusoma makala mbalimbali utajifunza vitu vya msingi ambavyo vitakusaidia katika maisha yako ya kila siku penda kujifunza kila paitwapo leo Ahsante kwa muda wako.
 

Attachments

  • MAFANIKIO by Iddy Bakari Omari.docx
    26.6 KB · Views: 3
Back
Top Bottom