Mafanikio yasikupe kiburi na jeuri

Mafanikio yasikupe kiburi na jeuri

Pia usinisahau na mm kesho naweza kuwa kama sponsor
Kabisa kabisa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] karibu unisponse na wewe
 
Magesa Mulongo hajawahi kuwa RC Pwani. Wakati Majaliwa ni DC Rufiji, Magesa alikuwa DC Bagamoyo. Ma RC wa Pwani wakati huo walikuwa ni Christine Ishengoma, Hajat Amina Mrisho na baadaye Mwantumu Mahiza.
 
Na wewe ulikuwa DC wa wapi
 
Safi Sana ndugu na hongera kwa inspirational message to night, GOD BLESS YOU
 
Wakati Majaliwa akiwa DC Rufiji, alikua anaripoti kwa RC Pwani Magesa Mulongo na Waziri wa TAMISEMI Stephen Wassira. Leo wote wawili hawapo tena serikalini.

Majaliwa alipoteuliwa Naibu Waziri TAMISEMI alikua anaripoti kwa Kepteni George Mkuchika. Leo mzee Mkuchika ndiye anayeripoti kwa Majaliwa.

Maisha ni mzunguko. Ukifanikiwa usijae kiburi ukadhani ndio mwisho wa safari. Al-Bashir alikua na madaraka makubwa na pesa nyingi. Lakini leo ni mfungwa. Anakula, kulala na kuamka kwa amri. Hana tena hiyari ya maisha yake.

Na pia ukikosa leo usikate tamaa ukadhani Mungu amekuacha. Bado lipo tumaini. Anayekudharau kwa sababu ni 'Housegirl' kesho unaweza kuolewa na Rais ukawa First Lady na akakuheshimu.

Wana wa Israel walipowekwa mateka kule Babeli, Esta na mjomba wake Mordekai walikua watumwa. Esta akachukuliwa na Hegai kuwa kijakazi kwenye nyumba ya Mfalme.

Hegai alikua kama 'Afisa Utumishi' kwenye kasri la mfalme Ahasuero. Vijakazi wote wa mfalme waliripoti kwake akiwemo Esta. Lakini baadae Esta akawa Malkia, na Hegai akawa anaripoti kwa Esta. Life is circle.

Hakuna aliyejua kiongozi mwenye ulinzi mkubwa na fedha nyingi kama Gadafi siku moja angeweza kujificha kwenye mtaro wa maji taka kama mwizi wa kuku wa Gongo la Mboto.

Usijivune kwa kufanikiwa leo, na usivunjike moyo kwa kufeli leo. Winston Churchill aliwahi kusema "Success is not final, and failure is not fatal. It is the courage to continue that counts"

siku njema kwako.

Andiko lako linaweza kuwa zuri ila kuna watu dunia hii wasiokuwa nacho badala ya kujifariji siku moja watapata, wao wamekuwa wachawi na wenye roho mbaya kwa wenye nacho na hutamani mabaya kwa walionacho, kubeza na kushika miguu ya walionacho badala kutafuta namna ya wao kufika hapo kwa bidii na njia halali zitakazowanyanyua.
 
Ni
Kweli
Mkuu
 
Back
Top Bottom