Mafanikio yana sauti -Quick Rocka

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,650
2,000
Quick Rocka 'Switcher' msanii anayesumbua masikio ya wapenda burudani na ngoma ya 'down' amewajibu wanaohoji mafanikio yake kuwa makubwa kuliko muziki kwa kusema siku zote mafanikio yana sauti kuliko mihangaiko.

Mbele ya kamera za eNewz ya EATV Rocka amesema kwamba mara nyingi watu wa nje hawawezi kujua ni kwa muda gani amekaa benchi kutafuta nafasi aliyonayo leo hivyo ni sahihi kwa wao kuzungumza kwamba anamafanikio mengi kuliko kazi zake za muziki.

"Mafanikio huwa yanaonekana zaidi kuliko Struggle, kipindi nahangaika hakuna mtu alikuwa anajua napata tabu kiasi gani kujitengeneza kuwa mtu wanayemuona sasa zaidi ya watu wangu wa karibu. Nina biashara za familia ninazosimamia, Lebo ya muziki na wasanii wake, studio na mambo mengine mengi lakini hayo watu hawayaoni, na mimi nitawaacha waendelee kuongea huku nikiendelea na kazi zangu", Quick Rocka alifunguka.
 

Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
42,861
2,000
Yeah ni kweli watu wengine hawajui watu wanavyostruggle...Jamaa ni mpambanaji
[HASHTAG]#Switcher[/HASHTAG]
 

Mlatinoh king

JF-Expert Member
Oct 14, 2015
5,124
2,000
green city stand up........ila mbeya imekaa mda mrefu sasa bila kuleta mkali mwngne tena kwenye game aisee......kuna nini huko?
 

gwa myetu

JF-Expert Member
Aug 18, 2014
4,398
2,000
green city stand up........ila mbeya imekaa mda mrefu sasa bila kuleta mkali mwngne tena kwenye game aisee......kuna nini huko?
Mbeya iko juu sasa, Ray vanny anawakilisha tz BET, Sugu, Shaa, witnes kibonge mwepesi, Young D, Gigy money, Amberlulu, Neyhuddah , .a wengine watajeni
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom