Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,498
- 113,604
Mkuu Morgan, kwanza naunga mkono hoja kuwa Masele amefanya kazi nzuri na Wanashinyanga bado wanamuhitaji hivyo asikatishwe tamaa na wasaka tonge, hata mimi binafsi Masele namkubali sana na niliwahi kumfagilia hapa*MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU JIMBO LA SHINYANGA MJINI (PARIS YA TANZANIA)JIMBO LA MH. STEPHEN MASELE(MB)*
Jimbo la shinyanga mjini ni moja ya mji wenye maendeleo ya mwendokasi chini ya uongozi wa mbunge kijana wa jimbo hilo Mh Stephen Julius Masele ambaye Pia ni Naibu Spika wa Bunge la Afrika( PAP).
Hakika mwenye macho haambiwi tazama, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni,Masele tumeona na tumeridhishwa na utendaji kazi wako.Hii ni kasi ya 5G ya maendeleo kutoka kwa mbunge kijana, msomi na mpenda maendeleo. Aluta kontinua Komredi Stephen Masele mbunge wa shinyanga mjini. Bado tunakuhitaji usikatishwe tamaa na wasaka tonge.
Sent using Jamii Forums mobile app
Steven Masele atamkwe Shujaa wa Taifa! Ni kweli Balozi wa Uingereza ni Jasusi. To Hell with...!
Wanabodi, Ile siku Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhre. Stephen Masele, alipomtuhumu Balozi wa Uingereza nchini kwa tuhuma nzito za ujasusi!, nilipandisha uzi huu, Ujasusi wa Balozi wa Uingereza: Tanzania, Can We Stand?!.nikihofia Mhe. Masele kufanywa "kondoo wa kafara!". Baada ya tuhuma...
www.jamiiforums.com
Lakini kwa vile hakuna hatimiliki ya jimbo lolote, wala hakuna mtu kuhodhi jimbo lolote, jambo la kwanza namshauri Masele, atengeneze 30 min video Documentary ya hayo mambo 10 uliyo eleza yawe kwenye Audio Visual, watu waone na wasikie. Kisha video hiyo irushwe kwenye TBC, ITV, Star TV, Channel Ten, na Azam TV kisha DVD zisambazwe zikiandamana na flash ya HD zigawiwe bure baa zote, hotels zote, saloons zote, sehemu zote za public na za starehe ili watu waone kilichofanyika.
Lengo la kufanya haya ni kitendo cha Masele kuonekana mwiba kwa bosi wake pale mjengoni Dodoma, na bosi wake na Mzee Baba ni dam dam hivyo it's possible no matter how good Masele is, hatapitishwa na chama chake, hivyo asipopitishwa, avuke upande wa pili, wananchi wake wamchague aendelee nao.
P