Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe walilolikataa Waashi litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni

Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe walilolikataa Waashi litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni

Nimetokea tu kumpenda Makonda na kupenda kusoma habari zake hata kumsikiliza akirushwa mitandaoni.

Keep it up
 
Paskali si kila mafanikio ni baraka za Mungu, God is a watcher akiwabariki awapendao kwa namna yake na si kwa vitu vya kidunia kama vya makonda...kumbuka njia za Mungu si za mwanadamu
 
Wanabodi,
Ukiisikia simulizi ya Makonda, alipotoka, alipo na anapokwenda, mtakubaliana na mimi kuwa hii ni kazi ya Mungu katika kuonyesha uwezo wake kwa wanadamu kwa kuufanya muujiza wa Jiwe Walilolikataa Waashi, Litafanywa Kuwa Jiwe Kuu la Pembeni.
Kwa kuanzia, wasikilize wazazi wake.

Sasa msikilizeni Makonda mwenyewe.

Historia Yake Kuzaliwa na Familia
Makonda alizaliwa Februari 15, 1982 majira ya saa 1:30 asubuhi, familia ya mzee Makonda (Baba hatajwi majina) na mkewe, Suzan, walimkaribisha mtoto wao pekee wa kiume katika Zahanati ya Kolomije, wilayani Misungwi mkoani Mwanza.

Elimu ya Msingi, Sekondari na Chuo.
Makonda ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi. Kabla ya kwenda Moshi, alipita katika Shule ya Msingi Kolomije na amesoma pia katika Chuo cha Uvuvi, Mbegani, Bagamoyo ambako alisoma hadi ngazi ya Diploma katika masuala ya uvuvi.Hakuna maelezo alisoma wapi Sekondari wala hakuna index number yoyote ya Necta yenye majina yake.

Kabla ya Chuo.
Makonda alianzia kazi ya kuchimba mchanga.
Akaja kazi ya kuchoma mkaa.
Akawa utingo kwenye mabasi stendi
Kisha akawa kondakta yaani Makonda akawa konda.

Ukiwa ni mpakwa mafuta kama Daudi, Mungu atakuinua kutoka chini ulipo na kukupandisha mahali pa juu palipo inuka.
Mibaraka.
Mibaraka kwa Makonda ilianzia siku yake ya kuzaliwa February 15, mwaka 2015 Rais Jakaya Kikwete alipomteua Makonda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na kutangazwa Februari 18, mwaka 2015. Kuteuliwa siku yako ya kuzaliwa sio coincidence bali ni mipango ya Mungu.

Kufuatia utendaji uliotukuka, sisi wenye jicho la tatu Machi 12, 2016 tukamtabiria makubwa kwa kuandika humu jf Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam. Na kweli ikatokea Machi 13, 2016 akateuliwa RC DSM.

Mibaraka Zaidi.
Hii ni kazi ya mikono yake kwa baraka za Bwana. (Not necessarily ni kweli)
Inasemekana Mungu amemuwezesha
Makonda kununua jengo (apartment), pale Viva Towers kwa Sh600 milioni. Makonda amempa mke wake gari aina ya Mercedes Benz lenye thamani ya Dola 250,000 za Marekani (Sh550 milioni) kama zawadi ya ‘Birthday’,”
Makonda ana gari aina ya Lexus, lenye thamani ya Sh400 milioni. Makonda anamiliki magari mengine ya kifahari aina ya V8, anajenga maghorofa jijini Mwanza na amekarabati ofisi yake kwa Sh400 milioni zake binafsi.

Japo there is something missing ambayo ni a missing link kwenye story ya Makonda ambayo wazazi hawajaisema, Makonda mwenyewe hajaisema, wala sijaisikia ikisemwa popote, kuhusu elimu ya Sekondari, the bottom line ni the end justify the means.

Mwacheni Mungu aitwe Mungu.

Paskali

Makonda amefanikiwa nini?
 
Pamoja na kukosolewa katika mengi kuhusiana na sharia, hakika uthubutu wake utaingia katika historia ya kulipigania Taifa katika kuliokoa na janga la madawa ya kulevya.
Kweli kabisa pia tunatumaini atapambana sana katiak swala elimu na pia waliotumia majina feki na kugushi vyeti vya elimu...Mungu amsaidie na amuongoze katika hili.
 
Ni wapumbavu tu ambao huona kuambiwa ukweli ni husda, matunda ya historia yangu hata ukiyafahamu hayatokusaidia kitu,kikubwa na cha kushukuru sina midanda kama ya nduguyo mimi jina langu lipo kamili wala halimfichi baba mzazi kama Pascal alivyoeleza na index namba imapatikana kila sehemu niliyopita kielimu, ukweli unauma ila Daudi anapaswa aipambanue education background yake kama alivyowachakata wenzie
Ukishajua ndo unafanyaje acha uganga, ww ukizeeka utakuwa mchawi siyo kwa roho hii ya korosho.. just concentrate of delivering
 
Huyu kijana ni jasiri hakika,Tanzania inajivunia "mapapa" wa mihadarati wametoweka na wengine wamejisalimisha huku wengine wakiogopa kupinga mkojo kwa mkemia mkuu.Mungu amlinde
Halafu wewe ni Mbunge na unasema umesoma lakini bado PASKALI Mayalla kakuingiza mkenge mpaka unadhani uzi huu ni wa kupongeza. Soma between the line utapata mantiki ya hoja iliyo mezani.
Kumbe wewe ni mbulula tuu, na sio kama unavyo jinadi kuwa msomi.
 
Pasco, stupidity at your best, rudi Marekani ukafanye vibarua naona njaa inataka kukua, kila kukicha ni kujipendekeza Kwa watawala, na unaandika ujinga mtupu.
Hivi ni Mungu gani anayeweza kumwinua Makonda ?labda mungu Shetani, unadhani kila aliye juu kainuliwa na Mungu?
Pasco wewe ni mtu mzima hovyo na kila leo unajidhihirisha ni kiasi gani hujitambui hata kidogo.
Hata Hitler, Saddam, Hissen Habre na Madikteta wengine na Viongozi wengine wana historia nzuri ya kupanda kimaisha Kama Makonda au zaidi pia.
Shetani ana watu wake na Mungu pia ana watu wake.
Mtu aliyeinuliwa na Mungu, very automatically 90% ya watu ktk taifa humkubali wala huwa hapambwi na waandishi uchwara Kama wewe kaka yangu pasco.
Nyie wasukuma sijui mna matatizo gani, kuna mwenzako Shigongo na yeye kila Siku ni kusifia ccm tu, Naamini Siku Chadema ikishika nchi atageuka kujipendekeza huko tena.
Pasco unakera Sana Kaka yangu unafanana Kama mtu primitive ambaye hajawahi ku explore dunia, Ukamdhalilisha Mungu eti kamwinua Makonda, Makonda huyu huyu aliyempiga Mzee warioba ili kufurahisha wakuu Wake ndipo wakamzawadia ukuu wa wilaya...
Pasco achana na Mungu kabisa, MUNGU hachangamani na dhambi, just imagine uzae Mtoto halafu umwite Makonda, sijui itakuwaje mitaani.
Kama maisha yamekushinda bongo, nakushauri urudi USA ulikokuwa, huko afadhali kuna fursa hata za vibarua vya kukuingizia hata $40 per day uta survive kuliko kupamba watu wasiokubalika na jamii inayowazunguka,you expose yourself into shame.
Pumba.vu kabisa..maneno meengi umeshindwa kumwelewa pasco...lofa kabisa weww
 
Back
Top Bottom