KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 18,896
- 36,213
Habari za wakati huu wapendwa wangu.....natumaini mfungo unaenda vyema kwa wale waliokwama kuendelea na mfungo basi mola atawafanyia wepesi.
Siku hizi limekuwa ni jambo la kawaida kuusikia msamiati wa MAFANIKIO.....kila uchao tunaona pirika pirika za watu wakihangaika huku na huko kuyatafuta mafanikio.
Wengine hata kudiriki kujaribu njia ama mbinu mbali mbali zikiwemo hata zile haramu kama kuutoa uhai wa mtu au hata tu kumjerehi mtu ilimradi huyo mtu awe na kitu kitachompa mafanikio.
Kama ambavyo tumetofautiana maoni na mitazamo yetu kuhusiana na mambo mbali mbali ndivyo tunavyotofautiana mitazamo kwenye namna tunavyoyatazama mafanikio.
Kuna wengine wana maoni na mitazamo mibaya kuhusu hayo mafanikio.
Lakini kosa kubwa linalofanywa na vijana au watu wa zama hizi ni kulinganisha mafanikio yao na ya wengine au kwa maana nyingine anashindana na wengine katika kuyatafuta hayo mafanikio watu wa aina hiyo kamwe hawatakuja kuyaona mafanikio yao na kuyafurahia kwani wao daima hujiona kuwa ndio kwanza wanaanza kwa kuwatazama wa juu yao.
Lengo na dhumuni la harakati za kimaisha sio kuwa tajiri mkubwa sana bali ni kukidhi mahitaji yale muhimu ambayo kila mtu anayafahamu.
Kwa mtu ambaye alikuwa anashindia mlo mmoja lakini kwa juhudi zake na sasa ameweza kumudu milo mitatu iliyo kamili hayo ni mafanikio.
Kwa mtu ambaye alikuwa akitembea kwa miguu kwenda kwenye shughuli zake na hatimaye akapata usafiri hayo nayo pia ni mafanikio.
Kwa mtu ambaye alikuwa anateseka na familia yake kwenye nyumba za kupanga na hatimaye amejenga ya kwake na anaishi kwa furaha na familia yake hayo nayo pia ni mafanikio.
Kwa mwanafunzi aliyefaulu level hii na kuingia level nyingine hayo ni mafanikio.
Yapo mambo mengi madogo madogo tunayoyafanikisha kila siku lakini tunashindwa kuyafurahia kwa kuwa siku zote vipimo vyetu vya kuyapima mafanikio ni vikubwa mno....hata hupelekea kuyadharau au kuyapuuzia mafanikio yetu.
Mafanikio yako ni kitendo cha wewe kuvuka kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine mbele huku ukipiga hesabu za kwenda mbele zaidi.
Kamwe huwezi kuziona neema za Mungu juu yako kwa kuwatazama wale wa juu yako bali kutapelekea wewe kupuuzia neema za Mungu juu yako.
Wakati wewe unalalamikia kujenga nyumba moja ambayo unaishi na familia yako vizuri watazame wale wanaolala nje kwa kukosa makazi.
Wakti wewe unalalamikia aina ya chakula unachokula watazame wale wanaoshinda na njaa.
Wakati wewe unalalamikia gari lako kuu kuu watazame wale wanaokoga vumbi kwa kutembea kwa miguu kufika makazini.
NB; lengo sio kuwa tajiri bali kukidhi mahitaji utajiri ni matokeo.