Maeneo yanayoongoza kwa bodaboda Tanzania

Kuna sehemu hapa nchini kuna bodaboda nyingi mno either kwasababu ya ubovu wa barabara hivyo magari hayawezi kufika baadhi ya maeneo au kwasababu ya uhaba wa usafiri wa umma.

Moja ya hayo maeneo ni Kibaha, Kwa Mathias. Wakazi wa maeneo hayo wanatumia zaidi bodaboda kwasababu hamna usafiri wa umma kutoka stand kuelekea maeneo ya mbali na hapo kama Msangani, Efatha nk

Maeneo gani mengine hapa nchini kuna bodaboda nyingi sana?
Ilo eneo angepatikana mtu mmoja tu au wawili wakuweka noah hapo 500 wangepiga sana hela
 
Bukoba Mjini
Bukoba mjini bodaboda kwanza wana bei nafuu sana. Nilishangaa nafika usiku saa sita natozwa 2,000 tu kutoka stendi mpaka Kivulini. Kitaa nako wale 'vilaza' waliokuwa wasumbufu darasani wote wanaendesha bodaboda na fursa kibao zipo hazina watu.
 
Bukoba kwanza walianzia zamani,walichukua utaratibu wa bodaboda kutoka Uganda kipindi ambacho ukubongo bado azijakuwa rasmi.ila nchi kama Uganda tayari zilikuwa ni usafiri rasmi.
Mwaka 2005 naanza kujitambua nilizikuta ila nilipoenda Mwanza sikuwa naziona. Kipindi wanaziita Sekido hata neno bodaboda sidhani kama lilikuwepo kipindi kile. Kulikuwa na hasa pikipiki za Senke. Mojawapo ya sehemu ambayo bodaboda wana very strong political influence nadhani pia walianza mapema kuwa na muungano.
 
Watu wanamiliki kuanzia 5 zaidi ya familia yake.

Tunapoelekea zingine zinaweza kuanza kujiendesha kabisa maana idadi ni kubwa kuliko watu.
Aaah mkuu acha kudanganya bana, boda boda zinaanzaje kuzidi idadi ya watu? Inamaanisha kuna nyingine zinajiendesha Zenyewe
 
Kuna sehemu hapa nchini kuna bodaboda nyingi mno either kwasababu ya ubovu wa barabara hivyo magari hayawezi kufika baadhi ya maeneo au kwasababu ya uhaba wa usafiri wa umma.

Moja ya hayo maeneo ni Kibaha, Kwa Mathias. Wakazi wa maeneo hayo wanatumia zaidi bodaboda kwasababu hamna usafiri wa umma kutoka stand kuelekea maeneo ya mbali na hapo kama Msangani, Efatha nk

Maeneo gani mengine hapa nchini kuna bodaboda nyingi sana?
Ruvuma
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom