Mambo ya kuzingatia unapotumia usafiri wa bodaboda

Kasi kazini

Member
Sep 7, 2023
5
11
Siku hizi usafiri wa bodaboda ni usafiri maarufu sana hapa nchini na watu wengi wanautumia usafiri wa bodaboda kwenda kwenye majukumu yao mbalimbali.

Wewe kama ni (mtumiaji) wa usafiri wa bodaboda. Naomba nikupe mambo machache ya kuzingatia unapotumia usafiri wa bodaboda.

Haya mambo nayaandika kutokana na uzoefu wangu katika kuendesha bodaboda.

1. Hakikisha bodaboda unayopanda ni salama ina taa, ina side mirror, na ina taa za kuonyesha ishara ya kwenda kulia au kushoto (endiketa)

Wakati mwingine ajali za bodaboda zinasababishwa na kukosekana kwa hivyo vitu kwenye bodaboda
Unastuka tu bodaboda kaenda kulia au kushoto bila kuonyesha ishara yeyote, au anakatisha barabara bila kujua nyuma kuna nini kwa sababu ana side mirror anasababisha ajali.

2. Usalama wa dereva
Kwa muonekano tu unaweza kumtambua huyu dereva ni salama kiasi gani. Je? Anajijali, ana elimenti, amevaa viatu vya kufunika mguu, mana kuna wengine wanavaa ndala au yebo yebo je? ni msafi

Maana kama dereva ajijali atakujalije wewe abiria wake. Mtazame dereva vizuri usoni ukihisi ni mlevi au amelewa usipande hiyo bodaboda.

3. Kama unapanda bodaboda usiku labda umesafi upo sehemu ngeni pandia bodaboda kwenye kituo rasimi sehemu yenye bodaboda wengine.

Mana kama itatokea changamoto yeyote huyo bodaboda ni rahisi kumpata mana bodaboda wanasajiliwa kwenye vituo.

Mwisho kabisa vitu nilivyoviandika namba 1 na namba 2 unaweza kuvitambua ndani ya sekunde 20 tu

@kasikazini one love
 
Usalama wako ni kitu cha muhimu mkuu.
Kuna kitu muhimu Acha nkuongeze

Unapotaka usafiri wa bodaboda,usisimamishe zile za njiani
Yaani za juu kwa juu
Unless labda,una juwa kumsoma mtu
Kama ni kweli boda au mhalifu

Ova
 
Siku hizi usafiri wa bodaboda ni usafiri maarufu sana hapa nchini na watu wengi wanautumia usafiri wa bodaboda kwenda kwenye majukumu yao mbalimbali.

Wewe kama ni (mtumiaji) wa usafiri wa bodaboda. Naomba nikupe mambo machache ya kuzingatia unapotumia usafiri wa bodaboda.

Haya mambo nayaandika kutokana na uzoefu wangu katika kuendesha bodaboda.

1. Hakikisha bodaboda unayopanda ni salama ina taa, ina side mirror, na ina taa za kuonyesha ishara ya kwenda kulia au kushoto (endiketa)

Wakati mwingine ajali za bodaboda zinasababishwa na kukosekana kwa hivyo vitu kwenye bodaboda
Unastuka tu bodaboda kaenda kulia au kushoto bila kuonyesha ishara yeyote, au anakatisha barabara bila kujua nyuma kuna nini kwa sababu ana side mirror anasababisha ajali.

2. Usalama wa dereva
Kwa muonekano tu unaweza kumtambua huyu dereva ni salama kiasi gani. Je? Anajijali, ana elimenti, amevaa viatu vya kufunika mguu, mana kuna wengine wanavaa ndala au yebo yebo je? ni msafi

Maana kama dereva ajijali atakujalije wewe abiria wake. Mtazame dereva vizuri usoni ukihisi ni mlevi au amelewa usipande hiyo bodaboda.

3. Kama unapanda bodaboda usiku labda umesafi upo sehemu ngeni pandia bodaboda kwenye kituo rasimi sehemu yenye bodaboda wengine.

Mana kama itatokea changamoto yeyote huyo bodaboda ni rahisi kumpata mana bodaboda wanasajiliwa kwenye vituo.

Mwisho kabisa vitu nilivyoviandika namba 1 na namba 2 unaweza kuvitambua ndani ya sekunde 20 tu

@kasikazini one love
Ongeza hii ya tatu
3.Ukipanda bodaboda hakikisha haendi mwendo wa kasi sana uwe mwendo wa kawaida tu.Hata kama una haraka zako utakuwa ulijichelesha mwenyewe.Kama ni sehemu za mashimo mdanganye boda una operation ya miguu una vyuma ndani vitachomoka kama nauli ni 2000 muambie utamuongezea buku hau hata ulimpe 200 atakuendesha kama yai lisije vunjika.
 
Boda mwenye turasta flani sipandi.
Mwenye kiduku sipandi.
Mwenye vikaptula sipandi.
Mwenye jinzi imechanikachanika sipandi.
Napanda boda ya mtu mzima kidogo mwenye uso wa utulivu.

Kuna boda ukimuona tu unaanza kuona vidonda mwilini mwako na mivunjiko mbalimbali hata kabla hujapanda.
 
Msaidie boda kuangalia nyuma.kama Kuna gari liko rafu mhimize asogee pembeni kulipisha muendelee na safari.la sivyo mtasombwa
Hawa vilaza wengi huwa wanategesha side mirrors kuona USO wa mteja hata wadada sio nyuma

Jitahidi utembee na silaha usiku sana hasa mwanamke,boda wa midnight asilimia kubwa ni wahalifu.rafiki yangu amekoswa kubakwa mara mbili na boda sababu ilikua usiku sana na maeneo ni ya ndanidani hakujajengwa sana.alipambana nae Hadi Kwa mawe.
 
Back
Top Bottom