Maeneo gani Dar mazuri kwa kuishi?

Hello guys!!

Niaje, nivipi ndugu zanguni. Hivi jamani ni maeneo gani mazuri kwa kupanga nyumba nzuri lakini affordable na kuishi jijini Dar. Napata shida kidogo kuchagua.

Mbezi, Kimara, Ubungo, Kinondon, Kigambon, Gomes, Chanika, Pugu, Kivule, Sinza,..n.k

Ni sehemu gani nzuri?

Nb: Distance does't matter!
Kigamboni kupo poa kero ni moja tu hiyo kuingia na kutoka lazima ulipie pantoni darajani.
 
Una mke? Au mke na mtoto/watoto? Na mwaka wa4 toka nianze kupanga sijawai toka nje na mbezi Beach asee huku ni raha sana. Maji 24hrs, umeme sio wa shida, hakuna vibaka watu wanajiheshimu sana inshort hakuna uswahili. Bei za vyumba ni affordabe kabisa.
Mimi naona akiishi maeneo kama hayo hawezi kuwa mjanja. Ni vema kama akikaa sehemu zenye changamoto za vibaka, maji, umeme na barabara zisizopitika msimu wa Mvua.
 
Kwanza una budget kiasi gani, maana hizi ni aina ya maswali huwa nauliza nikiwa sina pesa...

Maana katika jinsi ya kawaida huwezi niambia hujui kama Masaki, O'bay, Mbezi Beach, Ununio, Mikocheni etc ndio sehemu nzuri kwa Dar...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom