BATTLE: Sinza kwa wajanja & Kinondoni kwa watukutu

Akilihuru

JF-Expert Member
May 20, 2022
1,444
2,833
Kwema ndugu, natumai kila mtu ni mzima wa afya.

Sinza na Kinondoni ni kata mbili tofauti zilizopo katika mkoa wetu mzuri wa Dar es salaam.

SINZA ambayo inatambulika kuwa kwa wajanja, ipo katika wilaya ya Ubungo na ni miongoni mwa maeneo yenye starehe nyingi na kubwa hapa Dar es salaam. Sinza inaongoza kuwa na baa nyingi kiasi kwamba inakisiwa kuwa kila katika nyumba tatu basi moja ni baa. Lakini vile vile Sinza inaongoza kuwa na madada poa wengi wanaojiuza hovyo barabarani.

Pia Sinza ipo vizuri kibiashara maana kuna watu hutoka maeneo mbali mbali ya mkoa wa Dar es salaam huja Sinza kutembea na wengine kula bata. Ndo maana kuna sehem panaitwa Sinza madukani. Yani maduka kibao na bado watu wanauza deile.

Kuhusu watu na maendeleo Sinza ina mchanganyiko wa watu wa vipato tofauti. Kuna wa vipato vya juu, kati na vya chini. Na imeendelea kimtindo, kuna viji sahanati vya mitaani, barabara za mitaani japo baadhi kwa sasa zimeshakuwi hazifai, na huduma zingine za kijamii. Sinza mijengo mingi mizuri ila ni ya kizamani.
Nyumba za ibada misikiti na makanisa pia zipo.


KINONDONI ambayo inatambulika kuwa kwa watukutu, kama jina lake linavyojieleza yenyewe ipo katika wilaya ya Kinondoni, pia ni miongoni mwa maeneo yenye starehe nyingi na kubwa pia hapa Dar es salaam. Kinondoni pia ina baa nyingi, na inaongoza kwa kuwa na kumbi mbali mbali za starehe kiasi kwamba kuna baadhi ya maeneo watu huwa hawalali kutokana na sauti kubwa za miziki kutoka katika kumbi hizo. Vilevile Kinondoni kuna madada poa wakumwaga tu kiasi kwamba kila mtu ana urahisi wa kusafisha 'bunduki' kwa buku tu.

Kibiashara nayo Kinondoni haipo nyuma, maduka ya kumwaga kiasi ya kwamba mtu hauwezi jua uingie duka gani.

Kuhusu watu na maendeleo Kinondoni pia ina mchanganyiko wa watu wa vipato tofauti. Kuna wa vipato vya juu, vya kati na vya chini. Pia kuhusu maendeleo imeendelea kimtindo, kuna zahanati nyingi, barabara za mitaani na huduma nyingine za kijamii. Pia Kinondoni ina majumba mazuri mazuri na zilizochoka ni chache sana. Nyumba za ibada misikiti na makanisa zipo kadhaa.

Sasa ndugu mwanaJF ukiambiwa uchague wapi pa kwenda kuishi utachagua wapi?
 
Kinondoni ww hapa zamaradi pale TID halafu jonas mkude kwa mbali watoto wa mjini wote wapo kinondoni sinza huko ni sehemu ya kupoza moyo kwa kiburudisho cha bei nafuu.
 
Kinondoni ww hapa zamaradi pale TID halafu jonas mkude kwa mbali watoto wa mjini wote wapo kinondoni sinza huko ni sehemu ya kupoza moyo kwa kiburudisho cha bei nafuu.
Aisee we noma mkuu 😂😂😂😂
 
Sehemu hizo zote ukitembea mchana ni vituko kila mahala pananuka harufi za mikojo na mavi.
MTU yoyoye anayejielewa na kipato chake hawezi kuishi Sinza au Ubungo,mazingira ni ya hovyo sana.
Inatakiwa serikali itunge sheria kali kuhusu watu wanaoharibu mazingira kwa kukojoa kojoa hovyo barabarani.

Kwamba anaekamatwa adhabu yake ianzie laki 3 na kuendelea.
 
Wa Kinondoni wakija watapinga ulichoandika 😂😂😂
Uhuni Mwingi Kuliko Sinza e.g nenda Moscow...mkwajuni

Mabrotherman e.g Kinondoni yote
Tena Kuna Wale ving'asti kabisa

Ujanja e.g watot wa kino yote wanaamin mno hlo suala wao watt wa town lakn ujanja wao Kwenye kupendez na kutapeli tu halaf mwsho Kurud kula ugal kwa mama Mandingo😂
 
Kinondoni uwezi kufananisha na sinza,.. ,kinondoni sehemu nyingi Ni za hovyo hovyo Kama kinondoni shamba, moscoko, nyuma ya mahakama,zipo nyingi tu vijumba vimepangana pangana tu, sinza huwezi kukuta huu uchafu

Kinondoni wanya mnazi gongo na pombe za ajabu ajabu, kila kona vilabu vya pombe chafu, niambie wapi sinza wanauza mnazi au wanzuki

Vijana wa kinondoni wengi Ni shamba boi masaki na osterbay, sinza hakuna washamba boi,

Ukienda kinondoni shamba mpaka vijumba vya udongo vipo, sinza hakuna vyumba za udongo,,

Vijana kinondoni Wana utapeli wa jinga jinga Sana na vivuta unga

Wizi Kama viatu, ndala, kukata nyavu za madirisha, kuchungulia aka deo, kupigana ngeta kinondoni sehemu yake, sinza unaacha nguo kwenye kamba kesho unazikuta
 
Kinondoni uwezi kufananisha na sinza,.. ,kinondoni sehemu nyingi Ni za hovyo hovyo Kama kinondoni shamba, moscoko, nyuma ya mahakama,zipo nyingi tu vijumba vimepangana pangana tu, sinza huwezi kukuta huu uchafu....
Uchambuzi wako ni mzuri mkuu na ni rahisi kueleweka.
 
Back
Top Bottom