Maeneo 15 ya kihistoria yenye kuvutia zaidi Kinshasa

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
MAENEO 15 YA KIHISTORIA YENYE KUVUTIA JIJINI KINSHASA.

Na. Comred Mbwana Allyamtu (CMCA)
Saturday-10/07/2021.
Marangu, Kilimanjaro, Tanzania

Yafuatayo ni maeneo 15 ambayo ni alama ya jiji la Kinshasa, Maeneo hayo hushuhudiwa wageni wengi pamoja na kuwa kivutio cha jiji hilo la Kinshasa.

Jiji la Kinshasa ndio mji mkuu wa nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ndio jiji lenye watu wengi Afrika, pia ni jiji la tatu kwa ukubwa wa miji Afrika.

Kinshasa pia ni eneo kubwa zaidi ulimwenguni linalozungumza Kifaransa, kuliko Paris ya ufaransa yenyewe.

Jiji la Kinshasa ni jiji la 6 kwa maendeleo Afrika, hapa namanisha kuwa ndio jiji linaloendelea kwa kasi likishika ya 6 Afrika.

Ukiwa Kinshasa maeneo yafuatayo ni kivutio kikubwa cha jiji hilo;

Eneo la kwanza ni...

1. Palais du Peuple, Kinshasa (Bunge la Umma)
Jengo la Palais du Peuple, (kwa Kifaransa) ni jengo la bunge la Kongo, hapo ndipo ulipo ukumbi wa Bunge na Seneti ya Kongo, jengo hilo lipo jijini Kinshasa, Muundo wa jengo hilo ulibuniwa kufanana na jengo la bunge China linaloitwa jengo Kuu la Umma la China, Bunge hili la Kongo lilisanifiwa na Zhang Bo.

Jengo hili ni maarufu sana nchini Kongo na limeshuhudia hafla muhimu katika historia ya Kongo na jijij la Kinshasa kama vile kuagwa kwa miili ya mwanamuziki maarufu wa rumba wa Afrika Tabu Ley Rochereau na Rais wa zamani wa Kongo Mzee Laurent Kabila ambae mwili wake ulilazwa kwenye bunge hilo kama heshima.

Eneo la pili ni........

2. Académie des Beaux (Chuo cha Sanaa)
Jengo la chuo cha sanaa cha Académie des Beaux-Sana, ambacho zamani kilifahamika kama École Saint-Luc à Gombe Matadi ni chuo cha sanaa kikongwe nchini Kongo, chuo hicho kilianzishwa na mmishonari Mkatoliki wa Ubelgiji aliyeitwa Marc Wallend, mwaka1943.

Chuo hiki kimejumuishwa katika mfumo wa kitaifa wa vyuo vikuu vya ufundi vya Kongo na kinatoa elemu katika vitivo vya nyimbo, mapambo ya ndani, mawasiliano katika ubunifu, uchoraji na uchongaji wa sanamu, na uchoraji, Wageni wengi zaidi utembelea chuo hicho kijifunza na kutalii mambo kadhaa na kushuhudia namna maprofesa na wanafunzi wanaofanya kazi lakini pia wageni ununua kazi za sanaa hapo chuoni.

Eneo la tatu ni........

3. Stade Des Martyrs, Kinshasa (Uwanja wa taifa)
Uwanja huu wa taifa wa Kongo ni uwanja wa tatu wa mpira kwa ukubwa barani Afrika, uwanja huu wa Stade Des Martyrs una uwezo wa kubeba watu 80,000, Uwanja huo unatumika katikamechi za mpira wa miguu na uliboreshwa mwaka 2008 ili kufikia viwango vya kimataifa.

Uwanja huo uliitwa jina la Stade des Martyrs de la Pentecote, ili kurejelea kumbukumbu ya waasi waliotundikwa kwenye uwanja huo kipindi cha utawala wa Mobutu kwa makosa ya kukaidi amri za Serikali ya Mobutu mwaka 1976.

Eneo la nne ni........

4. Cathédrale Notre-Dame Du Congo (Kanisa Kuu la Notre-Dame Du Congo)
Kanisa la Cathédrale Notre-Dame Du Congo, inafahamika hivyo kwa Kifaransa, kwa kiswahili ni *Kanisa kuu la Mama yetu wa Kongo" kanisa hili ni la dhehebu ya Katoliki, kanisa hili lilijengwa wakati Kongo ilikuwa bado chini ya utawala wa kikoloni wa Ubelgiji mnamo mwaka 1947, Kanisa hilo hufuata ibada ya Kirumi au Kilatini na kanisa hilo ndio makao makuu ya Jimbo kuu la Kinshasa.

Eneo la tano.......

5. Tour de l’échangeur (Mnara wa Limete)
Mnala huu Tour de l’échangeur upo katika ya jiji la Kinshasa, mara nyingi mnara huu pia huitwa Mnara wa Eiffel wa Kongo, ujenzi wa mnara huo ulianza chini ya utawala wa Mobutu mwaka 1970 na ulikamilishwa na Joseph Kabila mwaka 2011, utaona ujenzi wake kuwa ulichukuwa mda refu kutoka na kipindi cha Mobutu ujenzi ulisitiswa na kipindi cha utawala wa rais Joseph Kabila alianza tena ujenzi wake na kuukamilisha mwaka 2011.

Mnara huo umeundwa na nguzo nne ambazo zina urefu wa mita 210 kwenda Juu, mnara umewekwa nyuma ya sanamu la Patrice Lumumba na kushoto kuna jumba la makumbusho ya kumbukumbu ya Lumumba ambalo hufunguliwa kila siku asubuhi.

Eneo la sita..............

6. Palais de la Nation (Ikulu ya Taifa)

Ikulu ya Palais de la Nation iko pembezoni mwa Mto Kongo, ndio ilikuwa makazi rasmi ya gavana mkuu wa Ubelgiji, kipindi cha ukoloni, ilisanifiwa na Mbergiji Marcel Lambrichs mnamo mwaka 1956.

Baada ya uhuru wa Kongo mwaka 1960, jengo hilo lilitumika kama bunge la Kongo mpaka ilipo hamishiwa Palais du Peuple 1998, mwaka 2001 Joseph Kabila alihamishia makazi ya Raisi wa Kongo kwenye jengo hilo, toka hapo mpaka sasa jengo la Palais de la Nation linafanya kazi kama makazi rasmi ya Rais wa Kongo.

Eneo la saba.........

7. Musée National de la République Démocratique du Congo(Makumbusho ya Kitaifa ya Kongo)

Jengo hili ndio makumbusho ya historia ya kitamaduni ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambayo ilifunguliwa kwa umma mwaka 2019.

Jengo hilo limejengwa kwa ushirikiano kati ya nchi ya DR Congo na Jamhuri ya Korea (Korea ya kusini) na ndio eneo ambalo Korea kusini imewekeza kiasi kikubwa zaidi Katika masuala ya utamaduni katika nchi za Afrika ya Kati.

Eneo la nane.............

8. De La Gare Centrale/Boulevard du 30 Juin (Bustani ya De La Gare Centrale)

Mahali hapa panaitwa De La Gare Centrale ni uwanja uliopo katikati mwa jiji la Kinshasa, eneo hilo limezungukwa na ofisi mbali mbali za serikali, ni mahali pazuri pa kulizama jiji la Kinshasa, eneo hilo ni eneo la wazi tangu uhuru, eneo hilo la Boulevard du 30 Juin ndio njia kuu ya barabara inayoumganisha maeneo yote ya jiji, eneo hilo linaunganisha eneo la kusini la Gombe (wilaya ya kisiasa na biashara ya Kinshasa) magharibi.

Eneo la Tisa ni........

9. Palais De Marbre, Kinshasa (Ikulu ya Marumaru)

Jengo la mwanzo la ikulu hii liitwalo central wing lilijengwa na Mberigiji kama makazi ya ugeni mkubwa hususani mfalme wa Uberigiji, baada ya uhuru jengo hilo likasanifiwa upya, ujenzi huo wa kuliboresha jengo hilo na kuongeza majengo mengine na kuongeza gorofa ya pili wa Ikulu hii ilijengwa na mbunifu majengo aliyeitwa Fernand Tala-Ngai mwaka 1970, mwanzoni ilikusudiwa kuwa makazi ya Mkurugenzi wa Benki kuu ya taifa Kongo, baadaye Mobutu akaifanya kuwa ofisi ya chama chake cha MPL, alipo ingia Mzee Kabila akaifanya kama makazi ya Raisi, na aliishi kwenye ikulu hiyo kipindi chote toka mwaka 1997 mpaka mwaka 2001, kwenye Ikulu hiyo ndipo mzee Laurent- Désiré Kabila alipo uwawa mwezi Januari 16, 2001.

Toka kifo cha Mzee Kabila jengo hilo lilifungwa, limekuja kufunguliwa mwaka 2009 na kutumika kama makumbusho ya taifa, kila tarehe 16,17 kila mwaka ufunguliwa kwa umma kuruhusu watu kutembelea, tarehe hizo ni siku za mapumziko za Kongo kukumbuka siku ya kifo cha Kabila.

Lakini pia Ikulu hii ya Palais De Marbre bado inaendelea kutumika kama moja ya ofisi na makazi ya Raisi japo toka kifo cha Mzee Kabila aijawai kutumika kabisa kama Ikulu.

Eneo la Kumi ni...............

10. Chuo Kikuu cha Kinshasa
Chuo Kikuu hichi cha Kinshasa ni moja ya vyuo vikuu vikuu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, chuo hiki kilianzishwa na wakoloni wa Ubelgiji na kiliitwa Chuo Kikuu cha Lovanium.

Chuo kikuu hiki kipo karibu kilomita 25 (16 mi) kusini mwa jiji la Kinshasa, ndio chuo kikuu kikubwa na maarufu nchini Kongo, kwa Tanzania tunaweza kukifananisha na Udsm.

Eneo la Kumi na mmoja ni.............

11. Kaburi la Laurent Kabila, Kinshasa
Mzee Laurent Kabila alikuwa Rais wa tatu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambaye aliuawa mwaka 2001, Kaburi lake linajengwa ndani ya jiji la Kinshasa na moja ya makumbusho kubwa jijini Kinshasa.

Kaburi hilo limejengwa kwa muundo wa paa la kaburi hilo kushikiliwa na mikono minne ambayo iko kwenye minyororo, mbele ya kaburi hilo limejengwa sanamu kubwa Laulent Kabila ambalo lilijengwa kwa msaada na taifa la Korea Kaskazini.

Eneo la Kumi na mbili...........

12. Symphonie des Arts (bustani ya Sanaa)
Eneo hili la Symphonie des Arts au Symphony of the Arts ni bustani ya kitropiki iliyopo jijini Kinshasa, bastani hiyo ndipo nyumbani kwa tausi wa Kongo, maua, maporomoko ya maji madogo, na kazi kadhaa za sanaa ambazo hupafanya kuwa mahali pazuri kutembea.

Kwa zaidi ya miaka 40, bustani hiyo imekuwa bustani ya sanaa mashuhuri nchini Kongo.

Eneo la Kumi tatu...............

13. Marché Central (Soko kuu la Kinshasa)

Marché Central ndio soko kuu la Kinshasa ni soko linaloongoza kwa kuuza vitu vya asili na madawa ya asili, pia ndio eneo lilopatikana vyakula vyote vya tamaduni zote za Kongo, soko hilo ni soko la tatu kwa ukubwa Afrika ya Kati.

14. Cimetiere de la Gombe, Kinshasa (Makaburi ya Gombe)

Makaburi haya ni moja ya makaburi ya zamani sana nchini Kongo, eneo hili la makaburi liliyengwa mwaka 1879 na Ubergiji, eneo hilo kipindi cha ukoloni walizikwa wazungu tu.

Baada ya uhuru makaburi haya yamekuwa eneo la kuwazika watu maarufu na viongozi wakubwa wa Kongo.
Ndani ya Makaburi haya kuna mila za mazishi ya tamaduni zote na pia ndio eneo la kuchoma.

Eneo la Kumi na tano.................

15. Palais de la Stanley (Ikulu ya Stanley)

Ikulu ya Palais de la Stanley" japo kwa Sasa hufahamika kama "Palace of Téké" jina hili la pili iliitwa na Mobutu Seseseko Kuku Ngwendu Wazabanga mwaka 1971, Ikulu hii ya "Palais de la Stanley" au "Palais de la Téké" ipo kaskazini mashariki mwa jiji la Kinshasa, katika kitongoji cha Gombe, ndani ya viunga vya Ngaliema barabara iendayo jijini Matadi kilometa 60 kabla ya mpaka wa jimbo la Kongo Central (zamani Bakongo) na jimbo la Kinshasa.

Ikulu hii ipo kwenye eneo lenye muinuko wa mita 2017 kutoka usawa wa bahari, eneo lote la ikulu hiyo lipo kwenye mlima hufamikao kama mlima Ngaliema, ambao pia kipindi cha ukoloni wa Mberigiji mlima huo uliitwa Mlima Stanley.

Ujenzi wa Ikulu hii ilianza kujengwa mwaka 1901 na kukamilika mwaka 1905, jengo lake lilibuniwa na muhandisi wa majengo wa Kiberigiji aliyeitwa Marcel Lambrichs, wakati wa ujenzi wake lilijengwa kwa ajili ya makazi ya gavana wa Uberigiji nchini Kongo, lakini baadae kabla ya kukamilika kwake likabadilishwa matumizi na kuwa makazi rasmi ya gavana wa mkoa wa Leopoldville (Kinshasa ya Sasa), kisha ujenzi wa makazi ya gavana yakajengwa eneo jingine linalofahamika kama "palace de la Prima" (ambapo kwasasa ni makazi rasmi ya Waziri mkuu wa Kongo).

Ikulu ya "Palais de la Stanley" ilitumika kama makazi ya Governor wa Kinshasa (leopaldville) mpaka tarehe Juni 30, 1960, baada ya sherehe za Uhuru ambapo majengo hayo yakawa makazi rasmi ya Ikulu ya Kongo, ambapo raisi wa kwanza kuishi Ikulu hiyo alikuwa ni raisi wa kwanza wa Kongo Joséph Kasavubu, Kasavubu aliitumia "Palais de la Stanley" kama eneo la makazi ya Raisi japo ofisi zake zilikuwa Palais de la Nation.

Hivyo Ikulu ya Palais de la Stanley ikaendelea kuwa makazi ya Rais wa Jamhuri, Ikulu hiyo inaukubwa wa km za mraba 17km², Ipo kwenye eneo la Mlima Stanley, Eneo hilo pia kuna wanyama kadhaa ambao walihamishiwa humo mwaka 1969 na Mobutu, baada ya mapinduzi yaliyo fanywa na Mobutu mwaka 1964 aliifanya Ikulu hiyo ya Palais de la Stanley kuwa Ikulu rasmi ya Kongo, kusini mwa Ikulu hiyo Mobutu alijenga kambi ya makomando iliyopewa Jina la Ngaliema camp au Camp 8179.

Haya ndio maeneo 15 ya kihistoria jijini Kinshasa yenyewe mvuto, makala ntakayo fuata tutaangazia maeneo 15 yenyewe mvuto jijini Dar es Salaam


Copyright 2021, All Rights Reserved.

Maktaba Kuu.View attachment 1848667View attachment 1848668View attachment 1848669View attachment 1848670View attachment 1848671View attachment 1848672View attachment 1848674View attachment 1848673
FB_IMG_1625930851226.jpg
FB_IMG_1625930854261.jpg
FB_IMG_1625930869000.jpg
FB_IMG_1625930872083.jpg
FB_IMG_1625930877905.jpg
FB_IMG_1625930880334.jpg
FB_IMG_1625930882761.jpg
FB_IMG_1625930885819.jpg
FB_IMG_1625930888899.jpg
FB_IMG_1625930891376.jpg
FB_IMG_1625930894354.jpg
FB_IMG_1625930897062.jpg
FB_IMG_1625930899785.jpg
FB_IMG_1625930902556.jpg
FB_IMG_1625930905250.jpg
FB_IMG_1625930908154.jpg
FB_IMG_1625931332554.jpg
FB_IMG_1625931335692.jpg
 
Back
Top Bottom