Maendeleo ya Utalii Zanzibar: Uchafu watajwa kuwa kikwazo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
Waziri wa Utalii na Mambo ya kale Mh Lela Mohamed Mussa amewataka wakuu wa Wilaya kuanzisha siku maalum kwa ajili ya kusafisha vivutio vya utalii.

Hayo ameyasema katika uzinduzi wa kampeni ya usafi kwa maendeleo ya utalii katika kisiwa cha Kwale Mkoa Mjini Magharibi siku hiyo maalum ya siku ya usafi itakuwa inafanyika kila baada ya mwezi mmoja ikiwa ni muendelezo wa usafi huo ili kupambana na taka na uharibifu wa mazingira unaopelekea vivutio hivyo kukosa haiba kwa wageni wanoingia nchini.

Vilevile amezitaja changamoto zinazoikabili sekta hiyo ikiwemo uchafu katika vivutio vya utalii ikiwemo Mji Mkongwe, fukwe, Visiwa na maeneo ya biashara ambazo watalii huhudumiwa.

Amesema uchafu katika maeneo ya utalii hupelekea kupoteza haiba ya mji wa kitalii wa Zanzibar na kuhatarisha usalama wa afya kwa wageni hasa katika usalama wa vyakula majiani.

“Uchafu katika maeneo unaweza kuhatarisha usalama wa afya kwa wageni hasa wale wanaopata huduma ya vyakula njiani inabidi usafi uzingatiwe na kuwekwa mazingira safi kwa wauzao vyakula hivyo”, alisema Waziri huyo.

Aidha alisema hali inayosababishwa na utupaji ovyo wa taka unaochochewa na uduni na utaratibu wa utekelezaji sera na sheria za usafi wa mji katika maeneo ya kitalii.

Pia Waziri huyo amewataka halmashauri ya Magharibi B kusimamia na kuhakikisha visiwa vinakuwa safi na waendane na tozo wanazowatoza wafanya biashara ya utalii.

Aidha amesema Zanzibar ni moja ya visiwa vichache vilivyofaidika kupitia biashara ya utalii ambao ni sekta mama inayochangia uchumi wa nchi kwa asilimia 30.
 
Eti kutoka dar to zanzibar ni kilomita ngapi?
IMG_20210208_140624.jpg
 
Back
Top Bottom