SoC02 Maendeleo ya leo

Stories of Change - 2022 Competition

Shengesha

Member
Aug 31, 2022
5
0
Jamii ya sasa imekuja na nadharia ya maendeleo ya Leo ambayo kwa kiasi Fulani imeshika hatamu katika kuifanya jamii iache kufata utamaduni wao .

Nadharia hiii ndiyo iliowavisha dada zetu vimini na suruali mbano hadharani wakiamini ndio maendeleo ya Leo.

Nadharia hiii ndio iliwafanya vijana wetu badala ya kutafuta pesa kwa kujengea na kufanya miradi ya maendeleo anatafuta pesa kwa kuvaaa nguo ambayo mwanamitindo Fulani kaivaa hata ikiwa ni yagharama asiyoimudu atajali kulimbikiza fedha ili aweze kununua .

Nadharia hiii ndio iliowafanya viongozi wa Serikali kuamini kuiba pesa za Serikali kufanya mambo binafsi wakiamini maendeleo ya leo ni kuingia Serikalini kuchukua chako utoke.😁

Ukweli ni kuwa hiii nadharia inapaswa kukemewa Sana katika jamii kwasababu inachochea kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma mipango imara ya kimaendeleo.

EWE MWANAJAMII " NADHARIA YA MAENDELEO YA LEO " INAPASWA KUZINGATIWA VIZURI
 
Back
Top Bottom