Ndugu August, kama hukukusudia kupotosha kwa bandiko lako hili basi uelewa wako kwenye haya mambo bado ni mdogo.
Naona umetaja tu bila urari wala mantiki USSR ya Gorbachev na Ujerumani ya Hitler kama mifano yako 'bila katiba mpya", tena kwako hata dikteta fisadi Putin pia ni role model wa maendeleo.
Nigependa tuwe na mjadala mpana na sio propaganda, lakini kabla sijaenda mbele, je unajua Maendeleo ya Korea Kusini, Malaysia, Singapore, Ghana na Kenya yalipatikanaje?
Nchi kama Ujerumani na USSR (ulizotaja) na China uliyoitaja kwenye heading ni nchi/tawala/dola za zamani ni sawa sawa na tungesema Ufaransa, Japan na Canada au hata India, hao sio saizi yetu pia sio "rika" letu. Lakini hizo nchi nilizotaja hapo juu ni "rika" moja na sisi hivyo kama ni kujipima hao watatupa matokea halisi na yenye kushabihiana na sisi kama Taifa.