Maendeleo ya China yaliletwa na Katiba Mpya?

Maendeleo ya China yaliletwa na Katiba Mpya?

Hatuji ila tutasema. Maendeleo ya China yameletwa na uongozi bora. Maendeleo ya Rwanda yameletwa na uongozi bora. Mwalimu alisema: "Ili tuendelee tunahitaji watu siasa safi na uongozi bora." Hakusema na katiba mpya. Maendeleo ya Tanzania yataletwa na uongozi bora. Watu wakiuunga mkono uongozi wa Awamu ya 5, kama walivyounga mkono uongozi wa awamu zote tutapata maendeleo. Tunaona itihada za Raisi wa awamu ya 5 katika kuleta uongozi bora nchini.Bial shaka hatua za kuelekea kupata maendeleo zimekwisha anza kuonekana.

Hakuna Maendeleo yatakayo letwa na Utashi wa Mtu mmoja hata Siku moja ,sahau kabisa kuhusu hilo.Katiba ya Nchi ndio Mwongozo (Matakwa) ya Wananchi wanataka Nchi yao ienende kwa namna gani.Haiwezekani Mtu mmoja tu anaamka asubuhi anaamua kuvunja Mkataba (Kwa utashi wake) kisha tuna kuja kulipishwa Mabilioni ya Shilingi ya Walipa Kodi Masikini ,hatutaendelea kwa namna hiyo Mkuu...
 
..China na Rwanda "wamefanikiwa" huku wakiwa na katiba mbaya na sheria kandamizi.

..Tanzania tuna katiba mbaya. Pia mfumo wa vyama vingi upo ktk makaratasi tu, but in practice tunaendeshwa kama nchi ya chama kimoja--CCM.

..Kwa msingi huo basi unapozungumzia katiba, demokrasia, haki, na utawala bora, Tanzania inafanana na China na Rwanda.

..Sasa mfumo tulionao umekuwepo tangu miaka ya 60. Sote tunajua kwamba mfumo huo umeikwamisha nchi ktk tope la UMASIKINI. JE, kwanini tusibadilike?
Cha muhimu ni watu kuchapa kazi, mengineyo ni mazungumzo baada ya habari....enzi zile za kina Juma Ngondae wa RTD.
 
Walishaitupilia mbali siku nyingi.
Waliamini jiwe ni state na state ni jiwe.
Mkuu kwani katiba ni nini? Na kama katiba si muhimu nini maana ya kuendelea na hata hii tuliyonayo ya 1977? Kama katiba si muhimu why usiwashauri wanaccm wakaitupilia mbali katiba ya ccm ili wabaki na ilani tu? Tatizo kubwa la watanzania hasa wanaccm tunajilinganisha na mataifa mengine kwa mambo mabaya tu ili kuhalalisha ujinga wetu.right nguvu tunayoitumia kujilinganisha na wao kuhalalisha ujinga na upuuzi wetu tungetumia nguvu hiyo hiyo kujilinganisha hata katika mambo mazuri,Tanzania ingekuwa mbigu ya waafrica waliowengi
 
Back
Top Bottom