Waziri Kijaji: Tanzania ina viwanda 13 vya kuunganisha Magari

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
118,985
221,541
Taarifa hii iwafikie wabishi wote popote walipo, kwamba, ndani ya Tanzania kuna viwanda vya magari 13

Waziri wa Viwanda Dkt Kijaji amethibitisha
---


Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa Tanzania ina jumla ya viwanda 13 vya magari, kati ya viwanda hivyo, viwanda viwili (2) vinaunganisha magari ambavyo ni GF Trucks and Equipment Ltd kilichopo Kibaha, Pwani na Saturn Corporation Limited kilichopo Kigamboni, Dar es Salaam.

Dkt. Ashatu ameyasema hayo Leo Mei 21, 2024 Jijini Dodoma wakati akiwasilisha Hoja ya Bajeti ya Makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha 2024/2025 ya Wizara ya Viwanda na Biashara.

Dkt. Ashatu amesema kuwa Viwanda 11 vilivyosalia vinatengeneza matrela huku Kiwanda cha GF Vehicle Assemblers(GFA) sio GF Trucks & Equipment kina uwezo uliosimikwa wa kuunganisha magari 200 kwa mwezi na kimewekeza kiasi cha shilingi bilioni 10.752 na
kimetoa ajira 300.

Aidha Waziri huyo amefafanua kuwa . Ashatu Mradi wa Kiwanda cha Saturn Corporation Limited umegharimu mtaji wa kiasi cha shilingi bilioni 64.3 na kina uwezo uliosimikwa wa kuunganisha vichwa vya magari 900 na tipa 270 kwa mwezi huku kiwanda kikiajiri wafanyakazi 250.

PIA SOMA
- Waziri Kijaji: Tanzania ina viwanda vya chuma 28 vyatoa ajira 25,358 kwa Watanzania
 

Attachments

  • HOTUBA FUPI YA BAJETI - 2024-2025 - FINAL 21.05.2024 Read.pdf
    593.1 KB · Views: 1
Back
Top Bottom