Maembe aiomba BASATA na TRA kutowatoza kodi wasanii kwa muda huu wa zuio la mikusanyiko

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,069
10,012
Msanii wa muziki wa asili Vitali Maembe aliyewahi kutamba kwa kibao cha ‘Suma ya teja’ ameiomba serikali kuwasaidia wasanii kwa kipindi hiki cha marufuku ya siku 30 kama alivyotangaza waziri mkuu

Maembe ameiomba Wizara, BASATA NA TRA kuwapa unafuu wasanii kuwa kutowalipisha kodi kwa mwezi huu wa marufuku au serikali ijaribu kuwalipa wasanii waliosajiliwa kwa siku hizi ambazo mikusanyiko imezuiliwa

Ametumia msemo wa kiswahili wa Pwani kabisa, ‘Pa mwali pakiliwa na pa kungi napo paliwe’, Akiweka hoja ya kuwa wao kama wasanii wanapata hela kwenye mikusanyiko, na kama watatozwa kodi ilhali shughuli zao zipo katika marufuku anaona ni uonevu

Mawazo ya Vitalis Maembe yanfanana na mapendekezo aliyowahi kutoa Zitto Kabwe aliposhauri serikali itazame namna ya kuwafidia wafanyabiashara ili kulinda ajira za Wananchi

Msanii wa mashairi ya kuongea ‘spoken words poetry’ Malle Hanzi, alitofautiana na wazo hilo kwa kusema ni ubinafsi kuangalia maslahi ya wasanii peke yao na kusahau watu wengine wanaoathrirka kama washereheshaji, wapambaji, wauza vyakula nk

Post yake ameiandika hivi

MH. WAZIRI MKUU, BASATA na TRA
Mnatuachaje kwa siku hizi 30?

'Pa Mwali pakiliwa na pa Kungwi napo paliwe'

Serikali sikivu, Serikali ya wanyonge imetangaza kusitisha Shuguli zenye mikusanyiko isiyo ya lazima kwa Muda wa Mwezi mmoja!
Katika mikusanyiko hiyo isiyo ya lazima mojawapo na iliyosisitiziwa ni Maonesho na Matamasha ya Muziki!

Serikali imefanya Jambo la maana Sana kuwaepusha watu na Maambukizi, inaonesha inavyowapenda na kuwajali wasanii na wapenzi wao.
Muziki ni Kazi lakini ni kazi isiyo ya lazima, (waonavyo wao) na Kama ingekuwa ni kazi ya lazima basi Serikali ingetoa tamko lolote linaloonyesha linalojali kundi hili dogo la WALIPA KODI hawa katika kipindi hiki cha mpito.

BASATA na TRA
Tunawapa pesa kila kukicha, mnatulipisha Kodi kila kazi tunayofanya na ambazo hatujazifanya, na wengine tumesajiliwa na tumelipa vibali vya kazi na Mwezi huu unahesabiwa na Mwezi huu ndio hakuna 'Kimeo' kinachoruhusiwa.

Mnatuambiaje wananchi wenzenu, Familia zetu zitakula nini na watoto wote Sasa wapo nyumbani, mahitaji yameongezeka kutokana na janga hili.
Tumezowea kuwa, Wasanii wa Muziki ni wasindikizaji wa Maisha ya watu, watu wengi kama wanasiasa, viongozi wa Serikali na wafanyabiashara.

Nikiondoa neno tunachukuliwa kuwa ni Watumwa, naweza kusema kuwa wanajamii hawa wanatuaona wanamuziki kama Vijibwa au Vikaragosi vyao.
Wananchi wa kawaida nao wakiona Mwanamuziki ananyanyaswa na kunyimwa Haki yake wananyamaza tu, wanaona kuwa ni sawa tu!

Lakini mwanamuziki akielemewa na ugumu wa Maisha akapoteza muelekeo inakuwa ndiyo furaha, burudani, kichekesho chao mtaani, mitandaoni.
Waandishi wa habari ndiyo unakuwa mradi wao, watamfuata Mpaka nyumbani wamsumbue kufosi habari, utasikia kapoteza, kawa mlevi, kawa....
Wapenzi wanafiki nao wanawabwaga eti wanachagua msanii mwingine wa kumpenda!
Wazo!
Mwezi huu tusikatwe Kodi na Usihesabiwe kwenye Vibali vyetu.
Au Serikali itulipe tuliosajiliwa na tunaolipa Kodi mshahara wa mwezi mmoja.
Au Kama hiyo ni Hasara kwa Serikali basi BASATA, WAZIRI na TRA

Muungane nasi WASANII wa Muziki, msipokee mishaahara yenu ya Mwezi huu, pesa yenu isaidie Serikali kwenye gharama za tahadhari na hasara iliyotokana na janga hili la CORONA.

MUHIMU
HUU UGONJWA WA CORONA UPO, CHUKUA TAHADHARI NA ISAIDIE SERIKALI KUTATUA TATIZO..

Na sie tunaouza bidhaa gulioni ktk mikusanyiko je? Hilo ombi halima uzito. Kama ndio hivyo ziorodheshwe biashara zooooote ambazo ni mpaka mkusanyiko uwepo ndio watu wapate hela, kisha zifanyiwe msamaha zote hizo je itawezekana?

Halafu, kwani wasanii wao ni kina nani??? Sana sana wanaangusha maadili ya mtanzania kila siku. Hakuna.

Msamaha hapo
 
Nimependa huo msemo tu.

"Pa mwali pakiliwa na pa kungwi paliwe"
 
NA SIE TUNAOUZA BIDHAA GULIONI KTK MIKUSANYIKO JE ? HILO OMBI HALIMA UZITO. KAMA NDIO HIVYO ZIORODHESHWE BIASHARA ZOOOOOTE AMBAZO NI MPAKA MKUSANYIKO UWEPO NDIO WATU WAPATE HELA, KISHA ZIFANYIWE MSAMAHA ZOTE HIZO JE ITAWEZEKANA ?

HALAFU, KWANI WASANII WAO NI KINA NANI??? SANA SANA WANAANGUSHA MAADILI YA MTANZANIA KILA SIKU. HAKUNA.

MSAMAHA HAPO
nyie endeleeni kuuza bidhaa zenu kwenye mitandao ya kijamii.
 
Msanii wa muziki wa asili Vitali Maembe aliyewahi kutamba kwa kibao cha ‘Suma ya teja’ ameiomba serikali kuwasaidia wasanii kwa kipindi hiki cha marufuku ya siku 30 kama alivyotangaza waziri mkuu

Maembe ameiomba Wizara, BASATA NA TRA kuwapa unafuu wasanii kuwa kutowalipisha kodi kwa mwezi huu wa marufuku au serikali ijaribu kuwalipa wasanii waliosajiliwa kwa siku hizi ambazo mikusanyiko imezuiliwa

Ametumia msemo wa kiswahili wa Pwani kabisa, ‘Pa mwali pakiliwa na pa kungi napo paliwe’, Akiweka hoja ya kuwa wao kama wasanii wanapata hela kwenye mikusanyiko, na kama watatozwa kodi ilhali shughuli zao zipo katika marufuku anaona ni uonevu

Mawazo ya Vitalis Maembe yanfanana na mapendekezo aliyowahi kutoa Zitto Kabwe aliposhauri serikali itazame namna ya kuwafidia wafanyabiashara ili kulinda ajira za Wananchi

Msanii wa mashairi ya kuongea ‘spoken words poetry’ Malle Hanzi, alitofautiana na wazo hilo kwa kusema ni ubinafsi kuangalia maslahi ya wasanii peke yao na kusahau watu wengine wanaoathrirka kama washereheshaji, wapambaji, wauza vyakula nk

Post yake ameiandika hivi

MH. WAZIRI MKUU, BASATA na TRA
Mnatuachaje kwa siku hizi 30?

'Pa Mwali pakiliwa na pa Kungwi napo paliwe'

Serikali sikivu, Serikali ya wanyonge imetangaza kusitisha Shuguli zenye mikusanyiko isiyo ya lazima kwa Muda wa Mwezi mmoja!
Katika mikusanyiko hiyo isiyo ya lazima mojawapo na iliyosisitiziwa ni Maonesho na Matamasha ya Muziki!

Serikali imefanya Jambo la maana Sana kuwaepusha watu na Maambukizi, inaonesha inavyowapenda na kuwajali wasanii na wapenzi wao.
Muziki ni Kazi lakini ni kazi isiyo ya lazima, (waonavyo wao) na Kama ingekuwa ni kazi ya lazima basi Serikali ingetoa tamko lolote linaloonyesha linalojali kundi hili dogo la WALIPA KODI hawa katika kipindi hiki cha mpito.

BASATA na TRA
Tunawapa pesa kila kukicha, mnatulipisha Kodi kila kazi tunayofanya na ambazo hatujazifanya, na wengine tumesajiliwa na tumelipa vibali vya kazi na Mwezi huu unahesabiwa na Mwezi huu ndio hakuna 'Kimeo' kinachoruhusiwa.

Mnatuambiaje wananchi wenzenu, Familia zetu zitakula nini na watoto wote Sasa wapo nyumbani, mahitaji yameongezeka kutokana na janga hili.
Tumezowea kuwa, Wasanii wa Muziki ni wasindikizaji wa Maisha ya watu, watu wengi kama wanasiasa, viongozi wa Serikali na wafanyabiashara.

Nikiondoa neno tunachukuliwa kuwa ni Watumwa, naweza kusema kuwa wanajamii hawa wanatuaona wanamuziki kama Vijibwa au Vikaragosi vyao.
Wananchi wa kawaida nao wakiona Mwanamuziki ananyanyaswa na kunyimwa Haki yake wananyamaza tu, wanaona kuwa ni sawa tu!

Lakini mwanamuziki akielemewa na ugumu wa Maisha akapoteza muelekeo inakuwa ndiyo furaha, burudani, kichekesho chao mtaani, mitandaoni.
Waandishi wa habari ndiyo unakuwa mradi wao, watamfuata Mpaka nyumbani wamsumbue kufosi habari, utasikia kapoteza, kawa mlevi, kawa....
Wapenzi wanafiki nao wanawabwaga eti wanachagua msanii mwingine wa kumpenda!
Wazo!
Mwezi huu tusikatwe Kodi na Usihesabiwe kwenye Vibali vyetu.
Au Serikali itulipe tuliosajiliwa na tunaolipa Kodi mshahara wa mwezi mmoja.
Au Kama hiyo ni Hasara kwa Serikali basi BASATA, WAZIRI na TRA

Muungane nasi WASANII wa Muziki, msipokee mishaahara yenu ya Mwezi huu, pesa yenu isaidie Serikali kwenye gharama za tahadhari na hasara iliyotokana na janga hili la CORONA.

MUHIMU
HUU UGONJWA WA CORONA UPO, CHUKUA TAHADHARI NA ISAIDIE SERIKALI KUTATUA TATIZO..
'Pa Mwali pakiliwa na pa Kungwi napo paliwe'
Kuwaomba TRA kutolipa kodi ni kama kuomba usipumue kwa muda hadi taabu ipite!!!
 
Back
Top Bottom