Mimi mwana CCM Kindakindaki naapa kuwa nitampigia kura Edward Ngoyai Lowassa anayeiwakilisha CHADEMA kupitia mwamvuli wa Muungano wa vyama vya UKAWA. Kama kunawakati ambapo CCM inahitaji kujipanga vyema na kurekebisha mapungufu yaliyopo wakati huo ndio sasa.Kwa yeyote anayeipenda CCM kama mimi,naomba kwa Moyo Mkunjufu tuiweke CCM pembeni ili ikajikague,ikajitafakari na kisha ijipange kwa ajili ya 2020 - 2025.Gari ama mashine yeyote ile hata iwe tingatinga ikiharibika sharti iwekwe pembeni ili ifanyiwe marekebisho.Ukiilazimisha iendelee na kazi ama iendelee na safari madhara yake ni makubwa sana kwa abiria,mazingira na hata watu waliokaribu na mashine hiyo!!Kataa vitisho,kataa kununuliwa kama bidhaa,kataa uchochezi,kataa michezo michafu ya Kisiasa...Jiandae kupiga kura yako kwa Diwani,Mbunge na Rais wa UKAWA.....MUNGU ibariki TANZANIA na watu wake wote!!