Maelfu ya Wakulima wakesha wakisafiri usiku kucha kumfuata Rais Samia mkoani Mbeya

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,311
9,740
Ndugu zangu watanzania,

Ni upendo wa ajabu ,ni Kitendo cha kipekee ,ni Tukio la kuvutia,Ni Hatua iliyoteka hisia za watu wengi sana Baada ya kushuhudia maelfu ya wakulima kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa ya nyanda za juu kusini wakikesha wanasafiri usiku kucha kwenda kuonana na kumsikiliza Rais samia mkombozi wa wakulima ,Nuru ya wanyonge,Taa ya wapambanaji, Tabasamu la wengi ,furaha ya Taifa na jasiri muongoza njia aliyeleta na kuchochea mapinduzi ya kilimo hapa nchini na kuwafuta machozi wakulima waliohangaika na kilimo kwa miaka mingi pasipo kuinuka na kunyoosha migongo yao.

Wengi wao ambao ni wakulima wameonyesha kuguswa sana na namna Rais samia alivyogusa maisha ya wakulima wengi na kuleta mabadiliko katika kaya nyingi, ambapo kupitia kilimo sasa umasikini umebakia historia kwa kaya nyingi, hii ni baada ya kuwafanya wakulima kufaidika na jasho lao, hii ni baada ya Rais samia kukataa unyonyaji kwa mkulima,kukataa mkulima kuwa daraja la kuwavusha wengine huku yeye akibakia pale pale katika dimbwi la umaskini akishindwa kujenga nyumba bora, kusomesha watoto, kuwa na bima ya afya,maisha bora ,kuhudumia familia yake,kupata milo mitatu n.k, sasa kilimo kimekuwa kimbilio la wengi na wengi wanajisikia fahari kuwa wakulima na kufanya shughuli za kilimo, Hii ni baada ya Rais samia kukipa heshima yake na kutambua mchango wa wakulima katika kutunza usalama na utulivu wa Taifa letu.

Sasa wakulima wanakwenda na kumiminika kwa maelfu mkoani Mbeya katika kilele cha siku kuu za maonyesho ya nane nane ili kwenda kumsikiliza shujaa na mkombozi wao katika kilimo ,kumpa asante, kumshukuru,kumtia moyo ,kumpa faraja,kumuunga mkono na kumuahidi kuendelea kumpa ushirikiano katika uendeshaji wa serikali yao. Wanakwenda kuonyesha kuwa wameridhishwa na uchapa kazi wake na amekidhi matarajio ya mamilioni ya wakulima hapa nchini.

Wanakwenda kumvalisha medali ya ushujaa na uchapa kazi na utendaji kazi uliotukuka,wanakwenda kumtunuku Heshima ya kipekee na kutambua mchango wake katika kilimo na wanakwenda kumwambia kuwa wamemuandalia kura za kishindo uchaguzi ujao kama shukurani kwa mchango wake katika kilimo.

Kwa hakika kila ulimi unaendelea kukiri na kusema kuwa Rais samia anatosha kutuvusha watanzania mpaka 2030, Anastahili kuendelea kuaminiwa ,anastahili kuendelea kuungwa mkono ,anastahili kutiwa faraja na anastahili kuwa Nembo ya Taifa letu,kwa kuwa ameleta matumaini,furaha na Tabasamu katika mioyo ya wengi.Rais samia hazuiliki wala hapingiki katika mbio za urais.

Hatuwezi kumtoa Rais samia na kumuweka pembeni maana itakuwa ni sawa na kulifunga kamba Taifa katika mbio na kasi ya maendeleo,itakuwa ni kulirudisha nyuma Taifa ,itakuwa ni kujikoroga wenyewe,itakuwa ni kulikwamisha Taifa,itakuwa ni kutolitendea haki Taifa na watanzania wote kwa jumla.

Kwa kuwa ikumbukwe ya kuwa ni samia ndiye ameleta Elimu bure mpaka kidato cha sita,kuongeza bajeti ya kilimo katika historia ya Taifa letu kufikia billion mia Tisa 70,kujenga vituo vya afya mamia kwa mamia,kuboresha huduma za afya kuanzia ngazi za zahanati mpaka Taifa, kupandisha mishahara kwa watumishi wa umma,kutoa ajira kwa maelfu ya vijana kila mwaka,kujenga miradi na kuikamilisha ndani ya muda mfupi,kuongeza ukusanyaji wa mapato pasipo nguvu wala mtutu wa bunduki wala kufungiana biashara kufikia Trilioni mbili kwa mwezi,kukuza uchumi wetu na kuongeza mzunguko wa fedha mitaani , Biashara kufunguliwa na kushamiri kila kona ya nchi,kuongeza fedha za kujikimu kwa wanafunzi wa Elimu ya juu kufikia Elfu kumi kwa siku.

Kuimarisha Demokrasia,utawala bora na kuheshimu haki za binadamu,kutoa uhuru wa watu kuzungumza mpaka watu wanaishiwa vya kuzungumza na kuanza kutukana kama wafanyavyo akina Lissu na genge lake,kuleta maisha bora kwa watanzania wengi ambao wengi sasa wanapata milo mitatu badala ya kula mara moja kwa siku, kukuza utalii na kuchochea uwekezaji wenye Tija, kuifanya Tanzania kuwa changuo namba moja la wafanyabishara bila kusahau namna alivyokuza na kuleta hamasa katika michezo na burudani.Aliyoyafanya Rais samia na serikali yake ya CCM ndani ya muda mfupi wa uongozi wake ni mengi sana ambayo huwezi ukamaliza kuyaorodhesha hapa.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa,kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
CCMtumekataa CHAWA. Mbona unakaza fuvu?

Hatuteui machawa tena.
JamiiForums-1016409659.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi wewe ni mwanaume? Na kama ni mwanaume umeoa? Na kama umeoa una watoto?

Sioni ni namna gani unaweza ongoza familia na kulea watoto kwa namna ulivyo wa hovyo.
Kwani hoja yangu ni wapi inapozungumzia habari za ndoa au sheria za ndoa. Na ni vipi ndoa au watoto wanaongeza uzito wa hoja hapa jukwaani, acha kuonyesha umbumbumbu wako wa kihoja hapa.
 
Ila wewe kiumbe ni umepitiliza mpaka kwenye kiwango cha kuitwa CHAWA aisee! Sasa hao maelfu ya wakulima wanaosafiri usiku kucha kumfuata huyo mama huko Mbeya wanatokea wapi!!!
Wanatokea mikoa ya nyanda za juu kusini ambako kama unavyojua ndugu yangu Tate mkuu hii ndio mikoa inayoongoza kwa kilimo na uzalishaji wa mazao ya chakula chote kinachotumiwa na watanzania hapa nchini na hata nchi jirani kama kenya.
 
Ndugu zangu watanzania,

Ni upendo wa ajabu ,ni Kitendo cha kipekee ,ni Tukio la kuvutia,Ni Hatua iliyoteka hisia za watu wengi sana Baada ya kushuhudia maelfu ya wakulima kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa ya nyanda za juu kusini wakikesha wanasafiri usiku ti.

Lucas Hebel mwashambwa,kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Ni mkulima kichaa peke yake anayeweza kukesha kumsubiri huyo uliyemtaja. Wewe ni mzalendo kichaa
 
Ndugu zangu watanzania,

Ni upendo wa ajabu ,ni Kitendo cha kipekee ,ni Tukio la kuvutia,Ni Hatua iliyoteka hisia za watu wengi sana Baada ya kushuhudia maelfu ya wakulima kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa ya nyanda za juu kusini wakikesha wanasafiri usiku

0742-676627.
KWELI MKUUU. BEI YA MAZAO NI NZURI WATU WANATOBOA.
WALALAMISHI WAACHE WAEENDFLEE KULALAMA. LISU ALIKIMBUA JAMA PANTA LEO AMERUDI KWA HURUMA YA SAMIS.
SITAKI KUONGEZA UMEANDIKA MENGI .
 
Back
Top Bottom