ndugu hebu tuone hili. serikali imeshindwa kuajiri watu, sekta binafsi nako hakuna ajira. watu wengi wanasema serikali iliyopo ikiondoka madarakani ndo suluhisho hata mi naona kwa sehemu hilo ni suluhisho lakini hata kikiingia chama pinzani kinaweza ajiri watu wote?. mtu atasema kinatakiwa kitengeneze mazingira ya mtu kuweza kujiajili je kisipoingia madarakani inamaana mtu huyu atasubiri miaka mingine mitano na pengine kumi aje kutengenezewa mazingira ya kujiajiri! mi suluhisho la haraka kwa hii hali naona ni vijana waliomaliza shule kukaa pamoja wawili watatu kupanga mpango na kuhakikisha wanachukua hatua (kinachosumbua sana ni kuchukua hatua). we unafikiri suluhisho la haraka la hii hali ni lipi?
Kaka/dada nasikitika sipendi nikuvunjie heshima
1. Nani kakwambia serikari imeshindwa kuajiri na kwanini iajiri serikali? 2. nani kwambia kuna serikali dunian imeajiri watu wake wote? toa mfano
Nyinyi watu ndo mnatufanya wakenya watudharau watanzania kila siku kwa mawazo mgando ya ovyo kama haya yako.
Kazi ya serikali ni kujenga mazingira mazuri ya vijana kuajiriwa na kujiajiri (sifa kubwa kwa viongozi wenye maono na upeo)
- Serikali lazima iwe na mikakati ya wazi kuwekeza kwenye nyanja za kupanua ajira
Mfano
Serikali haikupaswa kuuza mashirika na viwanda mbalimbali vya uzalishaji, kwa maana huko ajira ingepatikana
Viwanda vyote vya nguo ni mahututi, ni watanzania wangapi wangeajiriwa na kuongeza mzunguuko wa fedha kuwafikia machinga, mama lishe na wakulima....... Tafakali. Vijana wote hao wangefaidika kwa uwepo wa ufanisi wa viwanada vya nguo tu - isitoshe soko la pamba la uhakika lingepatina, kama huna cha kuchangia kaa kimya.
Ukienda tanga, Kulikuwa na Kiwanda cha mbolea, kiwanda cha chuma, kiwanda cha plastic ambon, bandari wakati huo, vyote hivi vingeendeshwa kwa ufanisi watanzania wangapi wapepata ajira na kuingiza mzunguuko wa fedha kama nilivoanisha hapo juu!!!! kwa ujinga na uwezo mdogo wa viongozi chini ya chama cha ccm tumeuwa kila kitu.
Mifano iko mingi naachana nayo inatosha hiyo ukiacha kiwira, chai, kahawa, mkonge, Tumbaku, madini, kiparapara na hasari tumeuwa kilimo -kumbuka vyama vya ushirika vikuwa na nguvu sana lakini vikauwawa kimtindo kwa nini nk
Tunataka serikali ijenge mazingira ya
kufufuliwa viwanda vilivokufa na pia kufanya juhudi za makusudi kuingia ubia na makampuni ya inje viwanda vingine vianzishwe kwa usimamizi wa serikali siyo kuwaachia wageni 100% na kutesa ndugu zetu wakitanzania. Serikali iwabane mafisadi ili fedha itakayopatikana wakopeshwe vijana kwa misingi ya kuwawezesha- unataka sasahivi waunganishe nguvu, nguvu gani hawana fedha au wajifunge yokes shingoni wavute plau walime jamani hawana fedha watajiunga kufanya nini? wanahitaji kukopeshwa ili wakalime!!!!!!!!!!!!!!!!!
Hata ujerumani na marekani wapo wasiokuwa na kazi, lakini sio kama ilivyo kwa tanzania. hakuna serikali duniani inayoweza kuajiri raia wake wote. Moja ya sifa za viongozi katika nchi za ujerumani na marekani ni uwezo wa kuongeza ajira na kupunguza mfumko wa bei sio kama viongozi wako wanao toa taarifa hewa kila siku na kuvaa mashati ya kijani na kuhonga wafia njaa pilau, unaweza kuhonga pilau na kofia marekani wewe? hii inathibitisha vijana wamepigika ndo maana wakocheap kiasi hicho - Acheni siasa tunapojadili mambo ya msingi jamani.
Kusema kwa sababu hujawahi safiri na basi jipwa, ni bora kuendela na lazamani kwa sababu hutambui umadhubuti wa lile geni, ni ufinye wa mawazo chanya. kwahiyo kwenu CCM ndio kila kitu, vipi nchi zingine wanakobadili vyama na watawala kila siku wamegeuka mawe? mfano kenya, Zambia, malawi, Ghana nk. Mnaongelea kuthubutu, vijana hawathubutu kuanzisha miradi mbona nyinyi mnashinndwa kuthubutu kukiingiza chama kingine madarakani na kusingizia hamna uhakika na wageni!Kuweni jasiri wa kufanya maamuzi sahihi. CCM imechoka tuingize chama kingine iwe CUF, Chadema au NCCR ni sawatu.