Mkuu huwa naheshimu sana dini za wengine lakini kwa hapo kwenye yesu kuhukumu watu nimetamani hata kudeletia mbali hii thread nzima maana kumbe unajua jina la yesu ila humfahamu Yesu ni nani wakristo wenzio watakusaidia,
Mathayo 7:21-23 Neno:
Mfuasi Wa Kweli
21 “Si kila mtu anayesema, ‘Bwana, Bwana,’ ambaye ataingia katika Ufalme wa mbinguni ila ni wale wanaofanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Siku ile itakapofika wengi wata niambia, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii na kufukuza pepo kwa jina lako; na kufanya miujiza mingi ya ajabu kwa jina lako?’ 23 Ndipo nitawaambia wazi, ‘Sikuwafahamu kamwe. Ondokeni kwangu ninyi watenda maovu!’
Kutoka 20:3-5 Imeandikwa "Usiwe na miungu mingine ila mimi.
Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao."
Tubu mkuu maana hadi hapo uko mbali na Yesu wako pia watafute wakristo wakufundishe ni yupi mungu ambaye ni hakimu
Rakims