Maduka ya Kinondoni bwana

shelumwa

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
516
Reaction score
190
Ni leo usiku huu nimeenda dukani nikaulizia chumvi sasa nikajibiwa hakuna nikauliza tena kama chumvi wanayo wakasisitiza kua hakuna, nikaamua kuondoka kwenda duka jingine lakini baada ya hatua kadhaa akaja binti huku anakimbia akiniita kugeuka akaniambia hivi "KAKA USIKU HATUUZAGI CHUMVI TUNAUZA DAWA YA JIKO/DAWA YA CHAKULA".

Nikarudi kusema naomba dawa ya jiko kama nilivyoambiwa nikapewa kuangalia nikakuta ni chumvi sasa nimeshangaa sana inakuaje bidhaa hii ya chumvi usiku inaitwa kwa jina jingine je ni kawaida au imani za gizani maana sijaelewa nini maana ya kunyimwa chumvi kisa jina nililotumia.

HII NI DESTURI YA WAPI? JE, IPO HAPA HAPA KINONDONI AU NA KWINGINE NIJUZE!!
 
mme alafu sijajua kama umri wangu unasaidia nini katika ili jambo
 
Swali la mke mme anakutaka huyo msikilize...anatokea wapi kwanza..pemba unguja??
 

....sehemu nyingi Tanzania
 
Yaabda tupate ufafanuzi kwenye hoja ua msingi ambapo ni kwann hii kitu inachange jina kutokana na wakati! Ukiita chumvi usiku inamadhara gani?
 
Mbona tangu miaka chumvi hubadilika jina usiku......na wsla si kinondoni pekee bali ni Tanzania nzima.....!

mimi nimezaliwa na kukulia Dar hii hali nimeikuta kinondoni mpaka mtu wa duka kugoma kukuuzia chumvi kisa jina nililotumia ni mpya kwangu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…