Madudu ya Chama cha Walimu (CWT)

Mdaiwa-Sugu

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
284
910
CWT inavuna pesa za walimu isivyohalali kila mwezi kutokana na ukweli kuwa kwa mujibu wa sheria zilizopo hawana mamlaka ya kuchukua ada ya uanachama kwa asilimia ya mshahara wa mtumishi.

Nasema hayo kwakuwa hakuna sheria yoyote nchini Tanzania inayowaruhusu kufanya hivyo;

Kuna sheria ya mwaka 1961,"The organization of Tanzania Trade union Act,1961,[Act no. 20/91], the trade union ( Revocation of special powers)

Kuna sheria ya mwaka 1964[ Act no. 64/64] hadi hii ya sasa iliyofanyiwa marekebisho 2006 " The Trade union Act, 1998".

Katika sheria zote hizo hakuna mahali ambapo wamepewa mamlaka ya kukata mshahara wa mfanya kazi kwa kutumia asilimia isipokuwa kwa sheria ya "Employment and labour relations Act, 2004 part 4 ndiyo inayotoa maelekezo ya kitu gani kifanyike baada ya mwajiriwa kuridhia mbele ya mashahidi kuhusu makato husika ( siyo kwa %) ya mshahara wake kwenda katika Trade union husika.

Pamoja na upungufu huo mkubwa wa kisheria ila CWT pia inaupungufu mkubwa wa kiutendaji;

1. Wanachama wamenyimwa fursa na demokrasia ya kutoa mawazo na kutatua matatizo yao kwa njiavya mikutano katika vituo vyao vya kazi kwa sababu katiba ya CWT, toleo la tarehe 18 December 2009 kifungu cha 11(a)-(c), haviwapi madaraka wawakilishi kuitisha mikutano katika sehemu zao za kazi.

2. CWT imejilimbikizia wanachama hivyo kushindwa kuwahudumia wanachama wake kwa urahisi na usahihi. Walimu wote kuanzia msingi hadi vyuo vikuu wanahudumiwa na CWT. Eneo lake la kiutendaji ni pana sana hivyo kushindwa kuwahudumia walimu kwa ufanisi.

3. Chama hakina uwazi katika matumizi ya pesa za wanachama na wasio wanachama wake. Kwa mfano, makato ya ada ya uwakala(agency fee) ya wasio wanachama yanapaswa kuwekwa katika akaunti tofauti na ile ya wanachama wake kutokana na kifungu cha 72(3)(e) cha sheria ya ajira na mahusiano kazini Na. 6/2004.

4.Mapato yatokanayo na vitega uchumi vya chama mfano Mwalimu house na ofisi za CWT kila mkoa (rent), havimnufaishi mwalimu ambaye ni mchangiaji mkuu.

5.CWT wanakusanya michango kwa wanachama kila mwezi badala ya kukusanya mara moja kwa mwaka kama vyama vingine.

6.Walimu wanaokatwa asilimia 2% Wanakadiriwa kuwa zaidi ya 200,000,CWT wenyewe hawana idadi kamili,hivyo wanakusanya zaidi ya BILIONI 3 kila mwezi. Pamoja na fedha yote hiyo Kuna tetesi kuwa wamekopa shilingi bilioni saba mwaka huu.... Hizo fedha walizokopa Ni za nini?

7.Kwanini kuna tofauti katika makato ya kuchangia mfuko wa C.W.T wakati huduma ni sawa? Kuna nini kinachoongezeka kwa anayekatwa zaidi na nini kinachopungua kwa anayekatwa chini?

8. CWT wanafanya biashara ya Majengo kupitia kampuni ya TEACHERS DEVELOPMENT COMPANY LTD.Lengo kuu la CWT ni kutetea maslahi ya Mwalimu (mwanachama wake) na si biashara maana hata sheria inakataza chama cha wafanyakazi kufanya biashara. Nani aliwaruhusu kufanya biashara?

9. Ile Bank ya waalimu iliyoanzishwa toka 2015 na waalimu kupewa hisa za elfu hamsini Nani aliwahi kupata gawio la hisa zile?

10. Sheria ya Ajira na mahusiano Kazini inataka vyama vyote vya wafanyakazi wasikatwe mishahara yao bila kuridhia au kwa kutumia asilimia. Kwa Nini CWT imekiuka haya yote na hawashitakiwi Wala kuhojiwa?

11. Ni kwa Nini mishahara ya watendaji haipo wazi kwa wanachama? Je watendaji wapo wangapi? Maana kila ukiulizia fedha utaambiwa inatumika kulipa watumishi.

Tujikumbushe nyuma kidogo

Tarehe 27/3/2017 Katibu mkuu kiongozi alimuomba CAG afanye ukaguzi kwenye chama cha Waalimu CWT. Ukaguzi huo ulijikita katika tuhuma dhidi ya Uongozi wa chama cha waalimu zinazohusu ubadhirifu wa fedha na mali za chama.

Ukaguzi maalumu ulikagua taarifa za mapato na matumizi ya Chama, Uliangalia uhusiano uliopo kati ya Benki ya waalimu na waalimu wenyewe, uhusiano uliopo kati ya Mwalimu house na mwalimu mwenyewe.

YALIYOBAINIKA BAADA YA UKAGUZI HUO NI HAYA

1.Hakuna mfumo mzuri wa wanachama unaoonyesha kumbukumbu za wanachama. Katiba ya CWT inaeleza kuwa kunatakiwa kuwe na aina nne za wanachama lakini CWT hawaonyeshi aina hizo za wanachama hivyo haijulikani CWT ina wanachama wangapi.
Pia katika swala la wanachama hakuna taarifa zinazoonyesha wanachama walijiunga lini, mishahara yao kwa mwezi, namba ya uanachama, kiwango anachochangia kwa mwezi nk. Jambo hili CAG anasema kuna uwezekano kuna fedha nyingi zinaliwa kutokana na kutokuwepo kwa taarifa hizo.

2.Malipo ya shilingi 11,924,250,620.13 yakifanyika bila viambatanisho vyovyote. Hii ina maana hakuna nyaraka zinazoonyesha matumizi sahihi ya fedha hizo.

3. Shilingi 3,287,708,358 zilipwa bila kuidhinishwa na katibu mkuu au mweka hazina wa Chama na pia hakuna viambatanisho.

4. Shilingi 11,924,250,620.13 zililipwa bila kuzingatia makisio. Hii ina maana fedha hizi zilitumika bila kuzingatia bajeti ya CWT.CAG anasema viongozi wanakosa nidhamu ya matumizi ya fedha hivyo kuna fedha hapa zilitumika bila wanachama kujua zimekwenda wapi.

5. Hakuna nyaraka zinazoonyesha umiliki wa moja kwa moja wa CWT na miradi yake.

6. Hakuna nyaraka zinazoonyesha mtiririko wa mapato wa vitega uchumi vya chama toka CWT kianzishwe.

7.Mwalimu House imesajiliwa Brela kwa jina lingine la Teachers Development kupitia usajili wa Brela 45719 Badala ya TDCL. Na CAG amebaini kuwa kampuni hilo la Teachers Development halijawahi kufanya kazi toka kuanzishwa kwake. Kwa hiyo mapato yake hayaonekani.

Mbali na ukaguzi wa CAG, mnamo tarehe 14/3/2019 pia msajili wa vyama vya wafanyakazi nchini aliwaandikia CWT barua akitaka wajibu hoja zaidi ya kumi za ubadhirifu wa mali za chama hicho. Barua hiyo yenye kumbukumbu na. RTU/CWT/VOL.IV/12/89 iliwataka kwa haraka sana CWT kujibu hoja za ubadhirifu huo wa mali za chama ambazo zilikuwa zinalalamikiwa na baraza la wadhamini lakini mpaka leo hawajajibu na wala hakuna hatua zozote msajili alizochukua hadi sasa.

itaendelea.....

credited : Thadei ole mushi.
 
Hivi ni lazima kuwemo kwenye hicho chama ?

Yaani hakuna Option ya kujitoa kama ulijiunga na hutaki kuendelea ?
 
Walimu ni kama "punching bag" unajipigia tu..hata kesho kutwa wakiambiwa mtapunguziwa mishahara kuna corona hawana neno..
Kwa upande mwingine naweza kusema Walimu ndiyo wafanyakazi watiifu pengine kuliko kada nyingine kwahiyo CWT wanatumia utiifu wa walimu kama fimbo ya kuwaadhibia kwenye maslahi yao
 
Walimu wakiamua kusema hawataki chama, hakuna wa kuwalazimisha. Ulazima unakuja kwa kuwa majority wamekubali
Kazini kwetu tuna option ya kuchagua kuwa mwanachama wa chama kimoja kati ya viwili vilivyopo.Chenye wanachama wengi ndo kitatambulika na mwajiri. wafanyakazi wengi hawajachagua chama kati ya hivyo viwili
hivyo hakuna chama chenye haki ya kulazimisha uanachama au kukata mtu mchango kisa ni mwajiriwa wa hapa
 
CWT ni kitega uchumi cha serikali ya ccm kwasababu hata kama mtumishi hujajiunga lazima hela yako inakatwa na serikali inalijua hilo lakini hakuna hatua zinazochukuliwa.

Mwalimu haruhusiwi kujitoa hata ukijitoa hela yako inaendelea kukatwa tu.

Pamoja na madudu yote yanayofanyika lakini serikali ipo kimya kwakuwa yenyewe ndio mnufaika namba moja.

Ingekuwa kujiunga ni hiari ya mwalimu nadhani wangejiunga wacheche sana kwasababu hiki chama hakina faida yoyote kwa mwalimu wa kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuwatetee walimu, peke yao hawawezi
Sio rahisi kuwatetea na kusikika maana serikali Inajua haya yote na Ipo kimya means msaada kutoka kwa watetezi huru utasikilizwa kwa mbinde or kutokufanyiwa kazi kabisa.
Muhimu watetezi huru waendelee kupaza sauti hadi tone la mwisho huezi jua kesho Itakuwaje.
 
CWT inavuna pesa za walimu isivyohalali kila mwezi kutokana na ukweli kuwa kwa mujibu wa sheria zilizopo hawana mamlaka ya kuchukua ada ya uanachama kwa asilimia ya mshahara wa mtumishi.

Nasema hayo kwakuwa hakuna sheria yoyote nchini Tanzania inayowaruhusu kufanya hivyo;

Kuna sheria ya mwaka 1961,"The organization of Tanzania Trade union Act,1961,[Act no. 20/91], the trade union ( Revocation of special powers)

Kuna sheria ya mwaka 1964[ Act no. 64/64] hadi hii ya sasa iliyofanyiwa marekebisho 2006 " The Trade union Act, 1998".

Katika sheria zote hizo hakuna mahali ambapo wamepewa mamlaka ya kukata mshahara wa mfanya kazi kwa kutumia asilimia isipokuwa kwa sheria ya "Employment and labour relations Act, 2004 part 4 ndiyo inayotoa maelekezo ya kitu gani kifanyike baada ya mwajiriwa kuridhia mbele ya mashahidi kuhusu makato husika ( siyo kwa %) ya mshahara wake kwenda katika Trade union husika.

Pamoja na upungufu huo mkubwa wa kisheria ila CWT pia inaupungufu mkubwa wa kiutendaji;

1. Wanachama wamenyimwa fursa na demokrasia ya kutoa mawazo na kutatua matatizo yao kwa njiavya mikutano katika vituo vyao vya kazi kwa sababu katiba ya CWT, toleo la tarehe 18 December 2009 kifungu cha 11(a)-(c), haviwapi madaraka wawakilishi kuitisha mikutano katika sehemu zao za kazi.

2. CWT imejilimbikizia wanachama hivyo kushindwa kuwahudumia wanachama wake kwa urahisi na usahihi. Walimu wote kuanzia msingi hadi vyuo vikuu wanahudumiwa na CWT. Eneo lake la kiutendaji ni pana sana hivyo kushindwa kuwahudumia walimu kwa ufanisi.

3. Chama hakina uwazi katika matumizi ya pesa za wanachama na wasio wanachama wake. Kwa mfano, makato ya ada ya uwakala(agency fee) ya wasio wanachama yanapaswa kuwekwa katika akaunti tofauti na ile ya wanachama wake kutokana na kifungu cha 72(3)(e) cha sheria ya ajira na mahusiano kazini Na. 6/2004.

4.Mapato yatokanayo na vitega uchumi vya chama mfano Mwalimu house na ofisi za CWT kila mkoa (rent), havimnufaishi mwalimu ambaye ni mchangiaji mkuu.

5.CWT wanakusanya michango kwa wanachama kila mwezi badala ya kukusanya mara moja kwa mwaka kama vyama vingine.

6.Walimu wanaokatwa asilimia 2% Wanakadiriwa kuwa zaidi ya 200,000,CWT wenyewe hawana idadi kamili,hivyo wanakusanya zaidi ya BILIONI 3 kila mwezi. Pamoja na fedha yote hiyo Kuna tetesi kuwa wamekopa shilingi bilioni saba mwaka huu.... Hizo fedha walizokopa Ni za nini?

7.Kwanini kuna tofauti katika makato ya kuchangia mfuko wa C.W.T wakati huduma ni sawa? Kuna nini kinachoongezeka kwa anayekatwa zaidi na nini kinachopungua kwa anayekatwa chini?

8. CWT wanafanya biashara ya Majengo kupitia kampuni ya TEACHERS DEVELOPMENT COMPANY LTD.Lengo kuu la CWT ni kutetea maslahi ya Mwalimu (mwanachama wake) na si biashara maana hata sheria inakataza chama cha wafanyakazi kufanya biashara. Nani aliwaruhusu kufanya biashara?

9. Ile Bank ya waalimu iliyoanzishwa toka 2015 na waalimu kupewa hisa za elfu hamsini Nani aliwahi kupata gawio la hisa zile?

10. Sheria ya Ajira na mahusiano Kazini inataka vyama vyote vya wafanyakazi wasikatwe mishahara yao bila kuridhia au kwa kutumia asilimia. Kwa Nini CWT imekiuka haya yote na hawashitakiwi Wala kuhojiwa?

11. Ni kwa Nini mishahara ya watendaji haipo wazi kwa wanachama? Je watendaji wapo wangapi? Maana kila ukiulizia fedha utaambiwa inatumika kulipa watumishi.

Tujikumbushe nyuma kidogo

Tarehe 27/3/2017 Katibu mkuu kiongozi alimuomba CAG afanye ukaguzi kwenye chama cha Waalimu CWT. Ukaguzi huo ulijikita katika tuhuma dhidi ya Uongozi wa chama cha waalimu zinazohusu ubadhirifu wa fedha na mali za chama.

Ukaguzi maalumu ulikagua taarifa za mapato na matumizi ya Chama, Uliangalia uhusiano uliopo kati ya Benki ya waalimu na waalimu wenyewe, uhusiano uliopo kati ya Mwalimu house na mwalimu mwenyewe.

YALIYOBAINIKA BAADA YA UKAGUZI HUO NI HAYA

1.Hakuna mfumo mzuri wa wanachama unaoonyesha kumbukumbu za wanachama. Katiba ya CWT inaeleza kuwa kunatakiwa kuwe na aina nne za wanachama lakini CWT hawaonyeshi aina hizo za wanachama hivyo haijulikani CWT ina wanachama wangapi.
Pia katika swala la wanachama hakuna taarifa zinazoonyesha wanachama walijiunga lini, mishahara yao kwa mwezi, namba ya uanachama, kiwango anachochangia kwa mwezi nk. Jambo hili CAG anasema kuna uwezekano kuna fedha nyingi zinaliwa kutokana na kutokuwepo kwa taarifa hizo.

2.Malipo ya shilingi 11,924,250,620.13 yakifanyika bila viambatanisho vyovyote. Hii ina maana hakuna nyaraka zinazoonyesha matumizi sahihi ya fedha hizo.

3. Shilingi 3,287,708,358 zilipwa bila kuidhinishwa na katibu mkuu au mweka hazina wa Chama na pia hakuna viambatanisho.

4. Shilingi 11,924,250,620.13 zililipwa bila kuzingatia makisio. Hii ina maana fedha hizi zilitumika bila kuzingatia bajeti ya CWT.CAG anasema viongozi wanakosa nidhamu ya matumizi ya fedha hivyo kuna fedha hapa zilitumika bila wanachama kujua zimekwenda wapi.

5. Hakuna nyaraka zinazoonyesha umiliki wa moja kwa moja wa CWT na miradi yake.

6. Hakuna nyaraka zinazoonyesha mtiririko wa mapato wa vitega uchumi vya chama toka CWT kianzishwe.

7.Mwalimu House imesajiliwa Brela kwa jina lingine la Teachers Development kupitia usajili wa Brela 45719 Badala ya TDCL. Na CAG amebaini kuwa kampuni hilo la Teachers Development halijawahi kufanya kazi toka kuanzishwa kwake. Kwa hiyo mapato yake hayaonekani.

Mbali na ukaguzi wa CAG, mnamo tarehe 14/3/2019 pia msajili wa vyama vya wafanyakazi nchini aliwaandikia CWT barua akitaka wajibu hoja zaidi ya kumi za ubadhirifu wa mali za chama hicho. Barua hiyo yenye kumbukumbu na. RTU/CWT/VOL.IV/12/89 iliwataka kwa haraka sana CWT kujibu hoja za ubadhirifu huo wa mali za chama ambazo zilikuwa zinalalamikiwa na baraza la wadhamini lakini mpaka leo hawajajibu na wala hakuna hatua zozote msajili alizochukua hadi sasa.

itaendelea.....

credited : Thadei ole mushi.
Viongozi wapya wa cwt ni matarajio yetu mtaenda kutatua haya madudu yanayo kikabili chama chenu
 
Back
Top Bottom