Madudu mengine ya William Mhando wa TANESCO!

Status
Not open for further replies.
umeongea kidoogo sana
hebu jaza thread aisee

Hapana ndugu yangu, mengi yashasemwa tayari, nime edit kidogo kumwomba mzee Mhando anywe chai apishe uchunguzi uendelee kama hana kosa la kujibu atarudi tu....
 
Hapana ndugu yangu, mengi yashasemwa tayari, nime edit kidogo kumwomba mzee Mhando anywe chai apishe uchunguzi uendelee kama hana kosa la kujibu atarudi tu....

hii imani kuwa atarudi naona imetawala sana
najiuliza why..?
 
nami nina the same swali,

hiyo kampuni kama imefuata taratibu zote na imeshindanishwa kama sheria za manunuzi zinavyotaka mimi sion ubaya wowote wa mhando.

ebu mleta mada na wachangiaji wenzagu mnifafanulie hili suala.

Tatizo hapa kuna conflict of interest. Mhando hawezi kuwa na kampuni ya familia yake inashindania zabuni katika kampuni ya umma anayoiongoza halafu tukasema "kampuni imefuata taratibu zote na imeshindanisha kama sheria za manunuzi zinavyotaka".
 
Azimio La Zanzibar limetoa ruksa na mwanya kwa viongozi kufanya biashara.. hakuna kosa hata kama shirika hilo lingekuwa kla Mhando mwenyewe maadam amefuata masharti ya Tanesco. Na ndio maana Mkapa alifungua ofisi yake Ikulu kabisaaa isiwe taabu.. Hadi siku mtakapo badilisha sheria hizi sidhani kaa tunayokesi ya kujibu..

Na mgogoro huu siku zote nasema Tanesco mnawaonea sana tu kwa sababu kama hivi. Bajeti mwapangie nyie wizara na sio Tanesco wenyewe kutengeneza, madeni hamtaki kulipia, umeme hamtaki kulipia ofisi zote za serikali nchini na sasa Zanzibar wamegoma nao kulipa halafu mnategemea Tanesco watakuwa na viongozi genius ambao wataweza kuliokoa shirika mnalolinyonya wenyewe.

Ni nyie mloingia mkataba wa IPTL ambao Tanesco leo wana matumizi zaidi ya mapato! Kuna mashirka mengine yalikuwa ya dharura tu copntarct za miaka miwili waondoke wakati tunajiandaa kuzalisha umeme wa uhakika,hakuna kitu wote wanavuta mabillioni toka Tanesco wakisingizia mafuta ghali kuliko gas tuwaletee nayo..

Hii ni mitambo yao sii ya Tanesco kwa nini tuvute gas kuendesha mitambo ya haya mashirika ya dharura badala ya kujenga mitambo yetu na kuikabidhi tanesco ili kujiondoa ktk mikataba mibovu ya IPTL na meingineyo iliyokuwa ya dharura?. Hivi kweli tunavuta gas kutoka Songo na Mtwara ili ku feed mitambo ya hawa jamaa wanaotumaliza kila siku na bei za ajabu halafu mnasema Tanesco ndio wapiga ma deal. Nani atakayelipia gharama za ujenzi wa bomba hilo kama sio Tanesco na wananchi hayo mashirika hayatalipa hata senti maana yapo kwa dharura tu miaka inaondoka. Kina nani waloyachugua haya mashirika yanayozalisha umeme kwa mafuta?.
 
Mhando anahujumiwa na vigogo wizarani ilo lipo wazi..na hii stor imeletwa na wahusika jamaa alikuwa anasimamia haki na ukweli apa tanesco dat y anapgwa vta.

Risasi vitani humpata aliye mbele ya mtutu......naye kakaa upande huho huo

So hata kama alikuwa anasimamia haki kwa kupiga mstri chini ya majina saa mbili kasorobo asubuhi huku tenda zikiwa za mchongo huu......bado man kazi ya kutuelewesha vinginevyo
 
Tatizo hapa kuna conflict of interest. Mhando hawezi kuwa na kampuni ya familia yake inashindania zabuni katika kampuni ya umma anayoiongoza halafu tukasema "kampuni imefuata taratibu zote na imeshindanisha kama sheria za manunuzi zinavyotaka".
Kiranga ktk sheria hakuna kosa la Conflic of interest, linaweza kuwa tatizo lakini sio kosa. Viongozi wote wanatumia nyadhifa zao kuendesha biashara kupitia watoto, wake, ndugu namarafiki maadam hawaibi..
Hii ndio Bongo yetu karibu sana!.
 
Kwa maelezo ya magazeti yetu ni vema unaposoma ujitahidi kukaa jirani na maziwa maana sumu ni nyingi unaweza kupandisha presha. na pili sioni kwa nini unamchukuliaa kuwa ni mhalifu kwa mtazamo wa wajasilimali (magazeti) hebu tumuone kama mtuhumiwa.
 
Kiranga ktk sheria hakuna kosa la Conflic of interest, linaweza kuwa tatizo lakini sio kosa. Viongozi wote wanatumia nyadhifa zao kuendesha biashara kupitia watoto, wake, ndugu namarafiki maadam hawaibi..
Hii ndio Bongo yetu karibu sana!.

Ni busara tu ya kufanya haya unayoyasema sio makosa na ukipungukiwa busara basi ndo conflict hutokea na kuonekana..............so it is upon the one in position to be wise or to figure out and paint the so called conflict of interest
 
mtotowamjini
ku manage tanesco kwanini wasiibinafsishe?

Mkuu! Heshima yako! Kuibinafsisha TANESCO ni kama kumpa huyo mwekezaji bunduki akupige ufe. Uliona wapi nchi za wenzetu wanakabidhi Shirika kama hilo lichezewe na mtu binafsi? Atatamba kama wanavyotamba wauza mafuta na bei atapanga yeye na wauza mafuta. Wakati huo hata JF itakuwa haifanyi kazi. Mi niko Kenya kwa sasa. Wenzetu huku wanalisimamia Kenya Electric Power bila matatizo na hakuna kitu kama mgawo. Na hawana sources za umeme nzuri kama tulivyo nazo sisi. Sema hivi, kama wanashindwa kuimanage TANESCO waachie ngazi! Si wameshindwa?
 
Ni busara tu ya kufanya haya unayoyasema sio makosa na ukipungukiwa busara basi ndo conflict hutokea na kuonekana..............so it is upon the one in position to be wise or to figure out and paint the so called conflict of interest
Lakini mkuu wangu tuseme ukweli Conflict of interest haina busara wala kutokuwa na busara. Hiatakiwi kumpa mnmtu nafasi ya kufanya madudu haya na ndio maana ya kuwepo miiko na maadili ya Uongozi sio kuwa na tume ya maadili.. Sisi Watanzania tunafanya kila kitu kinyume cha busara halafu tunaitafuta busara kweli hiyo busara itapatikana wapi?
 
Mkuu wangu JokaKuu,
Uyasemayo yanaweza kuwa ya kweli lakini ili mradi ni yeye aliyewahiwa kuvikwa shada la miba; basi mie kwa sasa nitakayekazana kumtupia mawe ni huyu huyu kwanza hadi pale nitakaposikia tuhuma zisizo shaka dhidi ya hao wenzake!!

Kuhusu hilo la Katibu Mkuu, hata nami nimelisikia. Hata hivyo, utetezi uliotolewa na Katibu Mkuu huyo nauunga mkono hadi pale itakapothibitishwa vinginevyo!! Kimsingi, inasemekana kwamba; Vigogo wa TANESCO walitoa tenda ya uuzaji mafuta kwa kampuni nyingine kabisa. Lakini kilichokuwa kinafanywa na kampuni hiyo ya walaji wa TANESCO ni kwamba; walikuwa wananunua mafuta mazito toka kampuni ya Puma Energy kisha nao ndo wanakuja kuiuzia TANESCO kwa bei ya juu! Hiyo kampuni ya Puma Energy ilishindwa kwenye mchakato wa kumpata supplier wa hayo mafuta! Sasa alichokifanya Maswi(Katibu Mkuu), ni kuamua kununua mafuta moja kwa moja toka kwa hao Kampuni ya Puma Energy....hivyo basi; kosa la kwanza hapa ambalo labda tunaweza kuliona kwa Maswi; ni kuipa tenda ya ku-supply mafuta kampuni ambayo ilishindwa! Lakini uzuri uliopo ni kwamba; hao Puma Energy hivi sasa wanauza mafuta kwa bei ya chini kuliko ile iliyokuwa inatolewa na kampuni zilizoteuliwa na TANESCO....wanauza bei ya chini kwavile kampuni za akina Mhando zilikuwa zina-act kama middle men wa Puma Energy katika ku-supply mafuta kwa TANESCO! So, hata kama Maswi amefinyanga sheria; kwangu naona ni bora mara 1000 kufinyanga sheria kwa ajili ya maslahi ya taifa(ya wengi) kuliko kufuata sheria in favor of watu wachache! Ni hadi pale Mhando na watu wake watakavyothibitisha kwamba Maswi ana maslahi binafsi kutokana na hatua yake ya kuipa tenda Puma inayoiuzia TANESCO mafuta kwa bei ndogo; vinginevyo bado kwangu nitaona kitendo alichofanya kina maslahi kwa taifa!
 
Kiranga ktk sheria hakuna kosa la Conflic of interest, linaweza kuwa tatizo lakini sio kosa. Viongozi wote wanatumia nyadhifa zao kuendesha biashara kupitia watoto, wake, ndugu namarafiki maadam hawaibi..
Hii ndio Bongo yetu karibu sana!.

Angalia "The Public Procurement Act, 2004" 37 (6) halafu utuambie kama Mhando ali declare conflict of interest according to this law.

Sheria imesema wazi, sielewi unaposema "hakuna kosa la conflict of interest" una maana gani.
 
Mbona hajajibu lolote kuhusu majina ya wanaye kuhusishwa na hiyo kampuni ya mkewe???? Sintofahamu kwa kwenda mbele!!!!
 
Angalia "The Public Procurement Act, 2004" 37 (6) halafu utuambie kama Mhando ali declare conflict of interest according to this law.

Sheria imesema wazi, sielewi unaposema "hakuna kosa la conflict of interest" una maana gani.
Kwangu haifunguki sijui kwa nini?..Kwani inasemaje hiyo 37 (6)
 
Kiranga ktk sheria hakuna kosa la Conflic of interest, linaweza kuwa tatizo lakini sio kosa. Viongozi wote wanatumia nyadhifa zao kuendesha biashara kupitia watoto, wake, ndugu namarafiki maadam hawaibi..
Hii ndio Bongo yetu karibu sana!.

Mkuu Mkandara,
Naona umewaka sana hili Mhando lina tofauti gani na mwenyekiti Mbowe alipojipa tenda ya zaidi mil.300?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
1. Umesoma utetezi wake kaka?????
2. Umeona composition ya directors wa hiyo santa director's family and supplies????
3. Umeona muajiri wa mke wa director na rationale ya ajira??????

"........Sisi Watanzania tunafanya kila kitu kinyume cha busara halafu tunaitafuta busara kweli hiyo
busara itapatikana wapi?..........."
(Mkandara; 2012)
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…