Madudu mengine ya William Mhando wa TANESCO!

Status
Not open for further replies.
NasDaz

Hahahaaaaaaaa! Utetezi wke hun tofauti n ule wa Maige! Loooooooooh, CCM acha kabisa ni joka kuu!
 
Last edited by a moderator:
Na ilimradi tayari mwenyewe anaifahamu hiyo kampuni na kwavile ameshakiri kwamba ni ya mke wake; na kwavile ni very simple kama kufumba na kufumbua kuthibitisha kwamba Veronica na Fred ni watoto wake;

Na kwavile kuna kila dalili kwamba usajili wa kampuni ulilenga kuficha kwamba Wakurugenzi ni watoto wa Mhando(na ndio maana walitumia majina mawili tu; wakaacha ubini wa Mhando---atueleze WHY kwanini alitaka kuficha); basi hayo tu peke yake yanatosha kabisa kumfikisha Mhando Mahakamani kwa kosa hilo hilo wakati tunasubiria aongezewe mashitaka kutokana na tuhuma zingine zilizosababisha yeye kusimamishwa kazi. Bahati mzuri amekiri kwamba wakati anateuliwa kuwa MD, aliandikiwa barua na wizara kwamba mke wake aondolewe TANESCO ili kuepuka mgongano wa kimaslahi! Waungwana husema "kuepusha mgongano wa kimaslahi"

Lakini kuepusha mgongano wa kimaslahi Kimsingi ni kepusha "Technical Corruption".....hii ilitosha kabisa kumuonesha ubaya wa mgongano wa kimaslahi....lakini pamoja na hayo akaamua kufanya Technical Corruption!!
 
Zitto, mama Malecela na wote wanaomtetea huyu mtu mwizi wanajiaibisha sana. Huyu si tu wa kusimamishwa afukuzwe mara moja.

Zitto hafai na hili la yeye kutetea ufisadi wa Tanesco litamtokea puani mwaka huu maana watu wameshamfutailia anavyonuka rushwa.

Wana JF,

" Mpiga Zumari ndiye huchagua wimbo" Huo ni msemo nimeiga kutoka lugha ya Kiingereza sijui Kama nimepatia. Zito Kabwe na January Makamba walioteuliwa kwenye hizo kamati za Bunge kwa mapendekezo ya Rostam Aziz. Wajumbe wengi huwa wanalipwa pesa nyingi sana ili kuhakikisha maslahi ya wanowalipa yanatimizwa at any cost!

Kwa kupitia Mkurugenzi Tanesco aliyesimamishwa kazi , Kampuni za Rostam Aziz Symbion na Aggreko zimejipatia zabuni za kufua umeme kwa bei ya juu kuliko sehemu yoyote hapa Duniani.

Kwa hiyo kuondoka kwa Mhando kutawezesha kujulikana kwa Ufisadi huo wa Kutisha. Bei waliokubaliana kwenye Mkataba ya kuuza umeme kwa Senti za kimarekani 46 (USD 0.46) kwa Kilowatt moja sawa na Tshs. 700, ndiyo bei ya juu kuliko zote hapa duniani .Mwenye kuweza kuonyesha nchi inayonunua umeme kwa bei ya Tshs. 700 na kuuza kwa bei ya wastani ya Tshs 221 kwa unit moja na bado ikabakia inafanya huo utani atuhabarishe sisi wajinga! Lakini Bodi ipo na Zabuni ilifanyika katika mazingira yenye utata mkubwa na kuridhiwa halafu hata Hilary Clinton akasifia huo upuuzi? Basi kuna tatizo kubwa zaidi ya tunaloliona.

Tatizo ambalo liko wazi ni kwamba huo mkopo walikuwa wanapigania akina Zito na wenzake it's part of the clandestine project ya kuiua Tanesco kin pin akiwa na Rostam.

Bila kutafuna maneno tanesco ilikopa Tshs 300bn chini ya Syndicate loan Enzi za Dr. Idris na linakula RIBA ya 15%. Kulipa Hilo deni ni shughuli pevu. Kwa kuwa Tshs.408Bn wnazoshupalia akina zito na Wapambe kibao zitakuwa ni deni la Taifa Kama Hilo la Dr. idris . Vita hii ni ya kutaka kuendelea kuiba na hatimaye kuua hilo shirika at the expense of poor Tax payers.

Kitendo cha kujipatia zabuni Kampuni ya Mke wake ni cha kulaaniwa je kwa muda miaka miwili ya uongozi wa Mhando ni madudu mangapi ameyafanya kupitia hizo Kampuni marafiki zake. Yamkini anao washiriki wengi sana waliokuwa wakimsaidia kufanya huo uzandiki ndani na nje ya Kampuni . Panatakiwa fagio la chuma lipite kwenye Hilo shirika what we have seen is only the tip of the iceberg. CAG should do complete audit . What worries me that company has a Chief Internal Auditor are they on leave. It implies hakuna Board ya Wakurugenzi?
 
Na ilimradi tayari mwenyewe anaifahamu hiyo kampuni na kwavile ameshakiri kwamba ni ya mke wake; na kwavile ni very simple kama kufumba na kufumbua kuthibitisha kwamba Veronica na Fred ni watoto wake;

Na kwavile kuna kila dalili kwamba usajili wa kampuni ulilenga kuficha kwamba Wakurugenzi ni watoto wa Mhando(na ndio maana walitumia majina mawili tu; wakaacha ubini wa Mhando---atueleze WHY kwanini alitaka kuficha); basi hayo tu peke yake yanatosha kabisa kumfikisha Mhando Mahakamani kwa kosa hilo hilo wakati tunasubiria aongezewe mashitaka kutokana na tuhuma zingine zilizosababisha yeye kusimamishwa kazi. Bahati mzuri amekiri kwamba wakati anateuliwa kuwa MD, aliandikiwa barua na wizara kwamba mke wake aondolewe TANESCO ili kuepuka mgongano wa kimaslahi! Waungwana husema "kuepusha mgongano wa kimaslahi"

Lakini kuepusha mgongano wa kimaslahi Kimsingi ni kepusha "Technical Corruption".....hii ilitosha kabisa kumuonesha ubaya wa mgongano wa kimaslahi....lakini pamoja na hayo akaamua kufanya Technical Corruption!!

NasDaz,

..nadhani huyu jamaa kawanyima wenzake ulaji ndiyo maana yote haya yanaibuka.

..kuna mahali nimesoma kwamba Katibu Mkuu Nishati naye ana "watu wake" ambao wana-supply mafuta mazito Tanesco.

..ninachoona sasa hivi ni juhudi za kulipuana tu kati ya Wizara na Tanesco. Sioni mahali popote ambapo wahusika wamejielekeza kutatua tatizo la MGAO WA UMEME ambao umedumu toka miaka ya 90.
 
Mkuu Mokerema.
Sent 46 za dola ya kimarekani (0.46 USD/Kw) ikiwa sawa na Tsh 700/Kw,
Je kuna unit ngapi katika Kilo watt moja?
Ili nipate kujua wanatengeneza faida ya shilingi ngapi wakishauza huo umeme kwa mtumiaji.
 
Mhando anahujumiwa na vigogo wizarani ilo lipo wazi..na hii stor imeletwa na wahusika jamaa alikuwa anasimamia haki na ukweli apa tanesco dat y anapgwa vta.
 
Yaani amejaribu kujificha lakini hafichiki. Kuna kitu sijaelewa sasa hiyo kampuni imeanzishwa 2011 na mkewe aliacha ukurugenzi lini na tenda ya tanesko walipata lini
 
Yaani amejaribu kujificha lakini hafichiki. Kuna kitu sijaelewa sasa hiyo kampuni imeanzishwa 2011 na mkewe aliacha ukurugenzi lini na tenda ya tanesko walipata lini

na watoto ni wakurugenzi lol
 
Mke wa Mhando supplier wa Tanesco, serikali mtumiaji umeme bila kulipa. Hapa kweli kuna maendeleo zaidi ya kuwa ujambazi kwenda mbele tena mchana?
 
Wakati Wizara ya Nishati na Madini ikitarajiwa kuwasilisha bajeti yake kwa mwaka wa Fedha 2012/2013, mvutano miongoni mwa wabunge umezidi kutanuka kiasi cha kuhatarisha mjadala wa bajeti ya wizara hiyo.

Lakini wakati hali hiyo ya mvutano ikibainika miongoni mwa wabunge, kile kinachoelezwa kuwa ni mvutano kati ya viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini kwa upande mmoja na viongozi wa TANESCO waliosimamishwa umechukuwa sura mpya, ikielezwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO (aliyesimamishwa), William Mhando, ana maslahi katika zabuni ya kusambaza vifaa vya ofisi ya kampuni ya mkewe, Eva Mhando inayoitwa Santa Clara Supplies Co. Ltd.

Kampuni hiyo ya Santa Clara Supplies Limited inadaiwa kupewa mkataba wa Sh.884,550,000 na TANESCO kwa ajili ya kusambaza vifaa hivyo.

Lakini akizungumza ofisini kwa Raia Mweam jana Jumanne, Mhando alikiri kuitambua kampuni hiyo si mali ya familia yake bali mkewe, Eva ambaye awali alikuwa akifanya kazi TANESCO ndiye ameajiriwa na kampuni hiyo.

KAMPUNI KUPEWA ZABUNI:

Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa Mhando, akiwa Mkurugenzi wa TANESCO, bila kujali mgingano wa kimaslahi aliacha mchakato wa kuipa zabuni kampuni hiyo uendelee na hatimaye kampuni hiyo ikashinda zabuni hiyo ya kusambaza vifaa vya ofisi kwa TANESCO.

Mhando anadaiwa kuipa kampuni hiyo iliyosajiliwa April 04, 2011, taarifa zaidi zikieleza kuwa, kampuni hiyo ilianza na mataji wa Sh. Miliomi kumi na wanahisa wake ni Fred Willliam, Veronica William na Steven William na kwa mujibu wa usajili wa kampuni hiyo, wanahisa hao pia ni makaimu wakurugenzi.

Maelezo ya usajili wa kampuni hiyo ya Santa Clara Supplies Co. Ltd, ambayo Raia Mwema imefanikiwa kuyaona, yanaonyesha kuwa ipo katika kitalu namba 204, Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam.

Kwenye orodha ya wanahisa na makaimu wakurugenzi wa kampuni hiyo majina ya Fred na Veronica, yamebainika kuwa ni watoto wa Mhando.

MAJIBU YA MHANDO.

Katika kufafanua kuhusu suala hilo, Mhando alisema wakati akiwa TANESCO katika ngazi za chini alikuwa akifanya kazi katika shirika hiloo na mkewe, Eva.

Hata hivyo kwa mujibu wa maelezo yake, mara baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo pekee la kusambaza umeme nchini, Wizara ya Nishati na Madini, ilimwandikia barua ya kutaka mkewe aachishwe kazi ili kuepusha uwezekano wa kuwapo kwa mgongano wa kimaslahi.

“Mke wangu aliacha kazi, lakini tulikuwa na kampuni hiyo ya stationery Kariakoo na kwa sababu biashara haikuwa nzuri kutokana na uwezo mdogo wa kifedha, tuliuza kampuni hiyo mwaka jana.

Mke wangu aliajiriwa tu katika kampuni hiyo baada ya kununuliwa ili waweze kutumia uzoefu wake katika kuiendesha.

“Sasa kwa nafasi ya mke wangu, yeye ni Mtendaji wa hiyo kampuni lakini shughuli zote za kutafuta shughuli zote za kutafuta zabuni zinafanywa na wakurugenzi wa kampuni hiyo, si mke wangu.

“Kwahiyo, walipoomba kazi TANESCO hatua zote zilifanyika kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sharia na kampuni hiyo ilishandanishwa na kampuni nyingine na hatimaye ikashinda,” alisema Mhando.

NB: KWA MAELEZO ZAIDI, UKITAKA KUFAHAMU SINTOFAHAMU YA BUNGE NA SAKATA LA MHANDO, SOMA SOURCE YA HABARI HII-GAZETI LA RAIA MWEMA, July 25,2012.

MY TAKE:
Wale wanaomtetea Fisadi Chipukizi William Mhando, jaribuni kutetea na uozo huu....!!
Mimi si miongoni mwa watetezi wa Bwana huyu
 
Zitto na wenzake kwenye POAC wanaangalia ripoti za CAG tu. Madudu ndani ya mashirika ya UMMA hawayajui. Ndio maana hata uozo ndani ya Bodi ya Korosho ambayo mwenyekiti wake ni mbunge mwenzao wameshindwa pa kuanzia!

Speaking of bodi ya korosho wameacha nyumba zao zinaoza Oysterbay prime area, prime properties. Yaani ukiangalia tu unaona kielelezo cha uozo katika bodi hii.

Humu kwenye mashirika ya umma kuna uozo wa ajabu sana.
 
Mhando anahujumiwa na vigogo wizarani ilo lipo wazi..na hii stor imeletwa na wahusika jamaa alikuwa anasimamia haki na ukweli apa tanesco dat y anapgwa vta.

Hata kama anapigwa vita, swali je ni ya kweli? Huu uozo utaisha lini jamani? Embu waoneeni huruma watoto wa wakulima wanavyokosa mikopo japo ya kusoma hata digirii moja huku nyie mkijilimbikizia mijidola na kuwaweka watoto wenu eti ndo wakurugenzi wa hizo kampuni
 
Wana JF,

" Mpiga Zumari ndiye huchagua wimbo" Huo ni msemo nimeiga kutoka lugha ya Kiingereza sijui Kama nimepatia. Zito Kabwe na January Makamba walioteuliwa kwenye hizo kamati za Bunge kwa mapendekezo ya Rostam Aziz. Wajumbe wengi huwa wanalipwa pesa nyingi sana ili kuhakikisha maslahi ya wanowalipa yanatimizwa at any cost!

Kwa kupitia Mkurugenzi Tanesco aliyesimamishwa kazi , Kampuni za Rostam Aziz Symbion na Aggreko zimejipatia zabuni za kufua umeme kwa bei ya juu kuliko sehemu yoyote hapa Duniani.

Kwa hiyo kuondoka kwa Mhando kutawezesha kujulikana kwa Ufisadi huo wa Kutisha. Bei waliokubaliana kwenye Mkataba ya kuuza umeme kwa Senti za kimarekani 46 (USD 0.46) kwa Kilowatt moja sawa na Tshs. 700, ndiyo bei ya juu kuliko zote hapa duniani .Mwenye kuweza kuonyesha nchi inayonunua umeme kwa bei ya Tshs. 700 na kuuza kwa bei ya wastani ya Tshs 221 kwa unit moja na bado ikabakia inafanya huo utani atuhabarishe sisi wajinga! Lakini Bodi ipo na Zabuni ilifanyika katika mazingira yenye utata mkubwa na kuridhiwa halafu hata Hilary Clinton akasifia huo upuuzi? Basi kuna tatizo kubwa zaidi ya tunaloliona.

Tatizo ambalo liko wazi ni kwamba huo mkopo walikuwa wanapigania akina Zito na wenzake it's part of the clandestine project ya kuiua Tanesco kin pin akiwa na Rostam.

Bila kutafuna maneno tanesco ilikopa Tshs 300bn chini ya Syndicate loan Enzi za Dr. Idris na linakula RIBA ya 15%. Kulipa Hilo deni ni shughuli pevu. Kwa kuwa Tshs.408Bn wnazoshupalia akina zito na Wapambe kibao zitakuwa ni deni la Taifa Kama Hilo la Dr. idris . Vita hii ni ya kutaka kuendelea kuiba na hatimaye kuua hilo shirika at the expense of poor Tax payers.

Kitendo cha kujipatia zabuni Kampuni ya Mke wake ni cha kulaaniwa je kwa muda miaka miwili ya uongozi wa Mhando ni madudu mangapi ameyafanya kupitia hizo Kampuni marafiki zake. Yamkini anao washiriki wengi sana waliokuwa wakimsaidia kufanya huo uzandiki ndani na nje ya Kampuni . Panatakiwa fagio la chuma lipite kwenye Hilo shirika what we have seen is only the tip of the iceberg. CAG should do complete audit . What worries me that company has a Chief Internal Auditor are they on leave. It implies hakuna Board ya Wakurugenzi?

You have said well and very clear. He has to go.
 
Mhando anahujumiwa na vigogo wizarani ilo lipo wazi..na hii stor imeletwa na wahusika jamaa alikuwa anasimamia haki na ukweli apa tanesco dat y anapgwa vta.

Haki gani unayoisema kiumbe wewe? Ni ile ya kuinyima kampuni ya Kitanzania inayozalisha vifaa vya umeme mjini Arusha na kuipa kampuni ya Yusuf Manji iliyotoa bei takribani mara mia zaidi ya ile ya Kitanzania? Baada ya kubanwa Mhando akaomba wayamalize mambo nje ya taratibu za sheria? Hii ndio HAKI unayoisema? Usituchefue hapa, mwambieni kuwa wakati wa kuondoka umefika, madudu aliyokuwa anayafanya sasa yanawekwa wazi.
 
Maswi is protecting tax payer's money by awarding tender to ex BP ambao govt tuna shares na kuokoa 3bn tax payer's money,pesa zenyewe zimetoka wizarani so he might as well have an interest on its usage.

Ninashauri kitengo cha tender cha TANESCO kifumuliwe na kuangaliwa upya....ushauri wa PPRA uzingatiwe.

Kisha Eng Mhando nakushauri utulie kama NBC MD upishe uchunguzi, binafsi ningekuwa nalima shamba langu naendelea na mambo yangu
 
Maswi is protecting tax payer's money by awarding tender to ex BP ambao govt tuna shares na kuokoa 3bn tax payer's money,pesa zenyewe zimetoka wizarani so he might as well have an interest on its usage.

Ninashauri kitengo cha tender kifumuliwe na kuangaliwa upya....ushauri wa PPRA uzingatiwe.

umeongea kidoogo sana
hebu jaza thread aisee
 
Maswi is protecting tax payer's money by awarding tender to ex BP ambao govt tuna shares na kuokoa 3bn tax payer's money,pesa zenyewe zimetoka wizarani so he might as well have an interest on its usage.

Ninashauri kitengo cha tender kifumuliwe na kuangaliwa upya....ushauri wa PPRA uzingatiwe.

You are very right, some people use loopholes in our sheria to "**** up" this nchi. Maswi is right in this matter.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom