Madudu mengine ya William Mhando wa TANESCO! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madudu mengine ya William Mhando wa TANESCO!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NasDaz, Jul 25, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Wakati Wizara ya Nishati na Madini ikitarajiwa kuwasilisha bajeti yake kwa mwaka wa Fedha 2012/2013, mvutano miongoni mwa wabunge umezidi kutanuka kiasi cha kuhatarisha mjadala wa bajeti ya wizara hiyo.

  Lakini wakati hali hiyo ya mvutano ikibainika miongoni mwa wabunge, kile kinachoelezwa kuwa ni mvutano kati ya viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini kwa upande mmoja na viongozi wa TANESCO waliosimamishwa umechukuwa sura mpya, ikielezwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO (aliyesimamishwa), William Mhando, ana maslahi katika zabuni ya kusambaza vifaa vya ofisi ya kampuni ya mkewe, Eva Mhando inayoitwa Santa Clara Supplies Co. Ltd.

  Kampuni hiyo ya Santa Clara Supplies Limited inadaiwa kupewa mkataba wa Sh.884,550,000 na TANESCO kwa ajili ya kusambaza vifaa hivyo.

  Lakini akizungumza ofisini kwa Raia Mweam jana Jumanne, Mhando alikiri kuitambua kampuni hiyo si mali ya familia yake bali mkewe, Eva ambaye awali alikuwa akifanya kazi TANESCO ndiye ameajiriwa na kampuni hiyo.

  KAMPUNI KUPEWA ZABUNI:

  Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa Mhando, akiwa Mkurugenzi wa TANESCO, bila kujali mgingano wa kimaslahi aliacha mchakato wa kuipa zabuni kampuni hiyo uendelee na hatimaye kampuni hiyo ikashinda zabuni hiyo ya kusambaza vifaa vya ofisi kwa TANESCO.

  Mhando anadaiwa kuipa kampuni hiyo iliyosajiliwa April 04, 2011, taarifa zaidi zikieleza kuwa, kampuni hiyo ilianza na mataji wa Sh. Miliomi kumi na wanahisa wake ni Fred Willliam, Veronica William na Steven William na kwa mujibu wa usajili wa kampuni hiyo, wanahisa hao pia ni makaimu wakurugenzi.

  Maelezo ya usajili wa kampuni hiyo ya Santa Clara Supplies Co. Ltd, ambayo Raia Mwema imefanikiwa kuyaona, yanaonyesha kuwa ipo katika kitalu namba 204, Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam.

  Kwenye orodha ya wanahisa na makaimu wakurugenzi wa kampuni hiyo majina ya Fred na Veronica, yamebainika kuwa ni watoto wa Mhando.

  MAJIBU YA MHANDO.

  Katika kufafanua kuhusu suala hilo, Mhando alisema wakati akiwa TANESCO katika ngazi za chini alikuwa akifanya kazi katika shirika hiloo na mkewe, Eva.

  Hata hivyo kwa mujibu wa maelezo yake, mara baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo pekee la kusambaza umeme nchini, Wizara ya Nishati na Madini, ilimwandikia barua ya kutaka mkewe aachishwe kazi ili kuepusha uwezekano wa kuwapo kwa mgongano wa kimaslahi.

  "Mke wangu aliacha kazi, lakini tulikuwa na kampuni hiyo ya stationery Kariakoo na kwa sababu biashara haikuwa nzuri kutokana na uwezo mdogo wa kifedha, tuliuza kampuni hiyo mwaka jana.

  Mke wangu aliajiriwa tu katika kampuni hiyo baada ya kununuliwa ili waweze kutumia uzoefu wake katika kuiendesha.

  "Sasa kwa nafasi ya mke wangu, yeye ni Mtendaji wa hiyo kampuni lakini shughuli zote za kutafuta shughuli zote za kutafuta zabuni zinafanywa na wakurugenzi wa kampuni hiyo, si mke wangu.

  "Kwahiyo, walipoomba kazi TANESCO hatua zote zilifanyika kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sharia na kampuni hiyo ilishandanishwa na kampuni nyingine na hatimaye ikashinda," alisema Mhando.


  NB: KWA MAELEZO ZAIDI, UKITAKA KUFAHAMU SINTOFAHAMU YA BUNGE NA SAKATA LA MHANDO, SOMA SOURCE YA HABARI HII-GAZETI LA RAIA MWEMA, July 25,2012.

  MY TAKE:
  Wale wanaomtetea Fisadi Chipukizi William Mhando, jaribuni kutetea na uozo huu....!!
   
 2. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Kwa nini wezi/wabadhirifu/mafisadi nchini wengi wao wanatoka jamii moja? kuna nini huko katika hii jamii?
   
 3. W

  WildCard JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Zitto na wenzake kwenye POAC wanaangalia ripoti za CAG tu. Madudu ndani ya mashirika ya UMMA hawayajui. Ndio maana hata uozo ndani ya Bodi ya Korosho ambayo mwenyekiti wake ni mbunge mwenzao wameshindwa pa kuanzia!
   
 4. U

  Uswe JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  duh hapa hatoki!
   
 5. Advocate J

  Advocate J JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 3,880
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  shirika la tanesco matatizo matupu ,madeni inayodaiwa bdo na ufisadi kama huu mtalifilisi ohoo alaf gvt ibebe mzigo ten
   
 6. I

  IDIOS Member

  #6
  Jul 25, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Jamani kila siku afadhali ya jana
   
 7. Ndukidi

  Ndukidi JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 821
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  Aisee, hii wala hachomoi.. haya Mwanahalisi, Zito msafisheni tena hapa!! hivi kumbe jamaa ni mbaya hivi?
   
 8. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kama sikosei huyu mshkaji aliteuliwa na mkulu na ikazua mjadala kwa kuwa ni washkaji.

  Sitaki kwenda mpali ila ninapatwa na mashaka sana ni hizi teuzi na hasa hawa warembo kwenye mashirika yetu. SSRA, NSSF pale na viti maalumu na kadhalika.

  Mnyonge ananyongwa na haki anakosa
   
 9. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,116
  Likes Received: 351
  Trophy Points: 180
  haki utaipata ahera mpwa kama unaweza ingia barabarani tuiue ssra
   
 10. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Teuzi zote za Kikwete ni za kishkaji na kwa maslahi fulani binafsi.

  Ndio maana tunataka Katiba Mpya, itakayopatikana ktk mchakato na mazingira huru na haki. Rais hawezi kuwa na akili ndogo namna hii halafu atutie hasara kila kukicha nasi tukanyamaza. So it begin with Kikwete downwards.
   
 11. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 180
  Sisi tulishajua UDHAIFU wa kamati ya Zitto, kuna vitu wanajaribu kutetea lakini they are real unprofessional, haiwezekani leo mtumishi kasimamishwa halafu POAC wakuja na hoja nyepesi eti hawajaridhishwa na mchakato wa kumsimamisha mhando, this is outright ridiculous.Mh zitto naamini ata turn around to the original status he used to be ,other wise he gonna let down himself
   
 12. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,645
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo aisee... ndio maana mabarabarani watu wanasukuma ndinga za hundred millions na wana mahekalu ya billions mpaka mtu unajiuliza wenzetu hela wanazipata wapi kumbe au wenyewe wamependelewa sana na sir god?
   
 13. Z

  Zimamoto JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 464
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Tumezidi mno kusubiri 'kujiridhisha', ndio tuchukue hatua. Staili ya akina Mrema na Lowassa inatakiwa kwa kizazi kama hiki kilichojaa ufisadi.
   
 14. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  mkuu, ina maana unataka kukubaliana na Mh. Tundu Lissu pamoja na ubishi wake na AG!!!???

   
 15. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  tatizo la hapa bongo tuna shirika moja tu la umeme na ni la serikali so kila mtu anataka kula yake hapo... kama serikali imeshindwa ku manage tanesco kwanini wasiibinafsishe? tatizo la umeme hapa tanzania ni ndogo sana kama ukipata watu wako serious na wanaangalia maslahi ya taifa ni rahisi kusuluhisha..sema ndio hivyo kuna vigogo wengi ndio kula yao hapo
   
 16. P

  Prince Hope JF-Expert Member

  #16
  Jul 25, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 2,167
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kwa hili, hachomoki ng'o!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
   
 17. M

  MVENGEVENGE Senior Member

  #17
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  haya kweli madudu hivi mhando anawafanya watu wote wajinga, wewe uuze kampuni halafu mkewe aajiriwe na kampuni aliyouza, TRA alilipa kodi shs ngapi baada ya kuuza ???
   
 18. H

  Hon.MP Senior Member

  #18
  Jul 25, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zitto, mama Malecela na wote wanaomtetea huyu mtu mwizi wanajiaibisha sana. Huyu si tu wa kusimamishwa afukuzwe mara moja.

  Zitto hafai na hili la yeye kutetea ufisadi wa Tanesco litamtokea puani mwaka huu maana watu wameshamfutailia anavyonuka rushwa.
   
 19. R

  Ramos JF-Expert Member

  #19
  Jul 25, 2012
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kama Zitto alimtetea huyu jamaa... I have a lot to learn...
   
 20. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #20
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kosa la Muhando liko wapi hapo sasa?
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...