MADUDU mengine ya Mali asili na Utalii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MADUDU mengine ya Mali asili na Utalii

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chaimaharage, Apr 29, 2012.

 1. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna taarifa kutoka vyanzo vyetu vilivyo Wizara ya Maliasili na Utalii kuwa ile stock ya meno ya tembo ambayo serikali ilikataliwa kuiuza na shirikisho linalo simamia wanyama walio katika hatari ya kutoweka Duniani(CITES) imeanza kutoweka kinyemela.

  Kilichofanyika awali ni kwamba watumishi wote walipewa amri ya kutokuwa ofisini ifikapo saa moja jioni ambapo ni mwisho wa kuonekana mazingira yale. Kumbuka kuwa kuna wengine ambao wanakuwa wana kazi za kiofisi ambapo huweza kukaa hata saa 2 usiku ili kuweza kuzimaliza kwa wakati.

  Lakini cha ajabu baadhi ya viongozi hasa wa Idara ya wanyamapori wamekuwa wakionekana maeneo ya ofisi hata baada ya saa 2 usiku tofauti na amri waliyowekewa watumishi wa ngazi za chini inayo onekana kuwalenga zaidi wao.

  Sasa mchezo unaofanywa ni kwamba linaingia lori usiku na kuondoka na mzigo. Mtandao wenyewe unaohusika ni mkubwa na siyo kwa viongozi wa Idara hiyo peke yao. Zimefungwa hadi camera kwenye ma-godown yenye meno hayo ili hata kiasi cha mzigo unaoondoshwa kionekane ili katika mgao kusiwepo kuthulumiana. sababu mtu anaweza kusema tumetoa contena moja kumbe ni mawili.

  Kwa kawaida meno ya tembo yanapokamatwa iwe porini kutoka kwa majangiri au kwingineko huwa yana pigwa muhuri maalumu kama utambulisho ili yakitoweka ijulikane. Mihuri yenyewe hupigwa upande wa mwisho wa jino na juu. Na ndivyo askari wote wa wanyamapori wanavyoelekezwa kufanya. Sasa jiulize kwanini hawa ruhusiwi kupiga mihuri hiyo sehemu za katikati ya meno? Hebu ona sababu yenyewe;

  Wanachofanya hawa jamaa wana kata sehemu ya juu ya meno yenye muhuri na ya chini pia. Kwahiyo sehemu yote ya katikati inabaki haina alama yoyote kiasi hata yakikamatwa mbele ya safari isijulikane kuwa yametokea pale kwenye yale maghala.

  Hivyo mwisho wa siku mzigo wote utakwisha na hatujui wa kumkamata ni nani.
   
 2. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #2
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  DUUUUUUU
  kazi kweli kweli
  nahivi baraza la mawaziri ndio laenda kubadirishwa,basi kila mtu anafanya atakalo
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Tunakoelekea hata sijui ni wapi?
   
 4. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #4
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  DUUUUUUU
  kazi kweli kweli
  nahivi baraza la mawaziri ndio laenda kubadirishwa,basi kila mtu anafanya atakalo
   
 5. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  ...ndio shida ya kuweka majangili madarakani.
   
 6. Uda

  Uda JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 730
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kama kashare kanaenda serikalini itakuwa ni mpango wa kiakili sana.lakini kama zinaingia kwa kina maige mh!sina la kuchangia
   
 7. GEMBESON

  GEMBESON JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 256
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Check bob JK Kazi unayo.
   
 8. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nadhani ni wizara zote na siyo hiyo moja sema tu wanabahati habari zao wanafanikiwa kuziminya
   
 9. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,827
  Likes Received: 1,542
  Trophy Points: 280
  Duh! kumbe ndivyo ilivyo, hapa nimechoka kabisa nahisi hii wizara baada ya JK kumaliza muda wake kutakuwa hakuna kilichobaki
   
 10. GOKILI

  GOKILI JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 422
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  madudu hayakuanza leo ktk wizara hiyo na hasa idara ya wanyama pori.mnamshangaa maige kununua nyumba kwa $700 lakh,jiulizeni aliyepata kuwa mkurugenzi wa TAWICO na baadaye kuwa mkurugenzi wa idara ya wanyama pori alipatajepataje ubillionea?!Kwa nyongeza yule jangili mkuu Pano Calvarias anaishi na kuendesha shughuli zake nchini licha ya kuwa hatakiwi na uhamiaji.
   
 11. LESIRIAMU

  LESIRIAMU JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 4,005
  Likes Received: 2,222
  Trophy Points: 280
  Tutafika no sooner
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  please.............. Acha kuwa dumb a$$
   
 13. Olaigwanani lang

  Olaigwanani lang JF-Expert Member

  #13
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 480
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ama kweli chukua chako mapema......!
   
 14. Olaigwanani lang

  Olaigwanani lang JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 480
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  pia nashangaa sana kuna maafisa wengine wapo hapo wizarani wao wenyewe ni majangili ..tayari wana skendo nyingi lakini eti ndo viongozi wa idara ya wanyamapori hata juzi bungeni katajwa....mimi sijui sasa hii inchi yaelekea wapi.....wana JF....!
   
 15. Uda

  Uda JF-Expert Member

  #15
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 730
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  uelewa wako juu ya suala hili ni mdogo ndio maana unaishia kutukana.
  Wakenya walifanya harakati za kutuzuia tusiuze hizi pembe,ulinzi wa hizi pembe unatugharimu kwa hiyo kama tumebuni mbinu ya kuziuza itakuwa safi sana.Tatizo ni kwamba hela za mauzo zikishindwa kuingia serikalini.
  Hebu jaribu kuwa great thinker na sio mropokaji tu.asssssss hole!
   
 16. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #16
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Unajua when you are not serious hata subordinates wako nao watakukejeli!
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Apr 29, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,320
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  Hii nchi mpango mzima ni wizi tu hakuna deal nyingine?
   
 18. M

  Mchomamoto Senior Member

  #18
  Apr 29, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuhusu kutolewa ghalani inawezekana kabisa kuna watu wanafanya mchezo huo, lakini hilo la kutopigwa mihuri sehemu ya kati sio kweli meno mengine hupigwa hata kati inategemea na aliyekuwa anagonga mihuri husika. Nina utaalamu na mambo ya wanyampori.
   
 19. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #19
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nasikia kizunguzungu yaan kila kukicha unasikia hiki mara kile hivi tumelogwa na nani?Jamani hivi mkitembelea nchi za wenzetu hamuoni maendeleo na jinsi watu wanavyopenda nchi zao?Tunaishi kupia picha tu na kupost kwenye Blogs na FB.
   
 20. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #20
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
Loading...