Wizara ya Maliasili na Utalii bado ni tatizo

Upekuzi101

Senior Member
Aug 28, 2020
134
348
Kati ya wizara ilokosa maono na mwelekeo wa kimkakati ni wizara ya Mali Asili na utalii. Pamoja na kuwa wazito katika kukabiliana na majanga kama moto na uharibifu wa mindo mbinu hifadhini bado stragestist hakuna katika hii wizara.

Hivi sasa Kuna mkakati wanataka kuupitisha bila kushirikiana na wadau ikiwepo swala la kuongeza siku katika route za kupanda mlima.

Pamoja na kulipitisha swala hilo, wamesahau ni wageni wangapi tayari wameshabook packages na kulipa wameshalipa kwa hiyo utamuambiaje mgeni aliyelipa siku 6 Marangu route kwamba iyo route siyo ya siku 6 tena eti imefanyiwa siku 7 just tu kwa malengo ya kujiongezea tu makusanyo.

Kimsingi hakuna haja ya kuongeza siku kwenye route yoyote, zaidi wangekuja na mkakati wa kuandaa route fupi zaidi kama siku 3 au siku 4 ili kuvutia mountaineers huko dunia Kuja Tanzania to try something new.

Waziri wa Mali Asili najua ni mgeni kwenye hii wizara ila jaribu sana kuhusisha wadau wa utalii katika kila jambo unalotaka kulifanya ili upate mawazo sahihi maana wadau wengi wa utalii ni kama wametengwa tu, maamuzi yanatoka huko juu yanaishia kutelezwa bila maslahi yoyote ya msingi zaidi mambo yanafanywa kwa mihemko na hisia za watu wa chache wanaojiita big fish.

Zaidi waziri tunaomba uisome wizara vizuri ili mwisho wa siku uweze kuongea lugha moja na wana utalii, vinginevyo muda wako utaisha bila kufanya lolote la msingi.

Mwezako Kigwangala pamoja na madhaifu yake aliwezakuacha alama kwenye wizara hii kwa kushusha gharama za Leseni kutoka 2000$ hadi 500$ na haya yalikuwa mawazo mazuri na ushauri kutoka kwa wadau wa utalii.

IMG-20230405-WA0008.jpg
 
Katibu Mkuu anaacha kuongea na wadau wa Utalii namna bora ya kutangaza Utalii kimataifa anaenda kuonana na Diamond Platinum eti kujadili "Tanzania unforgettable".

Sasa Mond anaelewa nini masuala ya Utalii!

Kuna Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii aliyeteuliwa juzi,mbona naye hatujamsikia kulonga na wadau wa Utalii au na yeye ni walewale!

Nchi ngumu sana hii!!!
 
Back
Top Bottom