kumuhusisha mwakyembe na juice ya magogoni sidhani kama ni sahihi,maana kama ishu yake mkubwa amehusika asingekuwa naibu waziri mpaka sasa katika hali yake ile ya ugonjwa,the same to mwandosya.kwa hili mkulu mnamsingizia wadau.mimi sioni kama juice ya magogoni na kashata zile zina madhara!mbona makamanda walizipiga lakini fresh tu mpaka leo?
Halafu msiwasifu sana hao madaktari wakati wengine hapo imeshakuwa gumzo kuingia ikulu,tena mmoja kapost picha fb akipeana mkono na mkulu!!hamna lolote na juice wamekunywa sana tu sema mkutano wao ulikuwa ni closed-meeting ndiyo maana picha zipo chache!!hebu jiaminini nyie nani awawekee sumu kwenye vinywaji,kwa titlle gani mliyonayo na chuki gani ya mkulu juu yenu??
kama ni hivyo basi next time wawe makini hata na makochi maana yanaweza kuwa zaidi ya juice
Kilaza kweli wewe, watu wanapanga mipango ya kununua nchi we unaongelea ushawishi wa kukaa siku nne?Wamekunywa na kula na walipotoka hapo kimyaaa, hawajapata usingizi waliyoyakuta huko. Wanajuuta kwenda Ikulu, lakini ndio wametia adabu wameelewa huko kuna vichwa.
Huko wamesha Mkonvinsi Rais wa US aake Tanzania siku 4 wakati hakuna aliyewahi kukaa masaa 24? unafanya mchezo. Huko kuna vichwa vilivyi konvinsi white house ya US kuwa Rais wa kwanza kuingia Ikulu katika awamu mpya atakuwa ni kutoka hapo Ikulu. Unafanya mchezo?
Kilaza kweli wewe, watu wanapanga mipango ya kununua nchi we unaongelea ushawishi wa kukaa siku nne?
mgomo wao wa pili walisema watarudi kazini na vile vile kuendelea na mazungumzo na serikali mpaka waziri na naibu wake wa wizara ya afya waondolewe,vinginevyo wataendelea na mgomo usio na kikomo.Wameonana na Rais na wamekubali kusitisha mgomo,na katika taarifa yao kwa vyombo vya habari hawakuonesha kama walizungumzia suala la mawaziri hao.Somo taarifa yao kwa vyombo vya habari.jiulize walikwenda ikulu kwa madai mengine au lile kusudio la mgomo la mawaziri waondolewe? au kuingia ikulu na kumuona rais live? au kunywa juice na sambusa?Mnadanganyana hawakunywa juice,tatizo watoto wa shule wengi JF siku hizi.Waulizeni kama walijaadili suala la mawaziri mbele ya rais...acha kuropoka kama hujui kaa kimya kwani lazima na wewe u post
Nawashukuru sana wachangiaji hapa JF. Hili la madokta linawahusu wote tanzania, bila kujali itikadi ya chama au dini
Mimi sio Dokta. Nimepata uchungu sana jinsi sekta ya afya ilivyodorora hapa Tanzania. Pili Kumbuka kwamba Tanzania ina madokta wachache sana duniani. Sasa kuna motisha gani ili wanafunzi wasome PCB?
Kama wanafunzi wenyewe wako secondari wanaona madokta wanafanya kazi katika mazingira duni, vifaa hospitalini hakuna, mishahara duni, madokta hawana nyumba, Je wanafunzi watapenda sayansi?? Wanafunzi si wataona hamna haja ya kuumiza kichwa.
Wanafunzi watachepuka kwenye EGM, PGM, COmmerce na HGL ili waje kulipwa unono. na Hivyo Tanzania itazidi kukosa madokta na huduma za afya zitazidi kudorora.
Vile vile bila afya bora mtu atafanya kazi? je kama unaumwa utafanya kazi. Kama watu wanaumwa na hawapati huduma bora za afya watafanya kazi. Uchumi utazidi kudorora.
Nawapongeza Madokta kwa ujasiri na kutumia akili zao Mungu alizo wajalia. Madokta sio kama waalimu. Waalimu ni wanafiki, wanafanya mgomo baridi halafu wanafunzi wanafeli sana.
Waalimu amkeni, daini vifaa vya maabara katika secondari zote, daini mabweni ili wanafunzi watulie wasome. Daini nyumba za waalimu. Walimu daini mishahara.
Angalia mashirika mengine ya Umma yasio na umuhimu kuliko Afya na elimu wanavyotafuna kodi na rasilimali za nchi.
TANAPA, TRA, Bandari, Matraffic, TISS, JWTZ (maafisa), NSSF, PPF, SUMATRA, EWURA.
Teh teh--- Nyumbani kwa baba hapaaminiki ee!