madocs ya mitumba halahala na wake zetu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

madocs ya mitumba halahala na wake zetu!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by kipindupindu, Nov 2, 2011.

 1. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wakuu habari za usiku.kwa mara ya kwanza leo hii nimeamua kuongozana na mwenzi wangu na mke wangu mpendwa ili nikajionee sehemu anayonunulia vi-top,skin jeans,mapande manane na vimin skirts vya mtumba. Si mnajua vimwana wa kisasa wanajipendezesha kutoka kwenye viduka vidogo vya mitumba al-maarufu 'madocs'

  Kwenye kiduka nilichoingia nimekutana na pazia linalogawa kachumba haka kadogo ktk sehemu mbili. Sehemu ya ndani kuna kioo kikubwa cha kujitazama, hapa ndipo wenzi wetu wa kike husaula na kubaki na nguo ya ndani (chupi na sidiria) ili kujaribisha nguo wanazotaka kununua.

  Cha kushangaza na kushtusha utakuta mteja anabadilisha nguo kadhaa huku jamaa la kiume au kijana rijali(muuzaji) akimtazama miguu na kilichowatenganisha ni pazia ambalo upepo wa kaskazi ukivuma laweza kupepea na kuondoa usiri uliopo.

  Yaani leo nimefikiria mengi kwa sababu mke wangu hakuonyesha kuwa na wasiwasi au uwoga wowote kwa kaka muuzaji ambaye ni brazaman ile mbaya. Yaani anamuamini kama mgonjwa wa kike anavyomuheshimu daktari wa kiume.

  Nimejionea mengi ya kutilia shaka lakini kwa leo niishie hapa ili niwaachie wadada na wakaka wa jamvi hili tujadili jambo hili.
  hivi ni kweli kinadada mnatoka salama kwenye haya madocs bila kunanihii?
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  kwa nini asitoke salama? Akigawa kapenda mwenyewe. Ila kuna sehemu waachie wenyewe waende aisee presha inaweza ikapanda na kushuka kwa wakati mmoja
   
 3. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kumbuka jamaa anaangalia miguu na kuona skirts zinavyodondoshwa na kupandishwa.hapandwi na mihemuko?
   
 4. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  sasa wewe umeona anaona miguu tuu....
  kule ndani huwa kuna kioo....na hilo pazia linakuwa na viupenyo kidogo pembeni....kwa hiyo huyo bwana akiwa nje ...kupitia upenyo wa pazia anamuona mtu vizuri kuanzia anapochojoa nguo mpaka mwisho kupitia kwenye kioo....stuka jombaaa
   
 5. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  preta kuna mengi nimeyaona,sikanyagi tena kwenye madocs!
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mhhhhhhhhhh ukimchunguza kuku humli......

  wengi wanalambwa aisee.....believe me....anaijaribisha nguo,anatazama ilivyompendeza
  halafu muuza mitumba anakataa kushusha bei...so mwisho wanaelewana tu...

  but hivi kuna sababu gani ya kuvaa mitumba siku hizi ambapo kuna nguo za kichina za bei nafuu???mpya?????
   
 7. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #7
  Nov 2, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kuna mambo mengi ya muhimu ya kutilia shaka wakuu... Haya madogo madogo tuyapotezee
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  kuna madocs ya kinondoni nasikia yana magodoro kabisa. Dah!
   
 9. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  hayo sio madogo wewe. Kama una kamchumba hakajatulia tulia halafu wewe uwezo wa kumpigisha pamba huna ila kila siku yupo kwenye madoc inabidi ustuke.
   
 10. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  usiwe unaenda kila mahali na mamsapu....utapata wazimu....
   
 11. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #11
  Nov 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  yah...si unajua ukijaribisha skin jeans inahitajika msaada...au wewe Husninyo skin jeans zako huwa unanunulia wapi....
   
 12. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #12
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  nyie watu nyie kwanini mnapenda sana kununua presha
   
 13. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #13
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  akili za baadhi ya wanawake nii pasua kichwa..

  wauza mitumba
  wauza nyma buchani
  na madereva taxi....ukiwachunguza utatukana wanawake aisee....
   
 14. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #14
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  nanunua huko huko kwenye madocs. Kitu kavaa rihanna! Lol
   
 15. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #15
  Nov 2, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  leo nimejifunza ila baby kalazimisha sana nikaona sio mbaya tukaenda halafu achague ili mzee nizame deep deeper in my wallet!
   
 16. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #16
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  dah hii kali hata kama lazima uwe na wendawazimu kugawa hivo unagawaje
   
 17. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #17
  Nov 2, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kaka hili sio dogo mimi nilidhani ni dr tu naweza mwamini kwa mke wangu lakini duh wapo madokta wengi mjini!
   
 18. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #18
  Nov 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  sasa je...Boss anasema tuvae za kichina.....angejua ukimuona mwenzio kavaa top kama yako unatamani kuivua asingetushauri....
  sitaki kabisa kumuona mtu kavaa nguo inayofanana na yangu halafu tupo sehemu moja....
   
 19. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #19
  Nov 2, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  za kichina waachieni mahousegirl!
   
 20. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #20
  Nov 2, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,252
  Trophy Points: 280
  Je botike masaloon ya wakongo man na wanawawekea kusha urembo wakati mguu wa mmusapu wako kauweka kwenye paja la mkongoman!! we acha ukiangalia hayo utakuja kuzimika kama mshumaa wakongo man ni noma kwa wadada kinachotakiwa ni dada mwenyewe kujitambua kuwa yupo kwenye mahusiano!!na ni mali yamhusika lasivyo usiguse!
   
Loading...